Tozo

Member
Aug 23, 2021
11
45
Kama kuna mstaafu wa kisiasa utavutiwa kusoma maoni yake pindi afanyapo mahojiano na waandishi wa habari ni Prof. Joseph Mbwiliza.

Huyu ni mbunge wa zamani wa Kasulu kabla ya kugawanyika na kuwa majimbo 3, Mjumbe wa NEC akiwakilisha mkoa wa Kigoma enzi hizo, RC wa Kilimanjaro na Naibu waziri kama kumbukumbu zangu sijakosea.

Na aliwahi pia kuwa mhadhiri wa zamani UDSM kabla ya kuingia kwenye siasa. Hutoa ushauri makini tena pasipo woga wowote kwa manufaa ya taifa letu. Moja ya mahojiano aliyowahi kufanya ni kukosoa utawala wa awamu ya tano kuiga utawala wa viinchi kama Rwanda na Burundi.

Alizua mjadala mkubwa pale alipouliza " Tanzania tumefikia hatua viongozi wetu kujifunza kutawala kwa kuiga Rwanda na Burundi " Alisema maneno hayo akimkosoa Rais wa awamu ya 5 Hayati Mzee Magufuli. Natamani ahojiwe juu ya uaonavyo utawala wa awamu ya 6. wa Mhe. Raisi Mama Samia.

Nilitamani nionane naye Chato kwenye kumbukizi ya Nyerere na kilele cha Mwenge ili nipate kujadiliana naye mambo kadhaa juu ya mstakabali wa Taifa letu na auonavyo utawala wa awamu ya 6.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom