OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 669
Muhamad Yunus Muasisi wa mfumo wa kisasa wa mikopo midogo midogo, Micro-finance na Micro-Credit, alizaliwa Juni 28, 1940
Profesa huyu alitamani kuupeleka umasikini wa India kwenye makumbusho, yani kumfanya kila mtu kuwa tajiri na umasikini ukabaki kwenye makumbusho na akaamini vizazi vijavyo vitasimuliana kuhusu umasikini bila kuujua umasikini wenyewe.
Kwa kipindi chake aliangalia namna ya kuwasaidia masikini kwa mikopo, kwa kuwa mikopo ya awali ilikuwa inataka dhamana kubwa kama nyumba, shamba kiwanja au mali yoyote.
Muhamad aliona kwa watu masikini ambao wanauhitaji mkubwa wa mikopo hawana mali ila IMANI, ‘trust’ kati yao, na akatumia Imani hiyo kama kigezo cha kutoa mikopo kwa masikini.
Ndipo kukaja mfumo wa kuwakopesha watu wakiwa katika vikundi, ili kila mtu awe mlinzi wa mwenzie kwa Imani ya kwamba wote hawawezi kukimbia na pia wenyewe wanajuana kwamba nani anafaa kuaminiwa na asiyefaa kuaminiwa.
Mwaka 1983 ndipo muhamad yunus alianzisha Gramen Bank ili kuwakomboa wahindi kutoka kwenye umasikini.
Miaka ya mwanzo mfumo huo ulionyesha kufanikiwa kwa azma ya yunus ya kuuona umasikini ukielekea makumbusho, lakini ghafla hali ikabadilika baada ya Micro Finances kuvamiwa na mafisi wabinafsi walitaka faida Zaidi na sio kuwaondolea umasikini watu walio wengi.
Tafiti zimeonyesha umasikini ulipungua kwa kasi tangu kuanzishwa kwa Gramen bank, pia maeneo mbalimbali ambayo yali-adapt mfumo huo wa ukopeshaji na umasikini ukapungua.
Lakini ghafla kuanzia mwaka 2000 kuja juu, mafisi hao wakafanya umasikini wa masikini kuongezeka badala ya kupungua kama ambavyo Muhamad Yunus alivyowaza awali.
NB: Dhumuni la Makala haya sio kujadili kufeli au kufaulu kwa MicroFinance bank, lakini ni kuiangazia ndoto kubwa ya Muhamad Yunus ya kuupeleka umasikini kwenye makumbusho.
Je na sisi tuna wachumi/bankers wenye mawazo ya kuupeleka umasikini kwenye makumbusho?
Signed
Oedipus