Prof Mark Mwandosya Azushiwa Kifo!

Makyomwango

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
322
79
Wana jamii

Jana zilienea habari juu ya kufariki kwa waziri w maji Prof Mwandosya katika mikoa ya Mbeya na Dar es Salaam. hata hivyo baada ya kufuatilia niliweza kuongea na mtu wa kalibu naye ambaye alinieleza kuwa alikuwa ameongea na prof pamoja na mke wake mida ya saa 1:30 usiku wakiwa wachangamfu.

nawaomba watu walio kalibu na familia ya prof waendelee kutujuza maendeleo ya kiafya prof huko india. naomba pia tuendelee kujuzwa juu ya hali ya kiafya ya Dr Mwakyembe anayesadikiwa kalishwa sumu na kupelekwa india

nawasilisha
 
Kazi ipo mwaka huu, naona ccm haiowataki watu wa Mbeya, lakini ccm waangalie wanakotupeleka coz hatuta kubali ndugu zetu wafe coz ya maslahi binafsi. Naona nchi hii sasa inatakakuendeshwa kigaidi na hawa ccm. Ccm ole wenu narudia tena ole wenu.
 
Dah, wanazusha ili wamalizie. Mafisadi wana nguvu nchi hii. Tusubiri, tutasikia, watu wako kazini.
 
kunataarifa nimeiona kwenye facebook,mtu anamjulisha rafiki yake kuwa prof hatunaye tena hizi taarifa ni za kweli jamani?naomba mwenye taarifa atujuze,na kama ni kweli taifa limepoteza mtu
 
tataizo hakuna update yeyote ya viongozi wetu wanapo ugua,website ya nchi au bunge ilitakiwa kutueleza kila siku kuwa mbunge fulani au waziri anaumwa na maendeleo yake.update from juu zinatakiwa.
 
Wana jamii

Jana zilienea habari juu ya kufariki kwa waziri w maji Prof Mwandosya katika mikoa ya Mbeya na Dar es Salaam. hata hivyo baada ya kufuatilia niliweza kuongea na mtu wa kalibu naye ambaye alinieleza kuwa alikuwa ameongea na prof pamoja na mke wake mida ya saa 1:30 usiku wakiwa wachangamfu.

nawaomba watu walio kalibu na familia ya prof waendelee kutujuza maendeleo ya kiafya prof huko india. naomba pia tuendelee kujuzwa juu ya hali ya kiafya ya Dr Mwakyembe anayesadikiwa kalishwa sumu na kupelekwa india

nawasilisha
Usipende wala kushahabikia kuchuria watu kifo
 
kunataarifa nimeiona kwenye facebook,mtu anamjulisha rafiki yake kuwa prof hatunaye tena hizi taarifa ni za kweli jamani?naomba mwenye taarifa atujuze,na kama ni kweli taifa limepoteza mtu

una tatizo la kisaikolojia!. .kama zipo taarifa rasmi utazipata ila za feisibuku zitakutia aibu ipo siku
 
Hivi bado hajaponaga tu!miezi minne sasa imeisha!kulikon Mbeya?Mwakyembe mgonjwa,Mwandosya mgonjwa,jana mwigine kakamatwa kwa kutishia kuua!Ni vp nyie watu huko,kuna tatizo gani?
 
Kama haka kamchezo kanafanywa na wale mafisadi kazi ipo.
Ndio maana tuliambiwa mafisadi hawafai kugusa.
 
Kazi ipo mwaka huu, naona ccm haiowataki watu wa Mbeya, lakini ccm waangalie wanakotupeleka coz hatuta kubali ndugu zetu wafe coz ya maslahi binafsi. Naona nchi hii sasa inatakakuendeshwa kigaidi na hawa ccm. Ccm ole wenu narudia tena ole wenu.
Unanikumbusha vile vi mbwa vidogo ambavyo havikupata kunyonya vizuri,,, hivi huwa vinabweka hovyohovyo,, kikiona nguo imeanikwa kinabweka,, kikiona mbalamwezi kinabweka,, hata kikiona mkia wake tu kinabweka.. Sasa ni sawa na wewe na wengine wenye akili kama yako,, kila kitu CCM,, ukose pesa kwa kutojishughulisha,, ccm, uachwe na mumeo...ccm....upupu mtupu
Acheni ujinga nyie!! mnaboa sasa
 
kunataarifa nimeiona kwenye facebook,mtu anamjulisha rafiki yake kuwa prof hatunaye tena hizi taarifa ni za kweli jamani?naomba mwenye taarifa atujuze,na kama ni kweli taifa limepoteza mtu
Next time, unakuja na link, ili tuifatilie authenticity yake.
 
Mods naomba hii thread ifungwe mara moja. Hatujaishiwa hoja kiasi cha kuleta tetesi za aina hii humu. Kwanini jukwaa liwe la teteai jamani. Oooh Mwakyembe Kalishwa sumu mara ooh Mwandosya kafa. Mwisho tutaambiwa Yesu karudi sasa!
 
Samahanini wakuu ndo maana nimeweka alama ya kuuliza sikuwa na uhakika,samahani sana kwa wale nilio wakwaza
 
Back
Top Bottom