Prof. Makame amteua mwenyekiti wa bodi ya ushauri wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA)

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.

Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo.

Pamoja na uteuzi huo Profesa Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania ambapo John Bura – Mkandarasi kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango
 
Mtoa mada naomba kirefu cha TBA kwa hapa maana kinachonijia kichwani kwangu ni Traditional Birth Attendant (TBA) ...... nisaidie tafadhali.

Zaidi ya hilo nawapongeza walioteuliwa na kuwatakia kazi njema
 
Kuna Ngwale pia wa DS UDSM ingawa simkumbuki first name yake
 
Mtoa mada naomba kirefu cha TBA kwa hapa maana kinachonijia kichwani kwangu ni Traditional Birth Attendant (TBA) ...... nisaidie tafadhali.

Zaidi ya hilo nawapongeza walioteuliwa na kuwatakia kazi njema
Tanzania Building Agency [TBA]
 
  • Thanks
Reactions: Mj1
Back
Top Bottom