Ha ha ha, story za Muhongo ni kama za kwenye vitabu, huwa hayuko realistic kabisa.
Last time alisema Tanzania itazalisha umeme mwingi na mwingine utauzwa nje, leo karudi nafasi ile ile kaja na kuomba wawekezaji wazalishe ili waiuzie Tanesco umeme.
Sasa najiuliza, vile vyanzo vya umeme alivyotarajia kwamba vingezalisha umeme mpaka wa kuuza nje vimeenda wapi? Ilikuwa vya kufikirika?
Na unawezaje kuja na hesabu ya eti mpaka baada ya miaka mitano tutakuwa na MW 10,000 kutoka chini ya MW 1,500 tulizonazo leo wakati wewe siyo mzalishaji? Unategemea mwingine azalishe wewe ununue, asipozalisha au akazalisha kwa kiwango chini ya hitaji inakuwaje?
Eti umeme utakuwa wa bei ya chini wakati uzalishaji hufanyi wewe, anazalisha mwingine anakuuzia, na kwa sababu nature ya bidhaa husika siyo ile unaweza sema ngoja niachane na huyu niende duka lile pale, ni either ununue au uache usiwe na umeme.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.