Prof. Mbele: Tundu Lissu haichafui nchi, kumsema Spika wa Bunge na Serikali sio kuichafua nchi. Hata Nyerere alisema CCM ni kansa

Huu ni ukweli usiopingika kwamba serikali ya magufuli badala ya kuonesha utendaji wake sasa ni kujibu hoja za tundu lissu.
Kila kiongozzi wa ccm anapofanya press conference lazima wajibu hoja za lissu. Kwa bahati mbaya viongozi hao ni butu sana kujibu hoja za mhe lissu. Mfano katibu mwenezi ccm taifa ni butu sana kwenye uongozi. Anajisifia kwamba "anajua kiingereza kuliko lissu "swali gumu. Je, ni nani anayemzuia kwenda kwenye kipindi cha Hard talk???
Mbaya zaidi maccm yakifeli kwenye miradi yao wanaweka kusingizia kwamba kuna mwanasiasa mmoja(mhe lissu )anatumwa na mabeberu kuichafua nchi yetu!! Nani mzalendo wa kweli kati ya aliyejenga uwanja chato na anayetetea masilahi ya wananchi wanyonge??
Watanzania tumeshuhudia kila Siku matembezi ikulu kana kwamba ikulu ni ofisi ndogo ya vikoba!! Ikulu imeshushwa hadhi kwasababu ya kutaka kuaminisha umma kiholela kwamba hakuna kiongozi yeyote anayeweza kuliko rais , hii ni njia haramu kuweka mitizamo hasi kwamba anayepinga na kuhoji kama lissu si mzalendo nchi hii. Huu ni uongo wa wazi kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna damu zingine huwa hazimwagwi hovyohovyo mpaka akuruhusu mwenyewe, sasa mpaka na yeye amwage damu zao ndiyo salama ya ndugu zao wakati wao wapo kaburini
 
Anaandika Profesa Joseph Mbele

Mimi ninaufahamu vizuri utamaduni wa vyuo vikuu vya Marekani, kwa sababu nilisomea kule na ninafundisha kule. Nimeshatoa mihadhara katika vyuo vingi, sio Marekani tu bali sehemu mbali mbali za dunia.

Ninavyosikiliza mahojiano na hotuba za Tundu Lissu ninafahamu fika kwamba ataamsha fikra za wasikilizaje wake kwa kiwango cha juu. Ninafahamu pia kwamba katika vyuo vya Marekani, hawamwaliki mtu kwa ajili ya kumsikiliza tu, bali pia kwa ajili ya kumpiga masuali. Mtu anatoa hotuba halafu anakalishwa kitimoto.

Tundu Lissu ni hodari kwa yote hayo. Wanaombeza hapa Tanzania wanajisumbua. Kwa kusema hivyo, simaanishi kwamba mawazo yangu ni sawa na ya Tundu Lissu. Kuna ambayo ninatofautiana naye.

Lakini kutofautiana mitazamo ndio utamaduni wa watu wanaofikiri. Ndio utamaduni wa watu walioelimika. Vyuo vikuu ni mahali ambapo tunatofautiana na kulumbana muda wote. Ni uhai wa vyuo vikuu. Ni uhai wa taaluma. Tunawajibika sisi waalimu kujenga tabia hiyo miongoni mwa wale tunaowafundisha.

Kuna haya madai kwamba Tundu Lissu anaichafua nchi. Binafsi, sijawawahi kuona popote au siku yoyote ambapo Tundu Lissu ameichafua nchi. Anazilalamikia mamlaka za nchi, kama vile serikali na Bunge. Lakini serikali si nchi. Bunge si nchi. Anapomshutumu Spika, haichafui Tanzania. Spika si Tanzania.

Ingekuwa vinginevyo, basi kwa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoandika kitabu cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania" tungesema kwamba ameichafua nchi. Mwalimu anaiponda CCM na serikali yake, hadi kutamka kwamba kuna kansa katika CCM. Hadi akasema kwamba alitamani kitokee chama cha upinzani kilicho bora kuliko CCM ili kishike nchi badala ya CCM. Lakini itakuwa ni upuuzi kusema kuwa Mwalimu Nyerere aliichafua nchi.

Binafsi, siku nitakapoona Tundu Lissu anaichafua nchi, sitamlazia damu. Lakini sijaona. Badala yake, nimemsikia akitangaza kwamba yuko tayari kuitumikia nchi katika nafasi ya uongozi, iwapo atapata ridhaa. Ameelezea kuwa akishika uongozi, ataweka utawala wa sheria, haki za binadamu, na demokrasia. Kila mwenye kuwania uongozi wa nchi ana haki na wajibu wa kutueleza ana malengo gani. Kwa hayo malengo yake, sioni mantiki yoyote ya kusema kuwa Tundu Lissu anaichafua nchi.
Well Professor

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi hii kwa mara ya kwanza katika historia yake imempata Waziri wa Fedha na Bwana Fedha wa nchi. Bwana Fedha anagawa Fedha za umma kama zake. Leo tena kagawa 200m kwa Channel Ten. Usiniambie ni za CCM!!! Tutaleta mkeka (Ndugai: 9:1-2).
 
Nchi hii kwa mara ya kwanza katika historia yake imempata Waziri wa Fedha na Bwana Fedha wa nchi. Bwana Fedha anagawa Fedha za umma kama zake. Leo tena kagawa 200m kwa Channel Ten. Usiniambie ni za CCM!!! Tutaleta mkeka (Ndugai: 9:1-2).
Ndo maana tunasema ikulu si ofisi ya umma tena bali ni ofisi ya familia ya mkulu. Hizo fedha ni za umma %.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Prof buuana wewe si umeshaita wanao tofautiana naye ni kumkejeli. TL anatumikia hao wanaomtuma, Kauita ushoga ni ufaragha ndani ya katiba ya JMT akaacha kusema ni kosa la jinai linalo hukumiwa.
Kwani Msimamo wa CCM kuhusu ushoga ukoje? Halafu ujue ushoga si tu mwanaume kuingiliwa kinyume cha maumbile, bali ni zaidi ya hapo!!
 
Profesa wa ukweli sio wachumia tumbo kama kina kabudi ,kitila na wale waliohudhuria kongamano la jiwe pale chuo kikuu waliochanwa na sugu bungeni .
 
1549367006418.png

Profesa Mbele akiongea na "Beberu" aliyefika kwenye meza yake wakati wa Tamasha la vitabu kwenye nchi Kuu ya Mabeberu Marekani. Kumbuka wengine huogopa kwenda kwenye nchi za mabeberu kwa kuwa hawajui kwa ufasaha Lugha na maisha ya watu kwenye nchi za Mabeberu.
 
Prifessor kanifurahisha eti Lissu akimsema Spika,Spika siyo nchi.
Akilisema Bunge,Bunge siyo Nchi.
Akiisema sema serikali,Serikali siyo Nchi.

Naomba km kuna member anaijua I'd ya Jiwe amtag aje asome hili bandiko linamfaa sana. Najua Jiwe ni member hapa jf.

Sent using Jamii Forums mobile app


Wala usipate wasi wasi hii itafanyiwa copy kwenye Whatsapp itazunguka mtu wa kwanza kumfikia ni Bashite ndipo ataanza kubwabwaja maana yule ni ZERO yaani 0+ hakuna ajuacho zaidi ya kubana kalio
 
Back
Top Bottom