Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,433
- 7,055
Hii inafikirisha! NI kwamba Prof. anaondolewa kiaina kwenye utawala wa JPM?
Picha lilianzia hapa >> Prof. Mark Mwandosya aenguliwa Uenyekiti Bodi ya chuo cha Mwalimu Nyerere; nafasi yake apewa Stephen Wasira - JamiiForums
Kisha leo ikafuatia >> Rais Magufuli afanya uteuzi wa Viongozi mbalimbali wa Taasisi za Umma - JamiiForums
Baada ya nafasi yake kunyakuliwa tena, Prof. amefunguka ya moyoni;
"Aprili 2014 Mhe. Kikwete aliniteua Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya kwa kipindi kinachoisha 2020. Mhe. Pius Msekwa anachukua nafasi hiyo kuanzia leo. Nampongeza. Nashukuru kwa heshima ya kuwa Mlezi Mkuu wa Chuo. Asanteni jumuiya ya Chuo kwa ushirikiano mlionipatia". Prof. Mark Mwandosya.
Kwa wanaomfuatilia Profesa huko mitandaoni, watabaini ni kwa kiasi gani amekuwa mkosoaji mkubwa wa madudu yanayofanyika katika serikali hii ya awamu ya 5. Je, huenda hilo ndilo limepelekea muda wake ''kukatishwa' na kuondolewa kabisa kwenye utawala wa bwana mkubwa?