TANZIA Prof. Mathew Luhanga, aliyekuwa Makamu Mkuu wa UDSM kuanzia 1991 hadi 2006 afariki dunia

Yes!!! Tanzania hakuna prof zaidi yake na mark mwandosya.
Wengine wanapeana tu.
Mtu akikusimamia afu anakuchukia ama hakupendi anatafuta sababu za wewe kukuangusha.
Kuna story Dr Mfinanga na Masaoe mmoja akampeleka mahakamani Mana anambania mwenzake asiwe dokta.
Hata Dr Nyaoro aliukataa Prof Mana ni kupeana Kama wanavyopeana vyeo ,teuzi, kazi, n.k mpaka ujishushe ujinyenyekeze. Prof kanyimwa penzi Mara Caroline akadisco in Roma voice.

Pumzika kwa amani baba,profesa, mtumishi uliyetumikia Taifa lako na kuzalisha watalaamu wanajidai walipo.
Kati ya hao wawili nani alikuwa anabaniwa? Maana Dr David Mfinanga tunamfahamu vizuri sana. He is exceptional!!
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye anasikitika kutangaza kifo cha PROF. MATTHEW LUHANGA, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1991 hadi 2006, kilichotokea jioni ya leo tarehe 16.09. 2021. Tunatoa pole kwa familia, Chuo chetu na Tanzania kwa ujumla. Taarifa zaidi tutaendelea kujulishana. Tumwombee apumzike kwa Amani. Amina.

Dkt. Dotto P. Kuhenga, Mratibu wa Mawasiliano na Habari, UDSM.

View attachment 1941008

=======

Professor Matthew Luhanga ndie Mwanasayansi wa Zama hizi mwenye historia iliyotukuka duniani
Tulianza kumuita profesa mwanzoni mwa miaka ya sitini tukiwa naye N. A. Middle School Mbeya, alikuwa Time Keeper wa shule ni mdogo wake Elijah B. Luhanga aliyewahi kuwa mkurugenzi wa Tanesco.
MUNGU AWE NAYE DAIMA.
 
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye anasikitika kutangaza kifo cha PROF. MATTHEW LUHANGA, aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1991 hadi 2006, kilichotokea jioni ya leo tarehe 16.09. 2021. Tunatoa pole kwa familia, Chuo chetu na Tanzania kwa ujumla. Taarifa zaidi tutaendelea kujulishana. Tumwombee apumzike kwa Amani. Amina.

Dkt. Dotto P. Kuhenga, Mratibu wa Mawasiliano na Habari, UDSM.

View attachment 1941008

=======

Professor Matthew Luhanga ndie Mwanasayansi wa Zama hizi mwenye historia iliyotukuka duniani
IMG-20210917-WA0017.jpg
 
Prof. Luhanga akiwa VC iliishauri serikali itilie mkazo sana kwenye elimu ya chekechea na msingi badala ya sekondari, kufeli kwetu kwenye elimu kunatokana na wanafunzi kuanza kujifunza kusoma, kuhesabu na kuandika wakiwa sekondari tofauti na enzi za mkoloni. Alitoa ushauri huo wakati huo baada ya kuona kiwango cha elimu ya wanafunzi wanaoingia chuo kikuu hairidhishi.
 
Mpumzike kwa amani pamoja na msaidizi wako Prof. Mayunga Nkunya. Daima nitawakumbuka kwa ile hotuba yenu tamu na iliyo tukuka siku ya kutukaribisha First Year 2005!

Nakumbuka sana siku ile mlituusia kitu hiki "Graduate with A's and not with AIDS" Huu msemo ulikua ni mpya kabisa kwangu ukichukulia nilikua nimetokea kijijini, halafu moja kwa moja mpaka Udsm!
 
Nakumbuka siku moja tukiwa Mlimani UDSM, nilimsikia akisema alikuwa ana mheshimu Prof. Mark James Mwandosya tu!!!

R.I.P Prof. Mathew Luhanga!
Hata mm nilikuwepo siku hyo, alisema huwezi kuwa professor wa kiswahili au development study kisha ukajisifu eti ww ni professor! Nchi hii maprofessor tumebaki wawili tu mm na mwingine hayupo hapa anaitwa mark mwandosya" mbele ya jk na asha rose migiro nafikiri kulikua na uzinduzi wa coet kama kumbukumbu zangu ziko sahihi.
 
Back
Top Bottom