Prof. Mbarawa ni Presidential material! Tuwaspot na kuwagroom Presidential materials au tumwache tu yeyote awe?

Huyu wa sasa sio kabisa....na hata washauri wanashindwa kumshape.

Ndio maana umekuja na justification ndefu.

Hata Msekwa alikataa hoja ya Nkamia kwa kusema kuwa miaka kumi inatosha kuvumilia a none presidential person (kama huyu wa sasa)
Tunajua bavicha kila kitu ni bora jana.
 
Prof namkubali sana haswa mtazamo wake kwenye mambo ya msingi kitaifa
Ni mapema mno kumtamkia haya ili wabaya wasije wakajiinua dhidi yake lakini itoshe tu kusema ni mchapa kazi mzuri na mwenyezi Mungu aendelee kumpigania ili aweze kutimiza majukumu yake kwa ukamilifu wake
INSHALLAH
 
Mkuu Pasco, unataka kusemaje hapa? Ya kuwa tuliyenaye ni tulimwacha tu akapata na yakuwa hana uprezooo material
 
watu wa bara wameitawala zanzibar mfululizo,mkapa,kikwete,magu

natarajia mpambano mkali na mtoto wa mwinyi ambaye ni waziri wa ulinzi

pia mbarawa ajiepushe na kundi la kipara,maana linapingwa sana

pia nashauri apewe muda awe waziri wa mambo ya nje akapate uzoefu,tunaona wa sasa anavyoyumba katika siasa za kimataifa
Awe waziri wa foreign affairs Kwani ni mvaa Kaunda?
 
Tukitaka tupate rais bora cha kwanza kabisa KATIBA MPYA cha pili wananchi tukibadilika kutoka kwenye vyama hadi kwa mtu tunae muhitaji..kwani kwa mfumo wetu wa Tz hatuchagui mgombea urais ila wananchi tunachagua CHAMA kipi kiwe madarakani...
 
Mm nashindwa kuwaelewa wafuasi wa Upinzani, Mara mnasema 2020 mnachukua Ikulu?

Mama Samia Suluh akichukua nchi, nafikiri ataifikisha mbali sana naona kama mtu mwenye busara sana
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali,
Naanza kwa swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Yoyote Anayeutaka Urais, Awe Hata Kama Sio Presidential Material?.

Sifa za Urais wa Tanzania.
Nafasi ya urais wa JMT, inashikwa na raia yoyote wa JMT mwenye sifa na vigezo. Tangu JMT imezaliwa mwaka 1964, hadi leo Zaidi ya miaka 53, ni Mtanzania mmoja tuu kutoka Zanzibar, aliyekidhi sifa na vigezo hadi kuweza kuwa rais wa JMT, Wazanzibari wengine wote wenye sifa waliojaribu, hawakuweza kupata kutokana na kuzidiwa sifa na vigezo na wagombea kutoka bara, matokeo yake hadi leo sisi bara ni 4 kwa 1 Zanzibar. Hali hii ilipelekea nikashauri
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuwa Rais wa JMT?

Lakini leo, baada ya kumsikiliza Mtanzania huyu ambaye ni Mzanzibari, kiukweli kabisa, nimemkubali sana kuwa ana kidhi sifa na vigezo hadi sifa za ziada za nationalism ya Utanzania kwanza, na ni mzalendo wa kweli, kwa sababu kwa kauli na matendo, amethibitisha pasi shaka kuwa yeye kwanza ni Mtanzania, kisha ni Mzanzibari, wakati kiukweli kabisa, kwa Wanzanzibari walio wengi, wao kwanza ni Wazanzibari kwanza, kisha ndio Watanzania.

Hebu msikilize Prof. Mbarawa.


Tuwachagize Presidential Materials Wagombee?.
Kuna Watanzania wengi wenye sifa za kutuletaa rais bora kabisa, lakini wengine hawana vyama, wengine wala hawauwazi urais, hivyo wanapotokea watu wenye sifa kama Prof. Mbarawa, unaweza kukuta ndio wale type ya watu hawauwazii hata huo urais, lazima wachagizwe, hata katika hao wagombea Zaidi ya 40 wa CCM ile 2015, sio wote waliutaka urais, kuna baadhi walifuatwa na kuchagizwa kwenda kuchukua fomu na kugombea, hivyo mnaonaje wale wote wenye presidential personalities, or presidential materials, tuwachagize waanze kufikiria kugombe.

Hitimisho, Tusisubiri Marais Wajitokee Tuu, Tuanze Kutengeneza Marais.
Kuna kauli isemayo, leaders are born and not made, Mimi ni muumini wa good leaders are made, besides kuwa born, hivyo lets start making our leaders by grooming them to be good leaders. Kwa upande wangu kwa 2020, nimeishamspoti mmoja kutoka upinzani,
Tundu Lissu ndiye asimame na Magufuli 2020? ...Ameonyesha ...

Na kwa 2025, niliishamspoti mmoja.
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa ... - jamiiforums.com
huyu Prof. Mbarawa ni wapili, tuendelee kuwaibua presidential materials ili kufikia 2025, tupate viongozi bora, japo mimi binafsi niko kwenye lile kundi tunaotaka 2025 katiba ibadilishwe Magufuli aendelee kama nilivyouliza hapa.
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa ...

Namalizia kwa lile lile swali la msingi, Jee Tanzania, Tuanze Utamaduni wa Kuwaspoti Watanzania Presidential Materials, na KuwaGroom ili Tupate Rais Bora, Au Tuendelee Kuwaacha Tuu Yoyote Anayeutaka Urais, Awe Hata Kama Sio Presidential Material?.
Jumamosi Njema,

Paskali[/QU
Prof ametisha
 
Huku kwetu zanzibar tulimpiga chini ubunge. In short hana sifa hata ya kua shekha huku zanzibar alibebwa tu na Rais sababu swahiba wake. Mtazame tena 2020 labda huko bara.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom