Prof. Mbele: Tundu Lissu haichafui nchi, kumsema Spika wa Bunge na Serikali sio kuichafua nchi. Hata Nyerere alisema CCM ni kansa

Anaandika Profesa Joseph Mbele

Mimi ninaufahamu vizuri utamaduni wa vyuo vikuu vya Marekani, kwa sababu nilisomea kule na ninafundisha kule. Nimeshatoa mihadhara katika vyuo vingi, sio Marekani tu bali sehemu mbali mbali za dunia.

Ninavyosikiliza mahojiano na hotuba za Tundu Lissu ninafahamu fika kwamba ataamsha fikra za wasikilizaje wake kwa kiwango cha juu. Ninafahamu pia kwamba katika vyuo vya Marekani, hawamwaliki mtu kwa ajili ya kumsikiliza tu, bali pia kwa ajili ya kumpiga masuali. Mtu anatoa hotuba halafu anakalishwa kitimoto.

Tundu Lissu ni hodari kwa yote hayo. Wanaombeza hapa Tanzania wanajisumbua. Kwa kusema hivyo, simaanishi kwamba mawazo yangu ni sawa na ya Tundu Lissu. Kuna ambayo ninatofautiana naye.

Lakini kutofautiana mitazamo ndio utamaduni wa watu wanaofikiri. Ndio utamaduni wa watu walioelimika. Vyuo vikuu ni mahali ambapo tunatofautiana na kulumbana muda wote. Ni uhai wa vyuo vikuu. Ni uhai wa taaluma. Tunawajibika sisi waalimu kujenga tabia hiyo miongoni mwa wale tunaowafundisha.

Kuna haya madai kwamba Tundu Lissu anaichafua nchi. Binafsi, sijawawahi kuona popote au siku yoyote ambapo Tundu Lissu ameichafua nchi. Anazilalamikia mamlaka za nchi, kama vile serikali na Bunge. Lakini serikali si nchi. Bunge si nchi. Anapomshutumu Spika, haichafui Tanzania. Spika si Tanzania.

Ingekuwa vinginevyo, basi kwa jinsi Mwalimu Nyerere alivyoandika kitabu cha "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania" tungesema kwamba ameichafua nchi. Mwalimu anaiponda CCM na serikali yake, hadi kutamka kwamba kuna kansa katika CCM. Hadi akasema kwamba alitamani kitokee chama cha upinzani kilicho bora kuliko CCM ili kishike nchi badala ya CCM. Lakini itakuwa ni upuuzi kusema kuwa Mwalimu Nyerere aliichafua nchi.

Binafsi, siku nitakapoona Tundu Lissu anaichafua nchi, sitamlazia damu. Lakini sijaona. Badala yake, nimemsikia akitangaza kwamba yuko tayari kuitumikia nchi katika nafasi ya uongozi, iwapo atapata ridhaa. Ameelezea kuwa akishika uongozi, ataweka utawala wa sheria, haki za binadamu, na demokrasia. Kila mwenye kuwania uongozi wa nchi ana haki na wajibu wa kutueleza ana malengo gani. Kwa hayo malengo yake, sioni mantiki yoyote ya kusema kuwa Tundu Lissu anaichafua nchi.
Mtu ambaye ni Msomi wa kweli utamjua tu ni mwepesi wa kuchanganua mambo kwa weledi mkubwa kama alivyofanya Profesa Mbele, cha ajabu na cha kushangaza sasa wanaojiita Wasomi huko CCM akina Dr Bashiru na wenzao wamekariri Akili za cyprian Musiba Le mutuz na Bashite wasio na vyeti wala Upeo na kibaya zaidi kule bungeni wanaojiita wasomi wa CCM nao wamekariri Akili za Livingston Lusinde ( kibajaji) na Msukuma ni maajabu ya Dunia, Wanaojiita Wasomi CCM 80% ni wasomi wasiojielewa ama wamesahau walichokisomea kama proselii Lipumba ambaye sasa kichwani kasalia na Elimu ya Darasa la nne ya kutengeneza uchonganishi umbea kuvuruga vyama, propaganda za kijinga jinga kishamba nk
 
Ahsante Profesa Mbele.Umetoa elimu ya bure kwa wale wasomi wenzio wanaofikiri kwa kutumia tumbo na mdomo na sio akili.Wamekumbwa na mihemuko ya kimaslahi na siasa majitaka na kuishia kutukana na kupayuka badala ya kutoa hoja au kujibu hoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaojiita wasomi CCM wengi ni vilaza walisoma kijanja kwa kuiba mitihana kununua vyeti na wengi wamesahau walichokisomea kama profesa Kapuya na wenzake akina lupumba bashiru na Waziri wa sheria, Wanaojiita wasomi huko CCM wamewadharau watanzania kwa kiwango cha kutisha ndiyo maana huwaletea Sinema za kijinga kila siku wakiamini hawatajua chochote, Mfano halisi ni hii Tabia ya kishamba eti wazungu wakiongea na Wapinzani huwaita ni mabeberu lakini cha kushangaza hao hao wazungu wakienda ikulu huitwa ni Wanaume na wakitoa misaada kwa CCM huitwa ni wafadhili na Nchi rafiki, kwa CCM wazungu ni wafadhili lakini kwa Wapinzani huitwa mabeberu ni Aina Fulani ya propaganda za dharau kwa wananchi kwani CCM imewaona hawana Akili ndiyo maana wanawachezesha ngoma za CCM kwa nguvu pasipo kujali kuwa watanzania wa sasa wana Akili kuliko CCM wote.
 
Wasomi kwa CCM ambao bila fikra zao kusikilizwa ni vigumu chama kwenda mbele ni hawa wafuatao 1- cyprian Musiba 2-Le mutuz 3-Daud Albarty Bashite 4-Livingston kibajaji 5- Msukuma 6- polepole 7-simbachawene 8- mwigulu nchemba 9- kigwangala 10-ingizo jipya ni DC wa kigamboni 11- RC mnyeti 12- RC Gumbo na wenzao, hao ndiyo Wasomi tegemezi huko CCM wanategemewa sana bila wao hakuna chama ingawa bado ile kauli mbiu ya zidumu fikra za Mwenyekiti wa CCM inatumika huko CCM lakini mshauri mkuu wa fikra za Mwenyekiti ni Daud Arbaty Bashite kwa hiyo bado inazunguka humo humo kwa hao wasomi tegemezi wa CCM.
 
Back
Top Bottom