January 23, 2020
Profesa Makame Mbarawa - ''Wizara ya Maji Hakuna Uadilifu na Hatuwapendi Watanzania, Changamoto za Maji Tanzania wizarani Wakurugenzi, ma-Consultant, Wahandisi hawazijui'
Prof. Makame Mbarawa amesema watalaamu wake walioko wizarani hawajui miradi iliyopo bali wanakaa ofisini sana.
Alisema hayo alipokutana na Bodi ya Maji na Waziri kutoa mrejesho wa ziara zake Tanzania nzima. Ziara ya Mh. Makame Mbarawa imegundua na kumfundisha kuwa serikali inapoteza mabilioni ya shilingi kwa wakandarasi kutoa makadirio yaliyo zaidi ya gharama halisi kwa zaidi ya 100% na kuendelea.
Mfano mmoja Mh. Mbarawa Makame alitumia case study halisi kutokana na ziara zake, ni mradi mmoja ulikadiriwa na wataalamu kugharamia shilingi bilioni 16.
Lakini baada ya kukaa na mkandarasi na kupitia upya gharama zake ziliteremka mpaka shilingi bilioni 10 yaani serikali katika mradi huu mmoja ilikuwa inapoteza zaidi ya bilioni 6 kutokana na kuzidishwa makadirio ya mradi huo.
Waziri amesema hata kama serikali ikiipa wizara trilioni ya shilingi matatizo ya maji hayawezi kutatuliwa na kumalizia maana makadirio (estimation) hayana uhalisia na ni ya juu mara 4 ya gharama halisi.
Mh. Mbarawa alisema miradi mingi ya maji inayoteketeza pesa zaidi kuliko uhalisia ni iie iliyopo pembezoni mwa nchi yetu kama mikoa ya Mtwara , Ruvuma, Rukwa na Kigoma kwa kutaja kwa uchache.
Miradi hii mingi haitembelewi na wataalamu wa wizara waliopo makao makuu. Mh. Mbarawa kutaka kuthibitisha hilo aliutaja mradi mmoja wa majina kuwataka wanabodi kuutaja mradi huo upo wapi na unagharimu kiasi gani.
Hakuna aliyeweza kujibu swali la Mh. Mbarawa na waziri akasema hilo ni thibitisho kuwa wataalamu wanakaa sana ofisini na hawaelewi nini kinaendelea katika miradi ya maji nchini.
Mwisho Mh. Makame Mbarawa akasema dhuminu ya ziara yake kila kona ya nchi ilikuwa kujifunza changamoto za miradi ya maji nchini na hilo litamsaidia kutimiza wajibu wake vizuri.
Hivyo ametoa rai kwa wataalamu wa maji kutoka ofisini na kukagua miradi ili kuhakikisha fedha za umma wazipotei bure kwa wakandarasi kukadiria bajeti isiyo halisi.
Waziri anamalizia wataalamu wakitimiza wajibu wao kama alivyo-share alichojifunza katika ziara zake basi kwa bajeti iiliyopo wananchi wengi zaidi watapata huduma ya maji na tatizo la maji nchini kuwa kumalizika na kuw historia.
Source: Millard Ayo