Prof. Muhongo afanya Kikao na Viongozi jimboni kwake Musoma

Nyamemba

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
845
447
Jana Tarehe 23/12/2015 Prof. Muhongo amefanya Kikao na Madiwani, watendaji wa Halmashauri ya Musoma vijijini na wawakilishi wa wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi; wapo waliotoka Ujerumani; mabalozi na majaji wastaafu. Lengo la kikao hicho ni kujadili na kupanga mikakati ya maendeleo ya jimbo hilo.

Katika majadiliano hayo iliadhimiwa yafuatayo:-

1. Kuanzishwa kwa mfuko wa Elimu wa Jimbo ambapo Prof. Muhongo aliahidi kutoa shilingi milioni 100 ambazo atakopeshwa bungeni kwaajili ya kununua gari lakini yeye atazitumia kwenye mfuko huo badala ya kununua gari.

2. Kuanzishwa kwa ofisi tano za mbunge katika vijiji vya Busekela, Saragana, Murangi, Mugango na Nyegina. Ofisi hizo zitakuwa na mtumishi ambaye atakuwa mwakilishi wa mbunge na atafanya kazi kama Katibu wa mbunge kwaajili ya kusogeza huduma kwa wananchi.

Usaili wa kuwapata wawakilishi katika kila kijiji utaanza Tarehe 26-27/12/2015 na watakaofaulu wataanza kazi Tarehe 1/1/2016. Kila mwajiriwa atalipwa mshahara na pikipiki moja kwaajili ya kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo.

3. Katika kutekeleza Ilani ya ya CCM ya kujenga shule moja katika kila kata, kikao kimeadhimia kuchagua shule nne ambazo zitapewa kipaumbele cha kwanza ambapo zitaboreshwa vyumba vyake vya madarasa, maabara, kuongeza idadi ya walimu kutoka ndani na nje ya nchi na kujenga maktaba kwaajili ya kutunza vitabu.

Utaratibu huo utaanza katika kata tano za Majita shule mbili, Mugango shule moja na Bukwaya ambapo ilikubaliwa madiwani watakaa kuchagua shule watakayoona inafaa.

4. Katika kuimarisha Elimu, Mbunge (Prof. Muhongo) ametoa vitabu 20,000 katika shule mbalimbali ambapo kipaumbele kimetolewa katika shule zilizofanya vibaya. Aidha, vitabu vingine 22,000 vimeagizwa kutoka Marekani na vitakapofika vitasambazwa kwenye shule zote za kata za jimbo la Musoma Vijijini.

5. Kila shule zitawekewa umeme, maji, na nyumba za walimu ambapo ilikubaliwa mfuko wa Jimbo na Fedha kutoka Halmashauri zitatumika kuuendeleza mpango huo.

6. Prof. Muhongo aliahidi kusimamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Musoma hadi Makao Makuu ya Jimbo ambapo tathmini tayari imeshaanza na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba 2015.

Aidha, ilikubaliwa madiwani wakae kikao na kupitisha bajeti ya kukarabati barabara zote zilizo chini ya Halmashauri, kikao hicho kimetakiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwezi huu.

7. Ujenzi wa Kituo cha Afya uliosimama kwa muda mrefu sasa utaendelea ambapo Iliahidiwa kutolewa bati kwaajili ya kupauwa mapema iwezekanavyo ambapo Prof. Muhongo aliahidi kutoa gari la wagonjwa linalotarajiwa kuingia nchini baada ya wiki mbili.

#Hapa kazi tu#
 
Kama kila Mbunge angefanya hivi, nchi hii ingeandika historia ya pekee,

Nimependa hapo kwenye kipaumbele cha vitabu kwenda kwenye shule zilizofanya vibaya, maeneo mengine vitabu na vifaa hupelekwa kwenye shule zilizofanya vizuri kama zawadi ama kuuonesha umma kuwa kufanya vizuri huko kumetokana na vitabu hivyo

Hongera Muhongo, you are a man of actions that other MPs have to learn from
 
WELEDI WA HALI YA JUU WA PROF MUHONGO WAWATISHA MAFISADI.Ni ukweli usiofichika kuwa wazir wa nishati na madini Prof Muhongo anafanya kazi zake kwa kutumia weledi wa hali ya juu sn.Prof muhongo mara baada ya Rais Dr magufur kumteua kuwa wazir wa nishat na madin,Prof muhongo alianza kuonyesha weled wake wa hali ya juu sana kwa kutembelea mabwawa yote ya maji na vyanzo vyote vya umeme ili kujilizisha na uwezo wa mabawa hayo katika kutoa nguvu za kutosha za umeme.Baada ya ziara hiyo ya Prof Muhongo ,alikuanza kutoa report mbali mbali za kiasi cha umeme kwa siku .Prof alienda mbali kwa kusema kuwa kwa sasa ataomba watu binafs waingie pia kusaidia kutoa umeme.Weled huu wa hali ya juu wa Prof muhongo,umewatisha sana mafisadi wengi ambao hawapendi maendeleo ya nchi yetu .Na sasa wameanza kutumia mitandao ya jamii kutengeneza majungu kwa Prof muhongo.Mafisadi hawa ,wamekuwa wanamwogopa sana Prof muhongo.Jaman vijana munaopewa pesa na mafisad ili mumchafue Prof achen hizo kwan ,hamtamweza huyu Prof wa duniaW
 
Mbona hayo ni majukumu ya serikali, ...kuna ma VEO, WEO nk.

