Prof. Muhongo ammaliza rasmi Mhando; Mama Rwakatare naye alipuliwa!

Mama Mdogo

Ni kweli Prof Muhongo ni jembe la ukweli tatizo ni mifumo yetu haikawii kumweka kando.We subiri atatifutiwa zengwe la kufa mtu.

kaka wapiga zengwe wametibua mengine yanawahangaisha sasa hivi. Mpaka wakae sawa jamaa ameshaonyesha njia...siku hizi sio kama zamani. mambo yakiwa hadharani kuyazima inataka uwe na moyo wa chuma.
 
Acha kusifia ujinga, wizi wa umeme ni operational risk ambayo iko incorporated kwenye performance ya Tanesco, wizi wa umeme sio unaosababisha Tanesco kushindwa kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi, hii mambo ya kutaja taja watu majina imeonekana kuwa ni Performance indicator kwa wanasiasa wetu siku za karibuni.

Anaweza kutueleza hao watu wameishachukuliwa hatua gani za kisheria mpaka sasa? kuna taarifa zozote zimetolewa polisi kuhusu wezi hawa? anaenda kuwataja majina bungeni ili iweje? Kwamba senti meris wanaiba umeme, well, umeme kiasi gani wanatumia senti meris zaidi ya kuwasha kwa ajili ya vijana wetu kusoma? au hajui kwamba hata Serikali kutokulipa bili za umeme na bado haichukuliwi hatua zozote zile inasababishwa na conflict of interest? au anadhani hatujui serikali ndio mdeni mkubwa wa tanesco.

waziri anaenda kutaja wezi majina badala ya kutupa realistic road map ya upatikanaji umeme wa uhakika na wa nafuu??

Bila shaka utakua mume wa mchungaji Rwakatare!
 
Nimesikia mtaani kwetu kwamba wabunge walioomba rushwa kwa Maswi ni Ole Sendeka na Anna Kilango Malecela.
Kwenye matairi nimesikia likitajwa jina la Lucy Msafiri-huyu nadhani ni mbunge mstaafu.

Ndo maana jamaa bado anang'ang'ania kuwa waliokiuka sheria za manunuzi kwa kisingizio cha bei wawajibishwe. Huyu jamaa sasa amejishushia hadhi aliyokuwa nayo mbele ya jamii.
 
Yani misumari ikaagizwa kwasababu ni bei rahisi,ni sababu tu ya kutafuna pesa "nyingi" za spare parts,kweli I'm no longer proud to be a Tanzanian!
 
Yeye aliye mwaminifu 100% na awe wa kwanza kumhukumu Rwakatare. Simtetei na sina shirika naye, lakini yaelekea hapa anatwishwa mzigo usio wake. Ujambazi wa mpangaji unamhusu vipi mwenye nyumba? Hizo shule si zina wakurugenzi wake? Wapelekwe kwenye sheria na watakuwa wanamsaidia Rwakatare. Ndio maana JK analaumiwa sana kwa makosa wanayofanya wasaidizi wake, hiyo sio haki hata kidogo. Nitaiita hiyo ni husda! Au vipi?

Mh Rwakatare na wakurugenzi wake wote marikanyanga!
 
Mmh ufisadi huu utaisha lini kila mahali ufisadi .afya, elimu,maji,kilimo kwanza imekuwa kilimo mwisho.mama tilie akienda kukopa benki laki5 kupewa mkopo huo hadi atoe lak2.taifa letu ninazidi kuzama kulirudisha kwenye msingi lina hitaji Rais asiye cheka na mafisadi
 
Kuna wakati nilikuwa nina mazoea kuhudhuria ibada Mikocheni B Assembless of God.
Sasa kuna mgeni mmoja,wakati wa kukaribisha wageni,aliposimama ,alijitambulisha kuwa ni kiongozi wa CHADEMA kutoka Kigoma.Nakumbuka dokta mh.mch.alim interrupt na jamaa akaa chini kwa unyonge.
Kuna wakati,mch.dkt.mh.aliwahi kumwita madhabahuni muumini wake Patrick Tsere,wakati huo mkuu wa Wilaya ya Ilaya ,pamoja na mkewe kwa ajili ya maombi.Kisa!Ili Mungu atende muujiza kwa kesi ya uchaguzi iliyofunguliwa na Tsere,na ambayo hukumu ilikuwa itolewe wiki inaypfuata.Ikumbukwe Tsere alishindwa katika uchaguzi wa ubunge na dokta Slaa katika jimbo la Karatu!!Nakumbuka wakati watu wanaomba mimi nilitoa pipi mfukoni na kuanza kutafuna!!
Hapo nikaelewa sikuwa mahali sahihi..Kifupi pale kanisani Mikocheni ni kama kitengo cha CCM na serikal
i
 
....................................
Jamani huyu mama si ndo yule Mchungaji wa kanisa kubwa hapa Dar es Salaam..!!??
....................................

