Prof. Muhongo ammaliza rasmi Mhando; Mama Rwakatare naye alipuliwa!

Acha kusifia ujinga, wizi wa umeme ni operational risk ambayo iko incorporated kwenye performance ya Tanesco, wizi wa umeme sio unaosababisha Tanesco kushindwa kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi, hii mambo ya kutaja taja watu majina imeonekana kuwa ni Performance indicator kwa wanasiasa wetu siku za karibuni.

Anaweza kutueleza hao watu wameishachukuliwa hatua gani za kisheria mpaka sasa? kuna taarifa zozote zimetolewa polisi kuhusu wezi hawa? anaenda kuwataja majina bungeni ili iweje? Kwamba senti meris wanaiba umeme, well, umeme kiasi gani wanatumia senti meris zaidi ya kuwasha kwa ajili ya vijana wetu kusoma? au hajui kwamba hata Serikali kutokulipa bili za umeme na bado haichukuliwi hatua zozote zile inasababishwa na conflict of interest? au anadhani hatujui serikali ndio mdeni mkubwa wa tanesco.

waziri anaenda kutaja wezi majina badala ya kutupa realistic road map ya upatikanaji umeme wa uhakika na wa nafuu??
Umesomeka bwana Mhando aka Muumini wa Milima ya Moto kwa Mh.Dr.Rev Get-Rude Lwakwatare.
 
Inakuwaje shule inayomilikiwa na Mchungaji wanaiba umeme..labda wafanyakazi wameiba umeme bila mmiliki kujua..Ngoja tumsubiri Rwakatare atuambie..maana kwenye mahubiri anakemea wizi sasa inakuwaje ofisi yake inaiba umeme..

Wizi ni wizi tu! Kwani yeye si ndio mkurugenzi? Kama anatumia mali ya wizi nayeye ni mwizi ndio maana hata aliacha kuwasilisha hati ya mali zake. Huyu mama ni fisadi. Na madudu mengi tutayajua kwa hawa watakatifu kumbe niwachafu na wananuka uvundo.
 
Huyu Waziri Muhongo anayo maono. Amedadavua kuwa Shirika hili lilianza miaka ya 1850 lakini hadi leo bado alijaweza kukidhi mahitaji ya umeme zaidi ya asilimia 15%. Ameahidi sasa ni wakati wa kuleta mabadiliko na hawawezi kukaa kimya TANESCO ikiborongo kwa kisingizio cha kuingiliwa na Wizara. Amesema shirika ni la umma na linawajibika kwa Watanzania wote.

Gold Reserve tuliyonayo kama nchi ni kituko kingine tukiwa tunashindwa hata na nchi ndogo kama Malawi.

Amesema pia Bodi itavunjwa kwani nayo imechafuka kama Mh. Mbatia alivyosema, Amesema Wajumbe wa bodi watapatikana based on thir competency baada ya kutangaza nafasi hizo magazetini.
 
UNA TATIZO GANI KUMTUMIKIA MUNGU NA KUWA MWANASIASA???


rwakatare.jpg
Mchungaji Dk. Getrude Lwakatare akiapa kuwatumikia wananchi Bungeni, Dodoma

Naamini kanisa linaamini kwamba viongozi wa nchi wamewekwa na Mungu, pia Mungu ndiye kiongozi Mkuu wa Nchi, na katika agano la kale manabii waliwasapoti wafalme wa Israel, Katika agano jipya kulikuwa na tatizo kwa warumi kwani walikuwa wanachanganya Neno la Mungu, siasa ya nchi na kufanya biashara hekaluni na Bwana Yesu aliona hiyo haikuwa sahihi ndio maana ilitokea wakamtupa nje ya hekalu.

Tukirudi katika mada hivi kuna tatizo gani kwa mtumishi wa Mungu kuwa Mwanasiasa?
 
mama mchungaji rwakatare kama hili ni kweli nakushauri ufanye sala ya wazi ya toba kwa watanzania ili japo urudishe imani kwa waumini wako.
 
Hajaficha uozo na hana cha kuficha mambo yameanikwa hadharani. Hii ndio tofauti na maviongozi mengine maongo na kujidai kuficha vitu ambavyo si confidential.

Prof. amejipambanua yeye ni Kiongozi wa namna gani. Niliwahi kuongea naye na alinipa sana faraja aliponiambia yeye ni Mwanataaluma na si mwanasiasa na atafanya kazi kwa Weledi. Na kama akiona mizengwe anabwaga manyanga na kuendelea na maisha yake.
 
Amesema kuwa St Mary Secondary Schools za Mheshimiwa Rev Rwakatare ni mojawapo wa wezi wa umeme wa Tanesco, wameiba jumla ya Tshs millioni 10 plus.

Shame on you Mheshimiwa Rev Rwakatare.

Agreed Mama mdogo, ndio maana ''Truth is what stands the test of experience''.
 