Pia kuna wizara inayoshughulikia elimu nk.

Haya yatakuwa ni mazingira ya kuruhusu rushwa miongoni mwa wabunge.

Wabunge kazi yao ibaki kuisimamia serikali ktk kuwaletea maendeleo wananchi wao.
 
Tanzania nchi ya ajabu sana, Prof. msomi alobobea anakaa kujadiliwa na kuchambuliwa na darasa la saba bungeni, wakati mwingine na kutukanwa ndani ya bunge. Hili ni tatizo kubwa sana kwa maprf. wetu, watafakari upya
 
Jana Tarehe 23/12/2015 Prof. Muhongo amefanya Kikao na Madiwani, watendaji wa Halmashauri ya Musoma vijijini na wawakilishi wa wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na wageni mbalimbali wa ndani na nje ya nchi; wapo waliotoka Ujerumani; mabalozi na majaji wastaafu. Lengo la kikao hicho ni kujadili na kupanga mikakati ya maendeleo ya jimbo hilo.

Katika majadiliano hayo iliadhimiwa yafuatayo:-

1. Kuanzishwa kwa mfuko wa Elimu wa Jimbo ambapo Prof. Muhongo aliahidi kutoa shilingi milioni 100 ambazo atakopeshwa bungeni kwaajili ya kununua gari lakini yeye atazitumia kwenye mfuko huo badala ya kununua gari.

2. Kuanzishwa kwa ofisi tano za mbunge katika vijiji vya Busekela, Saragana, Murangi, Mugango na Nyegina. Ofisi hizo zitakuwa na mtumishi ambaye atakuwa mwakilishi wa mbunge na atafanya kazi kama Katibu wa mbunge kwaajili ya kusogeza huduma kwa wananchi.

Usaili wa kuwapata wawakilishi katika kila kijiji utaanza Tarehe 26-27/12/2015 na watakaofaulu wataanza kazi Tarehe 1/1/2016. Kila mwajiriwa atalipwa mshahara na pikipiki moja kwaajili ya kuwahudumia wananchi wa jimbo hilo.

3. Katika kutekeleza Ilani ya ya CCM ya kujenga shule moja katika kila kata, kikao kimeadhimia kuchagua shule nne ambazo zitapewa kipaumbele cha kwanza ambapo zitaboreshwa vyumba vyake vya madarasa, maabara, kuongeza idadi ya walimu kutoka ndani na nje ya nchi na kujenga maktaba kwaajili ya kutunza vitabu.

Utaratibu huo utaanza katika kata tano za Majita shule mbili, Mugango shule moja na Bukwaya ambapo ilikubaliwa madiwani watakaa kuchagua shule watakayoona inafaa.

4. Katika kuimarisha Elimu, Mbunge (Prof. Muhongo) ametoa vitabu 20,000 katika shule mbalimbali ambapo kipaumbele kimetolewa katika shule zilizofanya vibaya. Aidha, vitabu vingine 22,000 vimeagizwa kutoka Marekani na vitakapofika vitasambazwa kwenye shule zote za kata za jimbo la Musoma Vijijini.

5. Kila shule zitawekewa umeme, maji, na nyumba za walimu ambapo ilikubaliwa mfuko wa Jimbo na Fedha kutoka Halmashauri zitatumika kuuendeleza mpango huo.

6. Prof. Muhongo aliahidi kusimamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Musoma hadi Makao Makuu ya Jimbo ambapo tathmini tayari imeshaanza na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba 2015.

Aidha, ilikubaliwa madiwani wakae kikao na kupitisha bajeti ya kukarabati barabara zote zilizo chini ya Halmashauri, kikao hicho kimetakiwa kufanyika kabla ya mwisho wa mwezi huu.

7. Ujenzi wa Kituo cha Afya uliosimama kwa muda mrefu sasa utaendelea ambapo Iliahidiwa kutolewa bati kwaajili ya kupauwa mapema iwezekanavyo ambapo Prof. Muhongo aliahidi kutoa gari la wagonjwa linalotarajiwa kuingia nchini baada ya wiki mbili.

