Prof. Mahalu amtuhumu Kikwete kumfungulia kesi ya ufisadi kwa uonevu kwa unyemela aliosimamia mwenyewe akiwa waziri Mambo ya Nchi za Nje

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,774
Prof. Mahalu amemtuhumu Kikwete kwamba akiwa Rais alimfungulia kesi ya ufisadi kiuonevu, wakati yeye mwenyewe Kikwete ndiye aliyesimamia uuzaji wa nyumba ya Tanzania kinyemela huko Italy akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Prof. Mahalu amedai kwamba kwa kuwa Mkapa alijua ukweli wa jambo hili na kwamba Kikwete alikuwa akimuonea Prof. Mahalu na kumfanya scapegoat, alimamua kwenda Mahakamani kumtetea kama shahidi na hii ndio ilisababisha Prof. Mahalu kushinda kesi.

1584350036958.png

Hii naonyesha wazi basi jinsi baadhi ya viongozi wetu walivyo na sura mbili. Kwa lugha ya mtaani anachosema Prof. Mahalu ni kwamba Kikwete akiwa Raisi alimbambikia kesi ya uhujumu uchumi, huku akijua wazi kwamba Prof. Mahalu hakuwa na kosa na kwamba Kikwete mwenyewe alihusika katika uuzaji wa hiyo nyumba, kitu ambacho kilimuuma sana Mkapa hadi akaamua kwenda Mahakamani kuwa shahidi wa Prof. Mahalu katika kumteteta.

Chanzo: Mwananchi

MAHOJIANO MAALUMU: Profesa Mahalu aeleza siri ya urafiki na Mkapa
 
Hii mbn watu walijuaa na bila mkapa kwenda kupigilia Misumari wa mwisho prof angeenda kunyolewa

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee wa Msoga alikuwa mtoto wa mjini sana kwa kuingiza watu mjini. Anakukata msumeno huku anacheka na wewe unaamini kukatwa msumeno hakuna maumivu. Naona pia Mzee wa Msoga aliwakamia sana Ma-professor.

Ukitaka kujua mtu alivyoingizwa mjini na Mzee wa Msoga muulize Prof. Mwandosya! Anamwahidi Prof. Mwandosya kuwa wewe ndiye utakuwa raisi awamu ya tano hivyo chapa kazi kunisaidia ujipe uzoefu wa kuwa raisi baada ya mimi huku majina ya wagombea anaowataka ameficha mfukoni! Prof. Mwandosya na umakini wake wote ule akamwamini!
 
Kweli kabisa....
Hata wakina ruge wakitka kutusua kesi yao wamuite yeye pia mzee Wa msoga awe kama shahidi! Kesi itaisha

Ova
Mzee wa Msoga alikuwa mtoto wa mjini sana kwa kuingiza watu mjini. Anakukata msumeno huku anacheka na wewe unaamini kukatwa msumeno hakuna maumivu. Naona pia Mzee wa Msoga aliwakamia sana Ma-professor.

Ukitaka kujua mtu alivyoingizwa mjini na Mzee wa Msoga muulize Prof. Mwandosya! Anamwahidi Prof. Mwandosya kuwa wewe ndiye utakuwa raisi awamu ya tano hivyo chapa kazi kunisaidia ujipe uzoefu wa kuwa raisi baada ya mimi huku majina ya wagombea anaowataka ameficha mfukoni! Prof. Mwandosya na umakini wake wote ule akamwamini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasubiri story ya Lugola ya mkataba fake kwa hamu siku Magufuli akimaliza miaka yake kumi! I believe kuna story nzuri sana nyuma ya pazia!
Kila utawala unakuwaga na kukombatia watu wake Yaani mupe muruke.....
Lugola Ana defence ila angekuwa mwingine hapo Sahv yupo nyuma ya nondo
Tz bado tunalindana sana

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni vyema tu Prof Mahalu angekaa kimya milele.. Ushahidi wote ulikuwa unamtia hatiani. Ila kwa sababu shahidi wa mwisho aliyekuwa mtu mzito ambaye maneno yake yanatakiwa yachukuliwe kwa uzito wa juu alisimama na kutia neno, hakukua na namna tungeweza kusema anaidanganya mahakama hivyo ndivyo mahalu aliponea chupu chupu.
 
Prof. Mahalu amemtuhumu Kikwete kwamba akiwa Rais alimfungulia kesi ya ufisadi kiuonevu, wakati yeye mwenyewe Kikwete ndiye aliyesimamia uuzaji wa nyumba ya Tanzania kinyemela huko Italy akiwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.

Prof. Mahalu amedai kwamba kwa kuwa Mkapa alijua ukweli wa jambo hili na kwamba Kikwete alikuwa akimuonea Prof. Mahalu na kumfanya scapegoat, alimamua kwenda Mahakamani kumtetea kama shahidi na hii ndio ilisababisha Prof. Mahalu kushinda kesi.

View attachment 1389781

Hii naonyesha wazi basi jinsi baadhi ya viongozi wetu walivyo na sura mbili. Kwa lugha ya mtaani anachosema Prof. Mahalu ni kwamba Kikwete akiwa Raisi alimbambikia kesi ya uhujumu uchumi, huku akijua wazi kwamba Prof. Mahalu hakuwa na kosa na kwamba Kikwete mwenyewe alihusika katika uuzaji wa hiyo nyumba, kitu ambacho kilimuuma sana Mkapa hadi akaamua kwenda Mahakamani kuwa shahidi wa Prof. Mahalu katika kumteteta.

Chanzo: Mwananchi

MAHOJIANO MAALUMU: Profesa Mahalu aeleza siri ya urafiki na Mkapa
Dah profesa alikuwa anamgonga yule mama pale ubalozini Roma sijui ndio kilimuuma mkwere

Gt mrangi ongezea nyama hapa
 
Back
Top Bottom