Prof. Muhongo ammaliza rasmi Mhando; Mama Rwakatare naye alipuliwa!

Muhongo ni jembe lkn watu wema mara nyingi wanaundiwa zengwe,we subiri tu si umeona olesendeka alivyofanya?

Hakika chifu..huu ndiyo mtindo wa Tanzania ya sasa.

Nina wasiwasi pia na kasi ya NIDA..nao waweza kuundiwa zengwe...
 
Ajipime na si vibaya akaungama
Yeye aliye mwaminifu 100% na awe wa kwanza kumhukumu Rwakatare. Simtetei na sina shirika naye, lakini yaelekea hapa anatwishwa mzigo usio wake. Ujambazi wa mpangaji unamhusu vipi mwenye nyumba? Hizo shule si zina wakurugenzi wake? Wapelekwe kwenye sheria na watakuwa wanamsaidia Rwakatare. Ndio maana JK analaumiwa sana kwa makosa wanayofanya wasaidizi wake, hiyo sio haki hata kidogo. Nitaiita hiyo ni husda! Au vipi?
 
mmeshaanza ....
 
Maoni yangu ni kuwa Waziri Muhongo ni jembe aka kifaa; lakini ni bahati mbaya naona ana manaibu mawaziri kama wanapwaya sijui kama wataenda naye sawa huko mbele. Waziri yuko professional, muwazi na anaongea kwa uhakika; lakini Masele na Simbachamwene wanaonekana siyo professional na siyo wawazi. Cha pili, ni kwa nini wabunge zaidi ya watatu wameomba watajwe wale wahujumu wa Tanesco (walioomba rushwa kwa Maswi, waliouza matairi mabovu, wanaofanya biashara zingine na Tanesco). Kuna mwana JF / mtu ana hayo majina ayataje hapa, where we dare to speak openly!!! Natoa hoja.
 
Mch. Getrude Rwakatare ana mume Lakini Hataki Kukaa naye ila yeye ni Mshauli wa Ndoa Angalia Hapa yupo na Mumewe Mlimani City !!!!!!!!!!!!!!!!!

rwakatare.JPG
Pichani anaonekana Mchungaji Dr Getrude Rwakatare kulia akiwa na mumewe wakati wa harusi ya mtoto wao wa mwisho Bw Mutta Rwakatare alipokuwa akifunga ndoa siku ya juzi jumamosi tarehe 26.05.2012.Ndoa ilifungwa katika kanisa la Mikocheni na Harusi ilifanyika katika ukumbi wa Mlimani City.

Hivi haya madudu akina Ngeleja/Malima walikuwa hawayajui au waliuchuna tu kwa sababu na wenyewe wana tumirija twao humo?
 
Amesema kuwa St Mary Secondary Schools za Mheshimiwa Rev Rwakatare ni mojawapo wa wezi wa umeme wa Tanesco, wameiba jumla ya Tshs millioni 10 plus.

Shame on you Mheshimiwa Rev Rwakatare.

Huyu mama kwa kweli, mhhhhhhhhhhhhhhh! Maana shule zake inasemekana zimeajiri walimu wasio na vibali vya kufanyakazi kutoka nje ya nchi huku wakillipwa ujira mdogo maana hawawezi kupiga kelele. Michango ya wafanyakazi wake hapeleki NSSF na ni vinara wa kuwahonga wakaguzi ili waandikiwe ripoti safi, na hili tena la umeme. Toooooooooooooo baaaaaaaaaaaaaaaad kwa kweli.
 
mkuu mbwa wa jirani akikuibia utamshitaki mbwa au mwenye mbwa.?
Hilo nalo ni neno. Ndio maana hata Bungeni hoja za msingi za wapinzani huachwa na badala yake speaker anangojea Wheep wa ccm na accm wengine waombe mwongozo kuhusu spell mistakes na mifano iliyotolewa na mtoa hotuba wa upinzani, mwishowe wanasahau walikuwa wanazungumzia hoja gani ya msingi. Patamu hapo. Hata padri akihubiri na akatoa mfano wa paka na panya wanavyokimbizana, waumini hushika sana mfano huo na hata waliokuwa wamelala usingizi huamka kucheka, lakini ukiwauliza neno la leo lilikuwa nini hupati jibu kirahisi mbali na sifa kwamba padri leo amehubiri vizuri sana. Kisa? Mfano wa paka na panya wanaofukuzana alioutoa ati umewafurahisha sana. Yaani, weacha tu.
 
