Prof. Muhongo anafaa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania!

Leo nimefarijika sana kupata wziri Kama Prof Muhongo ambaye ni shujaa, kazi zake zinaonekana kabisa hana ubia na mafisadi Napendekeza liwalo na liwe apigwe chini, Prof. Muhongo aendeshe jahazi linalozama TUJADILI HOJA HII

Funguka zaidi kaka kakukosha na lipi ndugu.
 
Arvin Slaone,

Kikweli hata kama akija kufanana na wenzie, tayari atakuwa amesha iweka nchi hatua moja mbele; Ngeleja na malima hata wangekaa miaka mia katika wizara hii wasingefikia alipofikia leo Prof Muhongo kwa muda huu mchache tu.

Fuatailia wawekezaji wa madini, sasa wanalipishwa viporo vyote, na kuiboresha mikataba, hii inatokana na mikakati ya hawa mabwana. Kuna wakati hawa wawekezaji wanazuiwa ku'export, mpaka walipie kiporo na hamna longo....! Take it from me.......!

Kibanga Msese
 
Wasiojua watamsubiri sana awe mwanasiasa, hilo halipo, yule si mwanasiasa na anasimamia ukweli muda wote. Hana muda huo, lile jembe!
 
Leo nimefarijika sana kupata wziri Kama Prof Muhongo ambaye ni shujaa, kazi zake zinaonekana kabisa hana ubia na mafisadi Napendekeza liwalo na liwe apigwe chini, Prof. Muhongo aendeshe jahazi linalozama TUJADILI HOJA HII

Ushauri wangu ni kuwa kama kweli mmefurahishwa na utendaji kazi wa Prof Muhongo basi nashauri sifa hizi artificial tuziache tumpe muda. Otherwise tunaweza kuwa tunampalia makaa na makundi yanayowania urais, au hata yeye mwenyewe akalewa sifa na kulitotesha!
 
Hata msanii DHAIFU watu wakathubutu kumuita "chaguo la Mungu" na kauli zake zilizokonga nyoyo za Watanzania, "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana." "Tutaipitia tena mikataba yetu ya uchimbaji wa dhahabu ili iwe na maslahi kwa Watanzania." lakini miaka saba baadaye tumegundua jamaa ni hopeless kabisa.

Waziri mpya wa Madini na Nishati katoa kauli kwamba makampuni yote ambayo yamekuwa yakichimba madini nchini kwa miaka mitano au zaidi yaanze kulipa kodi ya 30% mara moja bila excuses za aina yoyote vinginevyo wafunge migodi warudi kwao. Sasa tuone ufuatiliaji wake katika hili.

Je, speed yake itazuiliwa na mafisadi ndani ya Serikali ambao wameshanunuliwa na makampuni hayo na kupewa shares nyingi sana au makampuni hayo yataamua kumnunua ili kumnyamazisha?

Ndugu zangu hawa wanasiasa huwa hawatabiriki.
Watu walikuwa na imani sana na 'mtoto wa mkulima' Pinda lakini mwisho wa siku amekuwa hopeless.
 
Ukweli ni huu...Hizi sifa mnazompa Prof Muhongo,kama ni kweli aliupata ubunge kwa kuteuliwa,basi sifa hizo lazima pia zimwendee JK.Zisipomwendea JK,hatofika mbali.Na pia kama JK naye ana any direct or even indirect interest on the matter.
 
abaki kwenye hii wizara aisafishe kwanza watu tunateseke sana na hii wizara
Wakuu mimi nimependa hiyo style ya public hearing badala ya kuwa na tume kibao. na nimempenda kukiri kwake kuwa hata bodi ya Tanesco iko mbioni kuvunjwa maana nayo ina matatizo. He looks sincere. cha muhimu JK amuunge mkono hata kama ni kwa kuvizia kama anavyofanya kwa Nape.
 
Leo nimefarijika sana kupata wziri Kama Prof Muhongo ambaye ni shujaa, kazi zake zinaonekana kabisa hana ubia na mafisadi Napendekeza liwalo na liwe apigwe chini, Prof. Muhongo aendeshe jahazi linalozama TUJADILI HOJA HII
Yaani kwa siku moja tu mtu unamjudge kuwa pm kwa hivyo vigezo? kesho si utasema awe Rais? kuongea ni tofauti na kutekeleza mkuu labda uje na hoja nyingine mi naona wote wameoza tu.
 
Mkuu huyu prof.. anafaa kuwa RAIS wa nchi. Nafasi hii aliyonayo sasa lazima atapata vikwazo tu toka kwa mafisadi walio ndani ya chama chake
 
just matther of time ..atafanana na wenzake soon

keep on dreaming!......hii ni mashine nyingine aisee.........na ndio maana nilipoona jina lake limeteuliwa na JK sikusita kumpa HONGERA JK kwa kulamba dume........
 
Leo nimefarijika sana kupata wziri Kama Prof Muhongo ambaye ni shujaa, kazi zake zinaonekana kabisa hana ubia na mafisadi Napendekeza liwalo na liwe apigwe chini, Prof. Muhongo aendeshe jahazi linalozama TUJADILI HOJA HII

watanzania ni watu wanaodananyika kirahisi sana na ii ndo inapelekea siku zote kuwa na watu dhaifu ,viongozi dhaifu kwa sababu ya fikra nyepesi nyepesi kama hizi
 
Leo nimefarijika sana kupata wziri Kama Prof Muhongo ambaye ni shujaa, kazi zake zinaonekana kabisa hana ubia na mafisadi Napendekeza liwalo na liwe apigwe chini, Prof. Muhongo aendeshe jahazi linalozama TUJADILI HOJA HII

kiongozi hiyo ni dharau kwa nafasi ya waziri mkuu. Huwezi kumpima mtu anaefaa kuwa kiongozi wa ngazi ya pm kwa kusikiliza majibu yake ya siku moja tu.
 
Back
Top Bottom