Prof. Mugaya Achanganya Lugha Kuhadaa Wazazi

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Namnukulu:

"mwanafunzi mmoja, wakati wa kukimbia mabomu ya FFU aliangukia front face, akapata deep cut amefanyiwa stitches"

tuchukulie kuwa huyo aliyeumia ni mtoto wa mzee Ng'wanambogolo kule kijijini Nyanguge. Akisikia hayo maneno si anaweza kudhani mtoto wake amefaulu mtihani?

hahahaha!!

source: BBC-Swahili
 
Wasomi wa kibongo hata hawaangalii wako mazingira gani... Wao wanadhani ukichanganya lugha ndio utaonekana umekula nondo kwelikweli.. ha ha ha ha ... Bado safari ni ndefu
 
Nje ya mada:
Wanaojua lugha vizuri wengi huwa hawachanganyi.Kama Mkapa,akiamua kuongea kiswahili basi ataongea kiswahili mpaka mwisho.Akianza kutema ngeli ni ngeli tu kwa kwenda mbele.Ukikutana na mtu anayejishebedua na kiswanglish,we mpe cha ukweli bila kuchanganya na kiswahili.Utaona anavyoanza kujiumauma!
 
Back
Top Bottom