Mama Mdogo

Ni kweli Prof Muhongo ni jembe la ukweli tatizo ni mifumo yetu haikawii kumweka kando.We subiri atatifutiwa zengwe la kufa mtu.

Maoni yangu ni kuwa Waziri Muhongo ni jembe aka kifaa; lakini ni bahati mbaya naona ana manaibu mawaziri kama wanapwaya sijui kama wataenda naye sawa huko mbele. Waziri yuko professional, muwazi na anaongea kwa uhakika; lakini Masele na Simbachamwene wanaonekana siyo professional na siyo wawazi. Cha pili, ni kwa nini wabunge zaidi ya watatu wameomba watajwe wale wahujumu wa Tanesco (walioomba rushwa kwa Maswi, waliouza matairi mabovu, wanaofanya biashara zingine na Tanesco). Kuna mwana JF / mtu ana hayo majina ayataje hapa, where we dare to speak openly!!! Natoa hoja.
 
Last edited by a moderator:
Hamna kitu. Hizo ndio benefits za kuwa Mkurugenzi bwana, solution ilikuwa kusitisha tenda tu sio kupolitisize namna hii.

Sidhani kama wewe ni mzalendo, huoni kwamba wizi kama huu hata kama ni mdogo ukiendekezwa utasambaa kiwa mkubwa? Sidhani kama uko serious!
 
Yeye aliye mwaminifu 100% na awe wa kwanza kumhukumu Rwakatare. Simtetei na sina shirika naye, lakini yaelekea hapa anatwishwa mzigo usio wake. Ujambazi wa mpangaji unamhusu vipi mwenye nyumba? Hizo shule si zina wakurugenzi wake? Wapelekwe kwenye sheria na watakuwa wanamsaidia Rwakatare. Ndio maana JK analaumiwa sana kwa makosa wanayofanya wasaidizi wake, hiyo sio haki hata kidogo. Nitaiita hiyo ni husda! Au vipi?

Mkuu kwani yeye (Mama) hajuwi analipa kiasi gani kwenye umeme? Haonyweshi hata risiti za malipo ya huo umeme? Kashfa ya hizi shule ni nyingi mno. Waliofanyakazi kwenye shule hizo wanafahamu maovu mengi yanayoendelea huko na mama anayafahamu. Kwa kifupi ni kuwa ili kuhakikisha maovu hayo yanaendelea mama ameajiri watu wasiowaaminifu katika nafasi nyeti kwa makusudi ili watoe rushwa na kufanya uhuni kama huu. Sitaki kuongea mengi hapa maana namheshimu "Mpakwa mafuta wa BWANA".
 
Maoni yangu ni kuwa Waziri Muhongo ni jembe aka kifaa; lakini ni bahati mbaya naona ana manaibu mawaziri kama wanapwaya sijui kama wataenda naye sawa huko mbele. Waziri yuko professional, muwazi na anaongea kwa uhakika; lakini Masele na Simbachamwene wanaonekana siyo professional na siyo wawazi. Cha pili, ni kwa nini wabunge zaidi ya watatu wameomba watajwe wale wahujumu wa Tanesco (walioomba rushwa kwa Maswi, waliouza matairi mabovu, wanaofanya biashara zingine na Tanesco). Kuna mwana JF / mtu ana hayo majina ayataje hapa, where we dare to speak openly!!! Natoa hoja.

Nimesikia mtaani kwetu kwamba wabunge walioomba rushwa kwa Maswi ni Ole Sendeka na Anna Kilango Malecela.
Kwenye matairi nimesikia likitajwa jina la Lucy Msafiri-huyu nadhani ni mbunge mstaafu.
 
Nafikiri kinachomsaidia Prof ni kuwa yeye hakuenda kujipendekeza kwa mtu. kwahiyo anajua kama mtu hatapenda anayofanya basi aachane naye arudi zake mlimani kufundisha. Kusema kweli ana wakati mgumu sana maana kuanzia kwenye manunuzi ya mafuta mpaka upatikanaji wa nishati, kuna watu wanakula kama hawana akili nzuri. Yeye anaweza kuwa kikwazo kwa wahusika na siushangai walipojipanga kumsambaratisha maana Muhando was one of theirs.

