Prof. Mkandala na jopo lake watuliza hatihati za mgomo mkubwa udsm. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Mkandala na jopo lake watuliza hatihati za mgomo mkubwa udsm.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by bampami, Dec 11, 2011.

 1. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,851
  Likes Received: 1,288
  Trophy Points: 280
  -Ni baada ya kuwarudisha wanachuo 43 ambao walikuwa suspended kwa kosa la kufanya maandamano ambayo hayakuwa na ruhusa.
  -Wengine 8 bado mazungumzo yanaendelea ili waweze kurudishwa.
  -Tangazo la kutoka kwa BOOM kesho lanyamazisha Mgomo mkubwa.

  Ni jana tu niliripoti kuhusu hatihati kubwa za kuwepo mgomo kesho J3 hapa Udsm hii ni kutokana na kufukuzwa kwa wenzetu 43 na pia kuhusu kutoingizwa kwa boom mpaka sasa.
  Leo jioni mida ya sa kumi hii yamebandikwa matangazo ambayo yanaelezea kurudishwa kwa wenzetu 43 na wengine 8 kujadiliana namna ambavyo watarudishwa. HII IMEKUWA FARAJA KUBWA SANA KWA WANAUDSM PAMOJA NA WAZAZI WA WENZETU UKIZINGATIA KWAMBA WALIKUWA WAKITETEA WADOGO ZETU.

  BOOM BOOM BOOM
  Hatimaye waziri wa mikopo Udsm mh naftari athibitisha kuingizwa kwa bum kufikia kesho mchana baada ya wiki mbili za tabu na shida kwa wanaudsm japo si wote kama ujuavyo kila mahali hapakosi kuwa na matabaka.
  -HABARI HII IMEKUWA FARAJA PIA KWETU NA IMEPUNGUZA HASIRA ZA KESHO.

  SWALI: JE ENDAPO HIYO KESHO HAKUAINGIZWA BUM NINI KITATOKEA HILI NDO JAMBO AMBALO WENGI WANACHUO WANAJIULIZA.

  Hii ndo khalì ya udsm kwa sasa.

  Mimi napenda kuwashukuru uongozi wa chuo, wakishirikiana na Daruso kwa busara walizozitumia k uweza kuwasudisha hao wenzetu manakeee sijui nini kingètokea kama si kufungwa chuo.

  Nikiripoti toka hapa hall 5 floor ya kwanza rum no mimi ni bampami wa Jffff!!
   
 2. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,368
  Trophy Points: 280
  Heheee, kumbe upo main campus!

  Asante kwa maelezo yako. Duh! Nawapongeza viongozi wa chuo. Wanajitahidi. Leo ngoja tukacheki a/c zetu tuone kama wametuwekea BOOM.
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kumbe uko hall 5 mkuu,mböna hatupeanag hata ishara?
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Mukandala muda wao si ulikwisha june.Wameongezewa muda?
   
 5. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwa hili nimpongeze Mukandala kwa kufanya kazi ya mzazi zaidi kuliko mlezi maana hapo ni kwenda kinyume na maamuzi ya baraza la chuo. Pili niwapongeze Raisi na Waziri mkuu wa daruso kwa kuwa makini wavumilivu na wasikivu heko kwa kuwa wakomavu wa siasa.

  Kuna kundi moja jana liliibuka baada ya kupata habari za uongo za kichochezi toka kwa chama fulani cha siasa bila kujua wanafaidika na nini na chuo kufungwa nasi kufukuzwa chuo wote, kilitudanganya kuwa boom lapili litatoka tarehe 24/12 kwasababu serikali imefulia na hela za bodi zimetumiwa na wajanja kufanyia biashara zao jambo ambalo kiufundi haliwezi kufanyika. Tuache porojo.

  Kwa taarifa nilizozipata asubuhi hii kuna kundi la vijana linalosumbua wenzao wakisoma usiku kwa kupuliza vuvuzela bila mpangilio ambapo ni kinyume na ustaarabu wa wasomi pia wameenda yombo kuleta vuguvugu la kuungwa mkono ili chuo kifungwe. Nasema mimi na kundi langu nitawataja wale wote watakao endeleza hizo njama za chuo kufungwa na kwa mujibu wa BARAZA la chuo ni kwamba kila atakayeleta kimbelmbele cha kuvunja amani jina lake likiletwa na wanafunzi wenyewe lifanyiwe uhcunguzi wa haraka na bila kupoteza muda apewe suspension ya miezi minne.

  Kila la kheri wana UDSM kwa kupambana kuleta elimu bora, matumizi sahihi ya boom na kukomaa kisiasa. Heko KILAWA na wenzako katika kufuatilia wenzetu waliosimamishwa masomo ili wote warudi na wenye kesi wafuwe kezi hizo. Heko MUKANDALA na timu yako kuhakikisha chuo kinakua salama na amani hasa kwa kutupatia taarifa iliyosahihisha uongo ambao tulishalishwa kuhusu kutoka kwa boom maana njaa ni njaa tu na kila mmoja ameishiwa kwa sasa hasa wale tunaotumia oom kulipa ada na kusaidia ndugu zetu. Pamoja na kuwa ni jumapili taarifa iliyosainiwa na DVC Administration ilisambazwa kila kona. Tunaomba utekelezaji wake uwe makini na timely kama taarifa inavyoahidi.
   
 6. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Napenda kukutaarifu kuwa search committee iliyoundwa na UDASA na wadau wengine ilishawachagua na kutangaza manaibu makamu wakuu wa chuo na Mukandala amepitishwa hivi punde subiri utasikia tangazo. Mimi kama mdau wa habari nimefuatilia sana hilo baada ya kusikia kuwa UVC unapewa tu na raisi hata kama unaowaongoza hawakutaki mradi tu awe rafiki. Tuache porojo tufanye utafiti
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,183
  Trophy Points: 280
  Makamu nao,I mean Maboko na DVC utawala wanaendelea?
   
 8. M

  Mabulangati JF-Expert Member

  #8
  Dec 12, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 779
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kama sijakosea niliona tangazo la Public Relations Officer likizungumzia swala hilo tangu mwezi June mwaka huu kuwa Chancellor amewateua kuendelea na nyadhifa zao kwa kipindi cha miaka mitano.
   
Loading...