Prof. Mkandara yuko SUA -Ushirikiano wa kusaidia wizi pesa za serikali

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,700
4,693
Hii ni taarifa niliyoipokea hivi sasa toka ndani ya kikao chuo kikuu cha SUA. Bado natafuta kapicha toka kikaoni. Kuna kikao maalumu cha baraza la chuo ili kupitisha taarifa ya upotevu wa milioni zaidi ya 500 za mradi wa ujenzi, uliotokea SUA na kutangazwa hapa na zygot. Hiyo imeniunganisha na mtandao wa wana SUA, na wananipa ushirikiano.

Kilichotokea nyuma ni wizi wa pesa na kusababisha jengo jipya lishindwe kumalizika wakati lilikuwa na pesa ya kutosha toka kwa wafadhiri wa NORAD. Kwa wizi huo, jengo linatafutiwa pesa za ziada toka serikalini ili limaliziwe. Baada ya chuo kushindwa kujieleza ni wapi pesa hizo zimepelekwa kwa zaidi ya miezi miwili. Sasa Prof. Mkandara wa UD ameitwa SUA, yeye kama mjumbe wao wa kamati ya fedha ili atoe msaada. Taarifa za siku mbili zinaonyesha Profesa huyu amekuwa akiwasihi wajumbe wenzake wasiyatoe nje mambo hayo ili kumsaidia VC mwenzake. Leo ripoti yake iko mezani kama mwenyekiti wa kamati kutoa maelezo na ruhusa ili chuo kitumie pesa zingine za serikali kumalizia ujenzi huo. Kisingizio cha leo kinachoelezwa toka kiakaoni, eti gharama iliongezeka kwa sababu ya mtumiaji kufanya mabadiliko ktk ujenzi. Uhalisia ni kwamba pesa iliibiwa na watu binafsi kabla jengo halijaisha.

Huu ndiyo nauita ushirikiano wa kufanya mambo ya wizi kwa viongozi wasomi wa nchi hii.
 
Kwa kuwa magu anapenda maneno ya kuambiwa anaweza kukuelewa
But sijaona uhusiano wowote ulichokileta na mkandara.
Watanzania tuache unafiki na husda
 
Shilingi dhidi ya dolari inaweza kuwa jibu zuri tu

Mkandarasi anaweza kusaidia baadhi ya majawabu.
 
Inawezekana una hoja nzuri, lakini umeandika kwa haraka (au woga??) kiasi kwamba umeshindwa kueleweka vema na hata baadhi ya vitu kama majina na takwimu umekosea. Hebu tulia, soma upya ulichoandika urekenishe vizuri ili tuweze kutoa michango mizuri
 
Nahisi kuna tabia imejengeka mkishindwa kuendana sawa kwenye mgao wa pesa za kifisadi mnakuja kuchomeana kwenye mitandao ya kijamii
 
Nahisi kuna tabia imejengeka mkishindwa kuendana sawa kwenye mgao wa pesa za kifisadi mnakuja kuchomeana kwenye mitandao ya kijamii
Ni vizuri tu! Yaani unaomba tuelewane ili siri isifichuke?
Ukitaka kujua waharifu wa nchi hii ambao hawajakamatwa, waulize mahabusu wa Keko. Utakataa kwa kuwa umeambiwa na mahabusu, mwizi?
 
Hii ni taarifa niliyoipokea hivi sasa toka ndani ya kikao chuo kikuu cha SUA. Bado natafuta kapicha toka kikaoni. Kuna kikao maalumu cha baraza la chuo ili kupitisha taarifa ya upotevu wa milioni zaidi ya 500 za mradi wa ujenzi, uliotokea SUA na kutangazwa hapa na zygot. Hiyo imeniunganisha na mtandao wa wana SUA, na wananipa ushirikiano.

Kilichotokea nyuma ni wizi wa pesa na kusababisha jengo jipya lishindwe kumalizika wakati lilikuwa na pesa ya kutosha toka kwa wafadhiri wa NORAD. Kwa wizi huo, jengo linatafutiwa pesa za ziada toka serikalini ili limaliziwe. Baada ya chuo kushindwa kujieleza ni wapi pesa hizo zimepelekwa kwa zaidi ya miezi miwili. Sasa Prof. Mtukuka VC wa UD ameitwa SUA, yeye kama mjumbe wao wa kamati ya fedha ili atoe msaada. Taarifa za siku mbili zinaonyesha Profesa huyu amekuwa akiwasihi wajumbe wenzake wasiyatoe nje mambo hayo ili kumsaidia VC mwenzake. Leo ripoti yake iko mezani kama mwenyekiti wa kamati kutoa maelezo na ruhusa ili chuo kitumie pesa zingine za serikali kumalizia ujenzi huo. Kisingizio cha leo kinachoelezwa toka kiakaoni, eti gharama iliongezeka kwa sababu ya mtumiaji kufanya mabadiliko ktk ujenzi. Uhalisia ni kwamba pesa iliibiwa na watu binafsi kabla jengo halijaisha.

Huu ndiyo nauita ushirikiano wa kufanya mambo ya wizi kwa viongozi wasomi wa nchi hii.
Nchi za Kiarabu hazina viongozi wengi wenye PhD lakini nchi zao zinameremeta kwa utajiri na mambo kwenda sawa. Sisi hapa kwetu wasomi ni wengi lakini hovyohovyo kila kona.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom