Prof Mahalu kuwakaribisha maaskofu Roma si udini. Balozi wetu ye yote wa Italy hawezi kulikwepa hili

Paschal Matubi

JF-Expert Member
Sep 15, 2008
235
302
Kwanza tazama kwa umakini picha hii ndipo uingie kwenye details zaidi

050820121037.jpg


Nimeona vyema kuanzisha a separate thread hii tofauti na ile ambayo sasa inaelekea page number four (Click here) kwa sababu ni ni ufafanuzi mahsusi kuhusiana na tuhuma za udini kwa aliyekuwa Balozi wa Italy, na sasa kesi yake inaendelea mahakamani, kwamba aliwakaribisha maaskofu wa Kanisa Katoliki huko Italy.

Thread ile inaeleka mtiririko wa kisiasa, hivyo mimi kama mkatoliki ninayeelewa baadhi ya taratibu zetu kuhusu maaskofu nifafanue kwa faida ya wengi.

Kwa utangulizi ukifungua link ile utaona sehemu ya post ile ilivyosema:

3: Kitendo chake cha kuwakirimu Ubalozini Maaskofu wa Kanisa la Katoliki waliotembelea Italia kilionekana kama kurasimisha UKRISTO wa Ubalozi pale Roma. Tuhuma hizi zipo sambamba na kile alichozusha Shehe na Mnajimu mmoja kwamba Balozi Mahalu ni adui wa Uislamu kwani Balozi Mahalu ndiye aliyetayarisha Memorandum of Understanding (MOU) kati ya Serikali na Kanisa ili Taasisi za Kikristo zilizokuwa chini ya Serikali zirudishwe na kuwa chini ya Kanisa kama ilivyokuwa awali.

Ukweli wa mambo uko hivi,

Utendaji ndani ya Kanisa Katoliki umetawaliwa na Sheria ziitwazo Canon Laws ambazo vifungu vyake hutajwa kama hivi Can. 143(1) yaani ni ibara ya 143, kifungu 1.

Can. 399(1) inasema hivi:

Every five years the diocesan Bishop is bound to submit to the Holy Father {Pope} a report on the state of the diocese entrusted to him, in the form and at the time determined by the Apostolic See.

Vilevile Can. 400(1) inasema hivi:

Unless the Holy Father (Pope) has decided otherwise, in the year in which he is bound to submit the report to the Supreme Pontiff, the diocesan Bishop is to go to Rome to venerate the tombs of the Blessed Apostles Peter and Paul, and to present himself to the Pope.


Ya pili ndiyo ya msingi kwa ufafanuzi. Ingekuwa hii ni forum ya wakatoliki watupu wala ile ya kwanza nisingeiweka, maana ya pili inatosha kueleza ninachotaka. Hata kama hutazisoma word to word basi soma walau ile part niliyo-bold kwa red.

Unapoisoma hasa hiyo red, utagundua kwamba kumbe kila askofu wa jimbo lolote duniani analazimika kila baada ya miaka mitano aende Roma kuhiji walipofia Mitume Petro na Paul na kuonana na Papa. Ile report huwa tunaiita Quinquennial Report na ile ziara ya kuhiji tunaiita Ad-Limina.

Lakini kumbuka sasa hivi Kanisa Katoliki lina maaskofu zaidi ya 5000 duniani. Kurahisisha utaratibu, Baraza la Maaskofu (Bishop Conference) la nchi au eneo fulani wanaji-organise na kufanya safari ya pamoja na kwenda Roma.

Maaskofu wa majimbo ya Tanzania wako 34 {exclude Kilani(Bukoba) and Eusebius(Dar)}. Hivyo, kila kitu tangu itinerary hupangwa na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na wote huondoka siku moja, ikibidi na ndege moja hadi Roma.

Kiongozi wa msafara huo wa maaskofu huwa ni Rais wa Baraza la Maaskofu wa wakati huo. Wanapofika Roma kila mmoja anafanya kama alivyotakiwa na zile Canon mbili. Kulingana na wingi, Vatican huchukua muda hata wiki nzima kushughulika na maaskofu wa nchi moja. Tanzania inao 34.

Sasa tuje anavyohusika Profesa Mahalu aliyekuwa Balozi Italy na maaskofu hawa.

