Prof. Mkumbo: Katiba iliyopo sasa sio ya Demokrasia ya Vyama Vingi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,097
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotumika kwa sasa ni ya demokrasia ya Chama kimoja.

Amesema hali hiyo imechangia kuwa na demokrasia dumavu ambayo inapelekea kuchelewa kwa maendeleo, ambapo amedai kuwa kuna uhusiano wa demokrasia bora na maendeleo

Pia ameshauri kuwa Katiba mpya ni muhimu ili kuwezesha demokrasia ya vingi kustawi ambayo itawezesha wananchi kushiriki ipasavyo.

Amesema kuwa kwa mazingira ya demokrasia ya sasa ni rahisi kutabilika tofauti na ilivyo kwa Kenya, ametoa mfano kuwa ni rahisi kutabili kuwa CCM itashinda uchaguzi 2025 kwenye nafasi ya Urais, amedai kuwa hiyo inachangiwa na takwimu za matokeo ya Urais kwenye chaguzi zilizopita.

Prof. Kitila Mkumbo ameyasema hayo leo Septemba 15, 2022 katika mdahalo ambao umeandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Nchini (LHRC) kwa kushirikiana na wadau wengine, katika siku ya demokrasia duniani ambayo imekuwa ikiadhimishwa kila mwaka.
 
Kutakuja kutokee changamoto ya maelewano miongoni mwa watu wa tume ya uchaguzi, siku zijazo. Hii itatokana na utaratibu mbaya wa the so called, Demokrasia.
 
Maneno yake nayaunga mkono.
Niabu kubwa sana kwa mtu kama Prof kuwa na maneno ya kutapatapa yaani yasiyoaminika mbele ya jamii yetu.
Kama kaona ni kipindi cha kuirudisha heshima yake ni vizuri sana tukumbuke prof ni elimu kubwa ni mbaya kwa prof kudhiakiwa kwa ajili ya Cheo cha kuteuliwa ambayo siyo ya kudumu
 
Back
Top Bottom