Huyu Prof. naona potential ndani yake kama hafanyi kazi kumfurahisha mtu. Uwazi na tabia ya kutotafuna maneno na kutokuwa na unafiki imenigusa ndani ya moyo. Nimeona ka mwanga kidogo kuhusu aina ya viongozi wanaotakiwa kuongoza TZ kwa sasa ndani ya Prof.

Hana ushabiki wa kisiasa na wala kashfa kwa vyama. Hebu tumwombee uzima na ulinzi wa Mungu kwani ni kiongozi tunayemhitaji na aliyofanya ndio tunaweza kuita MAAMUZI MAGUMU

ata mie nimemkubali.....sema watampoteza sasa ivi hawa mafisadi....maana nasikia anaingilia dili za watu wazito sana akiwemo General Mboma,na mtandao upo mpaka CONGO DRC.
 
Sasa ndiyo hayo matokeo yake. Mbunge anakuwa mfanyibiashara anaiuzia Tanesco nguzo kwa bei ya kuruka.
Mwalimu alituachia mfumo mzuri, mwanasiasa asijihusishe na biashara Mwinyi akaja na ujanja wake wa azimio la Zanzibar.
Sheria za kuhujumu uchumi zikafutwa kinyemela. Sasa Tanzania kila kona ni ufisadi tu. Anarchy reigns.
Hiki kibabu Mwinyi ndio kimetuletea haya matatizo yooote. Na ukiangalia hawa MAFISADI na UFISADI wote ni matunda ya uongozi wake. Mwinyi ndio mwanzilishi wa UFISADI na familia yake. Watanzania tulipumbazwa sana na enzi za "RUKSA", sasa tunaona joto ya jiwe. Haya ndio matokeo ya serikali lege lege na DHAIFU iliyoanzishwa na Utawala wa A.H Mwinyi.
 
Kaiba Rwakatare au St. Mary's? Au ndo mmiliki anajua!au menejimenti...lzm kama yupo smart ajibu mapema sana!
 
Nilishasema kuwa huko ndani kwene chungu cha CCM kuna chemka kweli kweli kwa kuni zao wenyewe huku zkikchagizwa na mkaaa wa CDM, japo hadi sasa kinachochemka hakijulikani, ni mawe au ni chakula bado ni kitendawili but at least tumefahamu kuwa kuna mchemsho
 
Acha kusifia ujinga, wizi wa umeme ni operational risk ambayo iko incorporated kwenye performance ya Tanesco, wizi wa umeme sio unaosababisha Tanesco kushindwa kusambaza umeme kwa wananchi wengi zaidi, hii mambo ya kutaja taja watu majina imeonekana kuwa ni Performance indicator kwa wanasiasa wetu siku za karibuni.

Anaweza kutueleza hao watu wameishachukuliwa hatua gani za kisheria mpaka sasa? kuna taarifa zozote zimetolewa polisi kuhusu wezi hawa? anaenda kuwataja majina bungeni ili iweje? Kwamba senti meris wanaiba umeme, well, umeme kiasi gani wanatumia senti meris zaidi ya kuwasha kwa ajili ya vijana wetu kusoma? au hajui kwamba hata Serikali kutokulipa bili za umeme na bado haichukuliwi hatua zozote zile inasababishwa na conflict of interest? au anadhani hatujui serikali ndio mdeni mkubwa wa tanesco.

waziri anaenda kutaja wezi majina badala ya kutupa realistic road map ya upatikanaji umeme wa uhakika na wa nafuu??

Sasa ulitaka asitaje ili iwe nini. Kama hukutaka ataje fumba masikio ili sisi tunaotaka tusikie na wewe usikie matamu toka kwa mkeo.

Unataka roadmap ipi ambayo hakuieleza kwenye budget na summations?
 
Heshima kwenu wanajamvi,

Mwanzoni nilikuwa najiuliza ni kwanini Rais J M Kikwete kaamua kumteua waziri wa Nishati na Madini nje ya wabunge wa CCM ?.Sasa nimeelewa sababu zake kwamba wabunge wangi wa CCM hawana uzalendo rushwa na tamaa ya madaraka ni sehemu ya utaratibu wao wa maisha ya kisiasa.Hakika zipo faida nyingi sana kama tukiweza kuwa na mawaziri ambao si wabunge.

Nyota ya Prof Muhongo ilianza kung'aa wakati wa uzinduzi wa bomba la gasi naomba kumnukuu "Tumepoteza sana kwenye migodi ya dhahabu nitahakikisha kwenye gesi watanzania tunafaidika" Hii statement si rahisi kuisikia ikitamkwa na kiongozi wa CCM. Tukipata mawaziri watatu kama Prof Muhongo hakika upo uwezekano taifa likaanza kusonga mbele.
 
....................................
Jamani huyu mama si ndo yule Mchungaji wa kanisa kubwa hapa Dar es Salaam..!!??
....................................

she was but !!!!kondoo wote wamefariki kwa ukame sasa atakichunga nini ?
 
Back
Top Bottom