Prof. Makame Mbarawa atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme

Jay Milionea

JF-Expert Member
Apr 19, 2015
1,185
154
Profesa Makame Mbarawa atengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ametengua uteuzi wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mhandisi Marcellin Benedict Magesa kuanzia Februari 18 mwaka huu.

Profesa Mbarawa amechukua hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa sababu mbalimbali zikiwemo, kushindwa kusimamia matengenezo ya magari na mitambo ya Serikali nchini, kushindwa kusimamia uendeshaji wa matenegenzo ya vivuko vya Serikali nchini pamoja na kushindwa kusimamia ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali.

‘’Mhandisi Marcellin Benedict Magesa atapangiwa majukumu mengine wizarani Na hivyo namteua Mhandisi Manase Lomayani Le-Kujan kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuanzia Leo hii ’’, alisema Profesa Mbarawa.

Aidha, Profesa Mbarawa amemuagiza Kaimu Mtedaji Mkuu huyo aliomteua kutekeleza mara moja mambo mbalimbali, ikiwemo kutengeua uteuzi wa Mkurugenzi anayeshughulikia matengenezo ya magari ya Serikali, Mhandisi Prisca Benedict Mukama na kumpangia majukumu mengine, pia kutengua uteuzi wa Meneja wa Karakana ya Magari ya Serikali (M.T Depot), Mhandisi John Alexander Mushi na kumpangia majukumu mengine.

Kabla ya uteuzi wake, Mhandisi Manase Lomayani Le-Kujan alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Ufundi na Ushauri katika Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).
 
Kwa hiyo huyo anayechukua hiyo nafasi yeye ana tofauti gani? si alikua hapo hapo tena mtendaji?

Hizi drama zinajenga au zinabomoa? time will tell
 
Hao TEMESA wana NISSAN new model VXV8, unajiuliza ni nani alipitisha ununuzi wa gari la namna hiyo
 
MAGUFURI HAPA AMETUMBULIWA KWANI HAWA WALITEULIWA NA MAGUFURI KAMA SIKOSEI
 
MAGUFURI HAPA AMETUMBULIWA KWANI HAWA WALITEULIWA NA MAGUFURI KAMA SIKOSEI

Basi kama ndiyo hivyo ni Magufuli mwenyewe kawatumbua. Maana mtumbuaji wa sasa, Prof. Mbarawa na mteule wa Magufuli
 
Tanzania ni movies zinaendelea kumbe amehamishwa baada ya kushindwa huko
 
Back
Top Bottom