#Hapa kazi tu#
Binafsi nimpongeze sana Prof, Muhongo kwa kupewa dhamana ya kuwaongoza wananchi wa Jimbo la musoma vijijijni kupitia Ubunge,Na pia kwa nafasi ya Waziri wa Nishati na madini, Ushindi wake alioupata Jimboni ni ushindi wenu, Msimwangushe, mmepata Kiongozi alie na nia ya dhati ya kutatua matatizo yenu, Ninaamini hata madiwani wenu pia wanatosha katika kuwatumikia wananchi ili kuleta maendeleo. Kumbukeni Musoma vijijini ni kati ya majimbo yaliyochangia Pato la Taifa na uchumi wa Nchi yetu kupitia Kilimo cha Pamba,uvuvi na mifugo lakini ikasahulika kwenye miundo mbinu ya barabara hali tuliyoishuhudia hata majuzi pale chumwi katika kipindi hiki cha Mvua, si nia yangu kujadili hayo kwa sasa isipokuwa Niongelee jambo moja;
Nina bahati ya kumfahamu Prof Muhongo kidogo Hapendi ubabaishaji katika kazi, Ni mtu anaeita kitu kwa jina kama kilivyo ni mtu wa hoja sasa Waheshimiwa madiwani, Mzee huyu Prof.mkimtumia vizuri jimboni Musoma vijijini haitakuwa hivyo miaka mitano ijayo na kuendelea , nasema hivyo kwa sababu MKIENDEKEZA SIASA BADALA YA KUFANYA KAZI maendeleo hayatakuwapo mipango yenu itabaki ndoto. Fanyeni kazi pamoja, mwenye jambo lolote zuri la kimaendeleo tumieni vikao vyenu kuwasilisha siasa za kuzungukana zisiwepo kati yenu,na MKIMTANGULIZA MUNGU KATIKA KAZI ZENU Historia itaandikwa kwa kuwepo kwenu maana kila zama ina kitabu chake.
Ombi kwa Prof, Muhongo Natambua upeo mkubwa ulio nao Mzee, Fufua kilimo cha umwagiliaji katika mabonde ya Bugwema ile miundo mbinu ikarabatiwe ajira zipatikane na zaidi chakula cha uhakika kipatikane pale, Saidia vijana kujiajiri, kupitia viongozi wao wachaguliwe vijana wenye nia ya kufanya kazi wawe katika vikundi wafanye ziara katika mikoa mingine nchini kujifunza vijana wengine wanafanyaje na kupata mafanikio ya halali mfano; Pale Arusha kuna vijana,vikundi vya wakulima wa mbogamboga kama Nyanya, Vitunguu, Kabeji n.k hawa vijana hutengeneza Kati ya Tsh 12,000,000/= hadi 15,000,000/= Hii ni ndani ya miezi 3 tu na maji ni ya mifereji kutoka milimani wana maisha tofauti kabisa kiuchumi kutokana na kujiajiri, Anza na wachache tu itakuwa chachu kwa wengine.
UFUGAJI, Kwa kuwa Nishatiya umeme inaendelea kusambazwa na sehemu nyingine Nishati hiyo tayari ipo Ni wakati pia Vijana wafundishwe kufuga Kuku kitaalamu ikiwamo uzalishaji Vifaranga kwa kutumia mashine (INCUBATOR) Hii ni ajira nzuri sana kwa kujitafutia kipato kwa wenye nia,Halmashauri zina wataalamu wa Kilimo na mifugo ni wakati sasa wa wao Kufanyakazi wakitumika vyema. vifaranga Huuzwa kati ya Tsh 2000/= hadi 5000/= kutegemea umri wa kifaranga.
UVUVI, vijana wapate elimu ya ufugaji bora wa samaki wajijengee mabwawa ufugaji huu una faida nyingi ikiwamo kuokoa muda na umbali mrefu wa kutafuta samaki ziwani kulingana hali halisi wavuvi hutumia zaidi ya saa 3-6 kusafiri tu tena kwa Boti kwenda katika eneo la uvuvi.
Mkienda pamoja katika utumishi Ninaamini Majimbo mengine Mkoani Mara wenye nia watakuja kujifunza kwenu na Mkoa wote utabadilika katika nyanja zote. NA HAYO NDIO MABADILIKO YA KWELI, MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mbona hayo ni majukumu ya serikali, ...kuna ma VEO, WEO nk.

Pia kuna wizara inayoshughulikia elimu nk.

Haya yatakuwa ni mazingira ya kuruhusu rushwa miongoni mwa wabunge.

Wabunge kazi yao ibaki kuisimamia serikali ktk kuwaletea maendeleo wananchi wao.

"My fellow Americans, ask not what your country can do for you, ask what you can do for your country." - John F. Kennedy
 
Back
Top Bottom