Tuliopata nafasi ya kusafiri nje ya Tanzania nadhani mnajua unavyofurahi kukutana na mtanzania yeyote mkiwa huko nje. Binafsi nifikapo nje, walau nafika ubalozini mradi kuwasalimia tu kama nchi hiyo kuna ubalozi wetu. ni kawaida ya wengi.

Binafsi nimekuwa nikipokelewa vizuri ubalozini na kwa masaa machache tunapoongea wanafurahi na wakati mwingine wanaweza kukupa visenti au vimizigo vichache visivyozidi flight limit, kuwatumia ndugu zao wazipokee utakapofika JNIA.

Hivyo, maaskofu nao, kama watu wengine, wanapofika Rome na shughuli ya pale Vatican inapoisha, hawafungwi kusalimia watanzania wenzao wanaoishi Rome na jirani ya Italy.

Wakati wa Ubalozi wa Prof. Mahalu nchini Italy, Rais wa TEC wakati huo alikuwa ni Askofu Severine NiweMugizi wa Rulenge-Ngara akiongoza msafara wa maaskofu wasiozidi 30.

Ingemshangaza kila anayeelewa kuwa kundi la maaskofu 30 wafike pale halafu wasikutane. Hata safari ijayo wakenda Ad-Limina, maaskofu watakutana tu na balozi mtanzania aliyepo pale bila kujali dini yake.

Kuwaumbua wasiojua history na kuleta hisia za udini, tunapaswa tuwakumbushe kwamba October 19, 1970, Rais Nyerere akiwa njiani kutoka New York (UN) akiwa na Thabiti Kombo, Abdularman Babu na Joseph Butiku walipita Roma (Vatican) wakamsalimia Pope Paul XVI.

Ukifungua kitabu cha Thabit Kombo kiitwacho Masimulizi ya Thabit Kombo (ISBN: 9976603290), ukurasa wa 186 kuna picha inaonyesha jinsi Pope Paul XVI alivyofurahishwa na ugeni huo hadi akampa Thabit Kombo zawadi ya sanamu ya Saint Joseph. Picha hiyo ndiyo nimeibandika hapo juu.

Hivyo, madai yale pimeni wenyewe yanaweza kutolewa na mtu wa akili ya aina gani.

Ziara hizo za maaskofu yaani Ad Limina, ni fursa moja ya balozi yeyote wa Italy kuwakaribisha maaskofu ubalozini na wala si Prf. Mahalu peke yake.

Zaidi ni kwamba wakati wa Mahalu kati ya February hadi March 2005, maaskofu wa Tanzania walifanya ziara maalumu kwa ajili ya kumsalimia Pope John Paul II ambaye alikuwa tayari mahututi. Hata hivyo maaskofu hao walichelewa kwani walipofika Vatican waliambiwa imefika kipindi Pope kwa hali yake haruhusiwi ovyo kuonana na watu na anatakiwa kutulia.

Pope alipoelezwa kwamba kuna maaskofu wa Tanzania wamefunga safari kwa ajili yake basi akaruhusu waje wawili tu ndipo akachaguliwa Severine NiweMugizi kwa sababu ndiye alikuwa kiongozi wao kama Rais wa TEC na mwingine akawa ni Polycarp Cardinal Pengo wa Dar.

Hivyo, hii ni wazi ni nafasi nyingine ya kuonana na watanzania walioko Italy na si Mahalu pekee. Mahalu asingeweza kuwa mjinga eti asiwapokee maaskofu kwake eti kwa sababu kuna wataalamu wa kuchonga tuhuma za udini.

Hiki ndicho ninachokielewa kuhusu safari za maaskofu jijini Rome. Lakini ikumbukwe kwamba, Rome ndiyo Jimbo Katoliki ambalo ni makao makuu ya Kiongozi wa kanisa hilo duniani. Hivyo, safari za maaskofu iwe mmojammoja au kundi kwenda huko siyo kitu cha mjadala.

In fact, mabalozi wa kitanzania walioko nje ya Africa, balozi wa Italy anaweza kuongoza kwa kukutana na watanzania wengi wanaowasili nchi aliyomo.