Mimi uwa nawashangaa maprofesa wa kitanzania ambao wanaingia katika siasa na haswa kupewa vyeo vikubwa vya kisiasa na utendaji. Wengi wao hawana guts za kusema inatosha na kuweka tools down na kurudi katika shughuli zao za zamani. Angalia Tibaijuka, Magembe, akina Kapuya, Mwandosya et al. walivyo na wanavyojidharirisha!

Subiri tuone huyo naye wa nishati na madini atafanya nini - akiwa na guts basi hachukui round hapo ataweka silaha chini na kurudi kutoa mihadhara. Lakini naye akiwa kama wenzake atadharirisha "uprofesa" wake kwa kutumiwa na vilaza katika serikali ya CCM.
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Mwanzoni nilikuwa najiuliza ni kwanini Rais J M Kikwete kaamua kumteua waziri wa Nishati na Madini nje ya wabunge wa CCM ?.Sasa nimeelewa sababu zake kwamba wabunge wangi wa CCM hawana uzalendo rushwa na tamaa ya madaraka ni sehemu ya utaratibu wao wa maisha ya kisiasa.Hakika zipo faida nyingi sana kama tukiweza kuwa na mawaziri ambao si wabunge.

Nyota ya Prof Muhongo ilianza kung'aa wakati wa uzinduzi wa bomba la gasi naomba kumnukuu "Tumepoteza sana kwenye migodi ya dhahabu nitahakikisha kwenye gesi watanzania tunafaidika" Hii statement si rahisi kuisikia ikitamkwa na kiongozi wa CCM. Tukipata mawaziri watatu kama Prof Muhongo hakika upo uwezekano taifa likaanza kusonga mbele.

Kwa hesabu zangu za haraka haraka 1 Prof Muhongo = 1,000 * (Ngeleja+Karamagi+Malima+Yona). Yaani ukichanganya akina Ngeleja, Karamagi, Malima na Yona; ndipo umpai busara na juhudi zao uzizidishe mara elf ndipo umpate 1 Prof Muhongo. Keep it up Pro Muhongo, Mwenyezi Mungu akujalie maisha mema, inabidi ujichunge usizoeane na mafisadi na washirika wao wasije wakakudhuru!!!!
 
Hivi haya madudu akina Ngeleja/Malima walikuwa hawayajui au waliuchuna tu kwa sababu na wenyewe wana tumirija twao humo?

Mkuu TANESCO ilishakuwa chaka la kuvunia pesa kwa viongozi wetu. Ngeleja likuwa pale kwa maslahi ya RA na alifahamu fika unyonyaji uliokuwa unaendelea pale. Kuna hii kampuni ya Sengerema something iliyopewa tender na TANESCO ya kusambaza nguzo, sijuwi ila huenda ikawa ya kwake. Kwahiyo pale kila mwenye nafasi aliweza kuunda kampuni yake na kujipa tenda ya mabilioni ya shilingi. Mhando naye kafika pale kaona uozo unaoendelea pale naye kaamua kuunda kampuni yake na mkewe kwa mtaji wa milioni 10 baada ya miezi 8 wanajipa tenda ya milioni 850, lol!
 
Mama Mdogo

Ni kweli Prof Muhongo ni jembe la ukweli tatizo ni mifumo yetu haikawii kumweka kando.We subiri atatifutiwa zengwe la kufa mtu.

Ngongo tayari mizengwe imeshaanza. Siumeona amehepa kihunzi cha kwanza, mhando alitaka kuondoka naye.
Sasa ajipange vilivyo kuwakabili wenye mirija yao Tanesco na kwenye madini.
 
Last edited by a moderator:
Kwa hesabu zangu za haraka haraka 1 Prof Muhongo = 1,000 * (Ngeleja+Karamagi+Malima+Yona). Yaani ukichanganya akina Ngeleja, Karamagi, Malima na Yona; ndipo umpai busara na juhudi zao uzizidishe mara elf ndipo umpate 1 Prof Muhongo. Keep it up Pro Muhongo, Mwenyezi Mungu akujalie maisha mema, inabidi ujichunge usizoeane na mafisadi na washirika wao wasije wakakudhuru!!!!

inaweza kuchukua miaka zaidi ya 50 kumpika Profesa Muhongo na inachukua miaka 25 kumpika Mr Ngeleja
 
Back
Top Bottom