Prof. Maji Marefu Bungeni aonya waganga wa jadi kutodharauliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Maji Marefu Bungeni aonya waganga wa jadi kutodharauliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MVUMBUZI, Feb 14, 2011.

 1. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mbunge wa Korogwe Vijijini Mr. Ngonyani au almaarufu Prof. Maji Marefu ameanza rasmi kuchangia bungeni sasa hivi. Na katika shukrani zake amewapongeza waganga wa jadi wote nchini kwa kumwuunga mkono na kuwezesha kuchaguliwa kwake.

  Hii inamaanisha nini? ni kwamba huyu jamaa waganga au wachawi wamechangia kwa kiasi kikubwa katika kuchaguliwa kwake kuwa mbunge. Kwa maana nyingine huyu bwana ameingia bungeni kugombea maslahi ya waganga wenzake.

  Na ameanza rasmi kuwaonya wanaowadharau na kuwa donoa donoa waganga wa jadi. Ameonya kila mtu inampasa aheshimu fani ya mwenzake

  hii inanifanya ni amini kuwa hata waliopiga kura inawezekana kwa macho walionekana ni watu lakini kimazingaumbwe walikuwa ghosts na hii inaonyesha kwa mtaji huu atakuwa mbunge mpaka atakapoamua kuacha mwenyewe.
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hicho ndicho nilichotegemea toka kwake, kweli profession matter! UGANGA WA TUNGURI MPAKA UBUNGE? duh! Ndugu zetu wa korogwe realy wajamaa!
   
 3. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  we unashangaa huyu..mbona kuna mtu pale magogoni alipewa ulinzi wa majini na sheikh yahaya
   
 4. k

  kingmakusa Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 4, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo ndiyo tanzania na karne ya 21!
  wabunge wanaongelea tunguli!
   
 5. t

  the mkerewe JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  aache kutuletea upuuzi wake kwanza hawa waganga ndio chanzo cha mauaji ya albino.
   
 6. doup

  doup JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  PLz taja hata Herufi Mbili Za mwanzo, tulinganishe
   
 7. A

  Anaruditena Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndio CCM - na serikali yake. Watu wanasafiri na viti vya kukalia -hakuna hofu ya Mungu kabisa
   
 8. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280

  Una maanisha MKAAZI wa Magogoni pale WHITE HOUSE YETU au ?
   
 9. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #9
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Prof. maji marefu amekiri kabisa yeye fani yake ni mitishamba na akaonya live watu wenye tabia ya kuwa donoa donoa waganga wa jadi waache tabia hiyo.

  Ninachoona hapa bunge limeingiliwa kwani kuna siku mtu atakuja bungeni akiwa uchi au akiwa anatambaa.

  Ina maana watumishi wa Mungu akina Mch. Mama Rwakatare, wamefuatwa hadi chumbani. Tumtafute Huyu mama tumwuulize ameupokeaje huo ujumbe wa prof. wa mitishamba huku tukijua kwamba yeye ni mlengwa mkubwa
   
 10. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #10
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Kwani we hujui,mbona kila mtu alielewa hilo live, mchana kweupe mpango wa ulinzi wa Boss!!!!!!!!!!!
   
 11. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #11
  Feb 14, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hebu agombee na uraisi, atafute ghosts hata million mia kama atashinda!!
   
 12. doup

  doup JF-Expert Member

  #12
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Hah ha hah haaa Tet tet Te Te ! nimekusoma mkubwa
   
 13. Dyslexia

  Dyslexia Senior Member

  #13
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona husemi kuhusu yeye kuzungumzia kilimo,barabara na umuhimu wa kujenga bwawa watakalotumia kwa kilimo!!!!
  Ovyo sana,kuona mabaya ya wenzio tu!!!
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kwa jinsi bunge letu linavyopenda mambo ya kishirikina basi atapata wateja wengi sana safari hii ambao watakuwa wanahitaji kupigiwa ramri na vitu vingine.
   
 15. doup

  doup JF-Expert Member

  #15
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  mkuu usiseme hivyo, unaweza kwenda kwenye kisanduku cha kura na hasira zote kwamba iwe na iweje huumpigii kura kufika pale ndio kwanza unapowe vema ya ndio bila kujua ndio kwake. inabidi tujue huyu jamaa alishinda kwa kura ngapi huko jimboni kwake, tunaweza pata picha
   
 16. n

  ngoko JF-Expert Member

  #16
  Feb 14, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 574
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Anatetea fani yake tu , sawa na wasanii wengine kama Yusufu Makamba , JK n.k ambavyo hutetea fani zao
   
 17. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #17
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Tunazungumzia suala la kitaifa hapa kwani masauala ya barabara, mabwawa nk. ni wajibu wake mkuu katika jimbo lake. Lakini kwa hili la onyo kwa wanao wasema vibaya waganga ni la kitaifa zaidi na linamhusu hata mbunge wangu hivyo linatuhusu wote
   
 18. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #18
  Feb 14, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Yeye atapata wateja wabunge wengi zaidi kwani yeye ni LIVING EXAMPLE jinsi uganga ulivyomsaidia kupata ubunge. Nakuambia alichofanya leo kusema yeye ni mtaalamu wa mitishamba amefanya advataisi ya kwanza tena ndani ya bunge Live.
   
 19. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #19
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Kawaulize waliogo,bea naye kura za maoni watakwambia yaliyowapata.

  Kifupi jamaa walipokuwa wanapanda jukwaani walikuwa hawaioni hadhira so walishindwa kuendelea na hotuba zao,
   
 20. B

  Big Dady Member

  #20
  Feb 14, 2011
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ulitarajia sangoma aongelee nini zaidi ya maruhani na majini ya masangoma wenzake.
  Hiyo ndo faida ya kupeleka waganga jadi bungeni. Na hiyo ni maendeleeeeeeeeeeo.
   
Loading...