Kwa nini nasema hivi? Jiulize, Wilbroda Slaa hakufikia kuwa askofu. Lakini je Phd yake kaipatia wapi? Pengo, Kilaini, Nzigilwa, Salutaris ni maaskofu wachache waliopata Phd zao wakiwa Roma kama alivyopata Slaa.

Hii mana yake ni nini? Tunaoufahamu ukatoliki ni kwamba Rome ina Pontifial Universities nyingi ambazo mapadri wengi duniani wakiwemo watanzania husoma huko.

Kwa ujumla ukipewa kazi ya ubalozi nchini Italy basi ukae ukielewa kuwa hata kama wewe ni mpagani hilo lazima ulielewe, maana halikujengwa na watanzania, dunia nzima inalielewa hivyo, inaliheshimu hivyo.

Hivyo, basi asiyekubaliana na ukweli huo unaokubalika dunia nzima,afute kabisa dhana ya kulikaribisha hilo mawazoni mwake.
 
Wajina Paschal Matubi,

TYK!

Asante kwa mada hii,

Mimi ni mmoja wa Tanzania ambaye nimeushuhudia ukarimu wa Balozi Rick Coster Mahalu.

Nikiwa mjini Rome miaka hiyo, nilipata tatizo tatizo la "black out" nikiwa kwenye mkutano wa FAO, nikapelekwa hospital na ambulance na kuwa addmited. Baada kupatiwa huduma ya kwanza, wakaomba Medical Insurance yangu ili niendelee kutibiwa. Kiukweli sikuwa na bima! wakasema then lazima nidhaminiwe na ubalozi ndipo nipatiwe matibabu!. Kwa msaada wa ofisa ubalozi wetu Mr. Mchemwa, Balozi Mahalu, aliridhia mimi kupatiwa udhamini wa ubalozi na kutibiwa!. Ubalozi uli foot bill yote!.

Baada ya matibabu na kutoka hospitalini, nilipewa hifadhi ya kibinaadamu nyumbani kwa Nchemwa, nilikirimiwa vizuri sana na familia yake yenye mkewe na mabinti wake wawili!. Baada ya kustabilize, nilikwenda ubalozini kumshukuru, and very unfortunately kulitokea ajali ya stand ya kamera yangu kudondoka na kudondokea meza ya kioo ya ubalozini na kuivunja!, "What an embarassment", kusema ukweli niuona utu wa Balozi Mahalu, badala ya kukasirika ndio kwanza alinifariji na interview iliendelea!.

Hivi mimi ni mmoja wa wengi ambao tunasali na kuomba kikombe hicho alichotwishwa, kipite salama!. Ukitenda Wema, utalipwa mema, hivyo huu ni Wema niliotendewa mimi mtu mmoja tuu, jee Prof. Mahalu, kawatendea mema wengine wangapi ambao wote kwa pamoja wanamuombea kikombe hiki kimpitie mbali?.

God Bless Prof. Costa Rick Mahalu!.

God Bless Tanzania.

Pasco.
 
****** anatupeleka wapi jamani na udini huuuu!!!! Mbona kasha tuumiza Watanganyika maana sidhani kama tupo salama. Kwa nini hajifunzi kwa wenzake waliomtangulia? Jambo la udini ni baya mno! Ila laana ya CCM kuanzisha hoja ya udini hasa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu 2010 matunda yake ndo haya sasa. Mnaporomoka kiumaarufu utadhani ndani ya CCM hakuna think tanks, ivi kazi ya akina Dr Laurian Ndumbaro huko ikulu ni ipi? Siyo vizuri jamani viongozi kupandikiza udini. Kibaya zaidi religious sentiments has the propensity to grow and harm unselectively. Hebu Kikwete uwe mstaarabu kidogo we ni msomi usiwaumize watu kwa misingi hiyo bwana!
 
Wewe Mujahidina kutoka Pemba mambo ya Tanganyika yanakuhusu nini!!?? nyinyi endeleeni kuomboleza kifo cha Gaidi mwenzenu Sheikh Osama Bin Laden.

Eeh yamekuwa haya tena. Ngoja nisome mada nyingine hii niiweke kapuni. Kichefuchefu
 
Mkuu Pasco.

