Prof. Mark Mwandosya: Kikwete aliniteua kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu hadi 2020, leo Msekwa anachukua nafasi hiyo..

Magufuli kama Rais ana haki ya kuteua na kuamua yupi afanye nae kazi na yupi ampumzishe. Mwandosya alikuwepo serikalini tangu enzi za Mzee Ruksa vipi hajatosheka tu?
 
Tena mm ningekuwa JPM, ningemfuta kazi siku nyingi huyu Prof. uchwara, kaiua TTCL, Airtel alifanya ufisadi na bado akawa anapinga maendeleo serikali awamu ya 5 inayofanya.. Mm ningemfyekelea mbali muda, sana.. JPM kambeba beba, mm singefanya hivyo.. unipinge pinge huku nikijua ume fisidi sana na nikuache ulipwe mshahara bure bure.. Nakufyeka kabisa
Chuki kwa Mwandosya haitabadilisha mchango wake kwa Tanzania wala haitapunguza akili Mungu alizompa. Prof. Tenda mema nenda zako ukisubiri shukrani nakusikiliza watu kama hao utachelewa
 
Hivi mwandosya awe tishio kwa Magu kwa kipi hasa alichofanya Mwandosya! mi naona anabebwa tu mpaka aliwai kuwa waziri asiye na wizara maalum banah!
Alipewa wizara maalum kwasababu ya afya. Alikua ametumikia sana taifa lake akiwa mzima.
 
Sema mzee atakuwa na maneno ya chini chini sana....na mafumbo kwenye social media....na yale mapicha kapiga na kina Sugu!!!...nikajua achukui round huyu....
 
Hata hao wanaoteuliwa sasa sina hakika kama wanafurahia teuzi hizi, maanake hazina nafasi ya kufanya kazi bila kila mara kuwa na wasiwasi kama utendaji wao utahojiwa.

Kwa maana nyingine ni kama kuwekwa kizuizini. Mteuliwa hana uhuru tena wa chochote, si mawazo, wala kushiriki katika makundi.

Kinachoangaliwa sasa kwenye teuzi au tenguzi sio kazi inayofanywa, bali kiasi cha kumsujudia mteuzi!

Hii katiba inayoruhusu mtu mmoja ajibinafsishie kila kitu haiwezi kutufikisha popote kama taifa.
 
Back
Top Bottom