Sijui Waumini wake huwa wanenda kufanya nini kwa mwizi huyu...hana maadili kabisa ....
1. Ndoa Tatizo kwake na watoto wake
2. Wizi wa Umeme


Je tujifunze nini toka kwa huyu mchungaji na Mbunge? hawa ndio kondoo wenye ngozi Chui
 
Mama mchungaji alikuwa anaiponda sana JF kule mjengoni, hadi anamuomba waziri aifungie isiwe tena hewani! Kumbe mchungaji G. Rwakatare ni MWIZI wa umeme? Kwa taarifa yako Jf hawadaiwi bili ya umeme.
 
quote_icon.png
By Mama Mdogo

Kwa hesabu zangu za haraka haraka 1 Prof Muhongo = 1,000 * (Ngeleja+Karamagi+Malima+Yona). Yaani ukichanganya akina Ngeleja, Karamagi, Malima na Yona; ndipo umpai busara na juhudi zao uzizidishe mara elf ndipo umpate 1 Prof Muhongo. Keep it up Pro Muhongo, Mwenyezi Mungu akujalie maisha mema, inabidi ujichunge usizoeane na mafisadi na washirika wao wasije wakakudhuru!!!!
Bi mdogo hako hako ka formula kako kanamshushia hadhi professor wa watu. Ngeleja+Karamagi+Malima+Yona = 100% Uoza. Inawezekana kweli 1 Prof Muhongo = 1,000*Uoza ??
 
Hiki kibabu Mwinyi ndio kimetuletea haya matatizo yooote. Na ukiangalia hawa MAFISADI na UFISADI wote ni matunda ya uongozi wake. Mwinyi ndio mwanzilishi wa UFISADI na familia yake. Watanzania tulipumbazwa sana na enzi za "RUKSA", sasa tunaona joto ya jiwe. Haya ndio matokeo ya serikali lege lege na DHAIFU iliyoanzishwa na Utawala wa A.H Mwinyi.

ndugu zanguni, matatizo ya tanesco yameanza wakati wa utawala wa Mzee ruksa(awamu ya pili), tutanyoosheana vidole na kusutana sana ila waliotuingiza kakika hil janga wapo pembeni,wanaomba na kutambikia, watu wasi recall back ili wasijekuwa answerable,tatizo si Mhando,Ngereja,Maswi.Mhongo, wapo wahusika wamejificha kwa kifupi tu,

1.tatizo lianza pale tulipoanza kufunga mikataba ya kitapeli kwa kuanza na (IPTL). kwa wanaokumbuka vizuri, kuna wakati gazeti la "Rai", wakati ule bado liko chini ya Jenerali Ulimwengu, lilianza kuchapisha report ya uchunguzi wa mwandishi wa kimataifa, jina nimemsahau.. kuhusu sakata zima,kuazia mwanzo mpaka mkataba wa kifisadi wa IPTL, ile report ilchapwa katika matoleo mawili tu alafu ikakatishwa, haijawahi kuchapishwa tena, tuitafute hiyo report tuisome, na tuipeleke bungeni ijadiliwe, tutajua ni akina nani walingiza taifa katika kadhia hii. na wahusika wachukuliwe hatua, wakati huo tujipange kuanza upya

2.baadaye mikataba mibovu ilyosainiwa wakati wa awamu ya nne ya (Benjamin Mkapa) na awamu hii ya nne ya (JK) ambayo ni " NET GROUP SOLUTION,AGGREKO SONGAS, DOWANNS-RICHMONDNDO,KIWIRA" imegonga msumari wa mwisho katika jeneza la Tanesco,

hawa wanasiasa wasitake kutusahaulisha, madhambi yao ya kinyonyaji, lazima tuendelee kuhoji uhalali wa mikataba mibova kama hii mpaka hapo wahusika watakapochuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na kunyongwa kwa gharama zao, na kufilisiwa mali zao zote, vinginevyo hatukubali kudangawa na porojo za bungeni, wakati tatizo mama linajulikana

nahitimisha kwa kusema kwamba ilishatabiriwa na wachumi mahiri huko nyuma ya kuwa kwa mikataba hii kuanzia mwaka 1995 tuna miaka takribani 25 ya kutaabika kiuchumi, na sioni dalili za tanesco kuimarika hivi karibuni,achaneni na porojo za wanasiasa, zipo tafiti za kichumi zinazoeleza tatizo

naunga mkono mwana JF
 
ndugu zanguni, matatizo ya tanesco yameanza wakati wa utawala wa Mzee ruksa(awamu ya pili), tutanyoosheana vidole na kusutana sana ila waliotuingiza kakika hil janga wapo pembeni,wanaomba na kutambikia, watu wasi recall back ili wasijekuwa answerable,tatizo si Mhando,Ngereja,Maswi.Mhongo, wapo wahusika wamejificha kwa kifupi tu,