Nimeona juhudi zako za utetezi wa Prof C Mahalu tangu jana hata ingekuwa mimi pengine ningemtetea kutoka na ukarimu na ufadhili aliokutendea.Bahati mbaya Prof Mahalu hajawakarimu mamilioni ya waTanzania wanaotaabika na maisha magumu,umaskini,maradhi,ujinga na ufisadi.Prof Mahalu ameshiriki kutafuna fedha chache sana ambazo zingeweza kutumika kuokoa maisha ya kina Mama wajawazito au wagonjwa masikini wanaokosa tiba sahihi hapa Tanzania [wakubwa wanakimbizwa India].Prof Mahalu badala ya kutumia elimu yake kwa faida ya waTanzania wote katumia elimu yake kwa faida ya tumbo lake na washirika wake.

Mkuu Pasco wakati mwingine jaribu kuyatazama na kuyaheshimu maslahi ya nchi dhidi ya maslahi binafsi.

Mungu Ibariki Afrika Mungu Ibariki Tanzania.

Ngongo@Arusha City.




Wajina Paschal Matubi,

TYK!

Asante kwa mada hii,

Mimi ni mmoja wa Tanzania ambaye nimeushuhudia ukarimu wa Balozi Rick Coster Mahalu.

Nikiwa mjini Rome miaka hiyo, nilipata tatizo tatizo la "black out" nikiwa kwenye mkutano wa FAO, nikapelekwa hospital na ambulance na kuwa addmited. Baada kupatiwa huduma ya kwanza, wakaomba Medical Insurance yangu ili niendelee kutibiwa. Kiukweli siku nayo, wakasema then lazima nidhaminiwe na ubalozi ndipo nipatiwe matibabu!. Kwa msaada wa ofisa ubalozi wetu Mr. Mchemwa, Balozi Mahalu, aliridhia mimi kupatiwa udhamini wa ubalozi na kutibiwa!.

Baada ya matibabu na kutoka hospitalini, nilipewa hifadhi ya kibinaadamu nyumbani kwa Nchemwa, nilikirimiwa vizuri sana na familia yake yenye mkewe na mabinti wake wawili!. Baada ya kustabilize, nilikwenda ubalozini kumshukuru, and very unfortunately kulitokea ajali ya stand ya kamera yangu kudondoka na kudondokea meza ya kioo ya ubalozini na kuivunja!, "What an embarassment", kusema ukweli niuona utu wa Balozi Mahalu, badala ya kukasirika ndio kwanza alinifariji na interview iliendelea!.

Hivi mimi ni mmoja wa wengi ambao tunasali na kuomba kikombe hicho alichotwishwa, kipite salama!.

God Bless Prof. Costa Rick Mahalu!.

God Bless Tanzania.

Pasco.
 
Hivi mbona wengine wakiiba mnashika bango kihivo? kama ameiba ashitakiwe na kama sio basi AMTAJE NANI ALIIBA CHENJI ILE!
 
Mnataka kumtetea Mahalu kwa mgongo wa dini.

Huyo ni mwizi tu, hakuna zaidi.
 
Huenda na wewe ni Mpemba au miongoni mwa Magaidi,

Dah, we kweli masikini wa mawazo! Hili ni jibu la mwisho, uki-'reply with quote' nakuchunia. Watu kama nyinyi hamfai, mnapandikiza chuki katika taifa letu ambalo limeshaelemewa na ufisadi. Tena wewe unaongeza ubaguzi wa sijui wa Pemba sijui wa Tanganika?!, wewe ni wa kuogopewa. period
 
Hili la ukarimu na mzigo wa udini anaobebeshwa Mahalu siungi mkono kwa dhamira ya kweli kwa nchi yangu. Ama hili la wizi kwangu bado kizungumkuti.

Ni ukweli kwamba kulikuwa na mikataba miwili ya mauziano, kwa maoni yangu "Mmoja kwa ajili ya manunuzi mwingine kukwepa kodi", na Ukisikiliza maelezo ya Mkapa mahakamani ni kama aliogopa kwenda in details kuelezea kwa hofu ya kuonekana kwamba serikali ilikwepa kodi.

Mawazo mengine: Je, baada ya mahalu kufanikisha ukwepaji kodi lile salio alibaki nalo au lilirudi serikalini?
 
Back
Top Bottom