Prof. Mkenda, waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2023 kutoka shule ya msingi moja wote wamehamishiwa sekondari moja

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,807
21,409
Mimi labda sijaelewa.

Unakuta shule ya msingi A, ina wanafunzi 123 waliomaliza darasa la saba na wamafaulu wote kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023.

Cha kushangaza wanafunzi wote wa hiyo shule ya msingi A wamepangiwa shule moja tu ya sekondari iliyopo kwenye hiyo kata kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.

Sasa kwanini wamehamishwa wote kutoka msingi moja kwenda sekondari moja iliyopo kiji hicho hicho na kata hiyo hiyo?

Kwanini wasingebakia hapo hapo msingi waendelee na kidato cha kwanza kwa shule ya msingi kuongezewa madarasa, walimu na vitendea kazi? Kulikuwa na haja gani kujenga shule jirani ya kuhamishia watoto wale wale , wa kijiji kile kile, kata ile ile?

Kulikua na haja gani kukopa mikopo ya Bank ya Dunia kujenga madarasa mapya kibao shule ya jirani na ilipo shule ya msingi kwa ajili ya kuhamishia hapo watoto?

Je Prof, huoni kuwa mitihani ya darasa la saba unaofanyika kwenda kidato cha kwanza sasa ni ya kufutwa na kuboresha shule za msingi ziwe hadi kidato cha nne?

Huoni sasa ni wakati wa shule za sekondari za kata kugeuzwa kuwa vocational training kwa ajili ya wanaomaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano?
 
Huu Mfumo ni wa kipuuzi kabisa.

1. Watoto wenye ufauli mdogo kwenye Shule ya Msingi A wanapelekwa wote Shule ya Sekondari A. Hivyo hivyo kwa wale waliofaulu vizuri. Hivyo hivyo kwa waliofaulu. Hapa Sasa tunafanya baadhi ya Shule ziwe Chini na zingine Juu kiufaulu.

2. Wanafunzi pia hatuwasaidii, kwa sababu tunahamisha tabia za Wanafunzi kutoka Shule Moja ya Msingi kwenda Shule Moja Sekondari.

3. Ufundishaji kwenye Shule za Sekondari unakuwa ni mgumu.

Mifumo hii ya kupanga Wanafunzi Shule kutoka Primary kwenda Sekondari ibadilishwe na Wanafunzi wawe wanachanganywa changanywa.
 
Mimi labda sijaelewa.
Unakuta shule ya msingi A, ina wanafunzi 123 waliomaliza darasa la saba na wamafaulu wote kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023.

Cha kushangaza wanafunzi wote wa hiyo shule ya msingi A wamepangiwa shule moja tu ya sekondari iliyopo kwenye hiyo kata kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2023.

Sasa kwanini wamehamishwa wote kutoka msingi moja kwenda sekondari moja iliyopo kiji hicho hicho na kata hiyo hiyo?

Kwanini wasingebakia hapo hapo msingi waendelee na kidato cha kwanza kwa shule ya msingi kuongezewa madarasa, walimu na vitendea kazi? Kulikuwa na haja gani kujenga shule jirani ya kuhamishia watoto wale wale , wa kijiji kile kile, kata ile ile?

Kulikua na haja gani kukopa mikopo ya Bank ya Dunia kujenga madarasa mapya kibao shule ya jirani na ilipo shule ya msingi kwa ajili ya kuhamishia hapo watoto?

Je Prof, huoni kuwa mitihani ya darasa la saba unaofanyika kwenda kidato cha kwanza sasa ni ya kufutwa na kuboresha shule za msingi ziwe hadi kidato cha nne?

Huoni sasa ni wakati wa shule za sekondari za kata kugeuzwa kuwa vocational training kwa ajili ya wanaomaliza kidato cha nne na kushindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano?
Msingi wana muundo tofauti na secondary.
Tukianzia Lugha, nidhamu, namna ya kufundisha, umri, peer group, nk.
Hatahivyo, kuwekwa pamoja hakuna ubaya ila si vizuri kuchanganya watu wenye makundi rika tofauti katika hatua za awali.
 
Una hoja nzuri bwashee.
NYONGEZA TU: Hizi shule zetu za kata zingeboreshwa kwa kujengewa mabweni ili linapokuja suala la wanafunzi kwenda sekondari kuwe na mtawanyo wa wanafunzi kwa kupelekwa wilaya, mikoa na hata kanda zingine tofauti na wilaya walizopatia elimu yao ya msingi. Hiki kitasaidia sana katika kujifunza na kuwa serious na masomo. Pia kutaongeza mshikamano miongoni mwetu watanzania.
 
Aliweza Nyerere tu miaka hiyo. Hawa mmmmhhhh.
 
Una hoja nzuri bwashee.
NYONGEZA TU: Hizi shule zetu za kata zingeboreshwa kwa kujengewa mabweni ili linapokuja suala la wanafunzi kwenda sekondari kuwe na mtawanyo wa wanafunzi kwa kupelekwa wilaya, mikoa na hata kanda zingine tofauti na wilaya walizopatia elimu yao ya msingi. Hiki kitasaidia sana katika kujifunza na kuwa serious na masomo. Pia kutaongeza mshikamano miongoni mwetu watanzania.
Kwanini mabweni wakati wanafunzi wanatokea kata husika?
 
Nimeshauri au ongezea kuwa badala ya wanafunzi kubaki katika kata waliyosoma shule ya msingi, wapelekwe wilaya na mikoa mingine tofauti na hapa ndipo umuhimu wa mabweni katika shule zetu hizi unapoonekana.
 
Nimeshangaa kwakweli kwa hii style waliyokuja nayo, ingawa kama nadhani na upendeleo bado uko ndani yake. Mfano shule ya Mwanza Sec ambayo ni kongwe ina walimu wa kutosha tena iko katika ya mji tulitegemea wapangwe wanafunzi wa shule za karibu yake kama Bugando Primary n.k , lakn wamepangwa wanafunzi wa kutoka shule za alliance na new alliance na nyinginezo.. ambazo ziko kata ya mbali. Natamani hizi shule kongwe za katika ya mji kama Pamba na Mwanza wangekuwa wanachanganya wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali kuliko kuchukua watoto wote wa shule moja kuwahamishia shule nyingine ya sekondari.
 
Back
Top Bottom