1.tatizo lianza pale tulipoanza kufunga mikataba ya kitapeli kwa kuanza na (IPTL). kwa wanaokumbuka vizuri, kuna wakati gazeti la "Rai", wakati ule bado liko chini ya Jenerali Ulimwengu, lilianza kuchapisha report ya uchunguzi wa mwandishi wa kimataifa, jina nimemsahau.. kuhusu skata zima,kuazia mwanzo mpaka mkataba wa kifisadi wa IPTL, ile report ilchapwa katika matoleo mawili tu alafu ikakatishwa, haijawahi kuchapishwa tena, tuitafute hiyo report tuisome, na tuipeleke bungeni ijadiliwe, tutajua ni akina nani walingiza taifa katika kadhia hii. na wahusika wachukuliwe hatua, wakati huo tujipange kuanza upya

2.baadaye mikataba mibovu ilyosainiwa wakati wa awamu ya nne ya (Benjamin Mkapa) na awamu hii ya nne ya (JK) ambayo ni " NET GROUP SOLUTION,AGGREKO SONGAS, DOWANNS-RICHMONDNDO,KIWIRA" imegonga msumari wa mwisho katika jeneza la Tanesco,

hawa wanasiasa wasitake kutusahaulisha, madhambi yao ya kinyonyaji, lazima tuendelee kuhoji uhalali wa mikataba mibova kama hii mpaka hapo wahusika watakapochuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na kunyongwa kwa gharama zao nakufilisiwa mali zao zote vinginevyo hatukubali kudangaw na porojo za bungeni, wakati tatizo mama linajulikana

hahitimisha kwa kusema kwamba ilishatabiriwa na wachumi mahiri huko nyuma ya kuwa kwa mikataba hii kuanzia mwaka 1995 tuna miaka takribani 25 ya kutaabika kiuchumi, na sioni dalili za tanesco kuimarika hivi karibuni,achanaeni na porojo za wanasiasa, zipo tafiti za kichumi zinzoeleza tatizo

naunga mkono mwana JF
Hiyo ni Nishati tu , hatujaenda kwenye madini. Hii ngozi nyeusi hii sijui nani aliiloga...
 
inaweza kuchukua miaka zaidi ya 50 kumpika Profesa Muhongo na inachukua miaka 25 kumpika Mr Ngeleja

Mimi naona inaweza kuchukua miaka zaidi ya 50 kumpika Profesa Muhongo lakini huhitaji gharama yoyote kumpata kiongozi wa level ya Mr Ngeleja, Mr Maige, Mr Yona, Mr Karamagi and other fisadis. I think that, you need a class of 1,000 students to get a leader of a caliber of Prof Muhongo; but only a class of 2 students to get a corrupt leader of a caliber of Mr Ngeleja, Mr Maige, Mr Yona, Mr Karamagi and other fisadis. Kudadeki.
 
Jamanimwenye taarifa sahihi za wabunge wanaotuhumiwa kuihujumu Tanesco,mwenzenu sijui,nimeona jina moja hapa la Lucy Msafiri,nani mwingine?wenye taarifa jamani tuwekeeni hapa,maana kusubiri kamati ya maadili ikae wanaweza kulipotezea jambo hili.wekeni majina yao tuwajue
 
Mimi naona inaweza kuchukua miaka zaidi ya 50 kumpika Profesa Muhongo lakini huhitaji gharama yoyote kumpata kiongozi wa level ya Mr Ngeleja, Mr Maige, Mr Yona, Mr Karamagi and other fisadis. I think that, you need a class of 1,000 students to get a leader of a caliber of Prof Muhongo; but only a class of 2 students to get a corrupt leader of a caliber of Mr Ngeleja, Mr Maige, Mr Yona, Mr Karamagi and other fisadis. Kudadeki.


hahahaaa, inamaana majority ya watanzania ni wala rushwa/fisadi
 
Eeeh Mungu mwingi wa baraka na rehema tunusuru sisi waja wako. Duuuuuuh!!!!! Hili suala la WIZI na UFISADI inawezekana ni janga kubwa la maafa zaidi ya tunavyofikiria WATANZANIA.
TUTAYAONA NA KUSIKIA MENGI MPAKA IFIKAPO 2012. Eeeh MUNGU tunaomba uzima.

Hapo kwenye red nadhani unamaanisha 2015. Lakini nadhani walitajwa ni Visangara tu Hivi unadhani viwanda haviibi? Na je, vipi kuhusu Idara na taasisi za serikali ambazo ni wadaiwa Sugu? nadhani hao ni kafara kutuwekea attention kwao wakati wanafix kitu kingine.
 
Back
Top Bottom