Prof. Maghembe: Marufuku kusafirisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda nyingine kuanzia Julai

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe ametangaza mabadiliko muhimu katika biashara ya mkaa nchini na kusema kuwa kuanzia mwezi Julai mwaka huu hakuna mkaa wowote utakaosafirishwa kutoka wilaya moja kwenda nyingine ili kunusuru misitu inayoteketea kwa kasi hapa nchini.

Amesema hayo leo wakati akifungua mkutano wa 24 wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Maliasili na Utalii uliofanyika katika ukumbi wa LAPF mjini Dodoma na kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali kutoka kwenye Idara, Vitengo na Taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara hiyo.

“Kuanzia mwezi Julai hakuna ruhusa ya kutoa vibali vya kuhamisha mkaa kutoka wilaya moja kwenda wilaya nyingine, mkaa utachomwa, utauzwa ndani ya wilaya kwa ajili ya matumizi ya watanzania wanaohitaji nishati ya mkaa, lakini biashara ya mkaa ya kutoa Dodoma kwenda Dar es Salaam mpaka Zanzibar marufuku.

“Wamekata misitu yetu yote, mito yetu imekauka, tunashindwa kupata maji ya umwagiliaji kwasababu watu wengi huko nje wanataka mkaa wetu, Tanzania jamani sio shamba la bibi, wale wote watakaotoa mkaa kutoka eneo moja hadi jingine kinyume na sheria hii watashuulikiwa kwa utaratibu wa uhujumu uchumi”, amesema Maghembe.

Amesema kuwa kwa upande wa miji mikubwa kama Dar es Salaam, Dodoma, Morogoro na Tanga vitaanzishwa viwanda maalumu vya kuzalisha mkaa ambao utauzwa kwa vibali maalumu katika mikoa mbalimbali hapa nchini. Amesema mkaa huo hautakuwa na athari nyingi za kimazingira kwa sababu utazingatia taratibu za uzalishaji endelevu.

Wakati huo huo, Waziri Maghembe amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kumuhamisha kituo cha kazi Mkuu wa Kikosi cha Kufuatilia na Kuzuia Uharibifu wa Misitu wa Wakala hiyo, Arjason Mloge kutoka Makao Makuu ya Taasisi hiyo kwenda chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) kilichopo mkoani Kilimanjaro na badala yake atafutwe mtu mwingine muaminifu.

Amesema uamuzi huo ni kufuatia udhaifu uliojitokeza katika usafirishaji wa rasilimali za misitu ndani na nje ya nchi ikiwemo usafirishaji kwa kutumia nakala za vibali ambazo sio halisi, yaani “Photocopies”. “Agizo hili litekelezwe mara moja kabla ya saa sita mchana wa leo na niwe nimepewa nakala ya barua hiyo ya uhamisho” amesema.

Kufuatia uamuzi huo amepiga marufuku kuanzia leo usafirishaji wa mazao ya misitu ndani na nje ya nchi kwa kutumia nakala zisizo halisi(Photocopies). Ameongeza kuwa katika kuunga mkono Sera ya Uchumi wa Viwanda ya Serikali ya awamu ya tano hakuna gogo litakalosafirishwa kwenda nje ya nchi.

“Wawekezaji wanahimizwa kujenga viwanda vya kuchakata magogo hayo hapa nchini ili kutoa ajira kwa Watanzania pamoja na kutoa faida halisi inayotokana na rasilimali hizo kwenye uchumi wa taifa”, amesema.

Akizungumzia changamoto ya mifugo kwenye maeneo ya hifadhi nchini amesema Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 sehemu ya 21 (1) hairuhusiwi kabisha kuchunga mifugo katika Hifadhi za Taifa, Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu na Hifadhi za Misitu. Amewataka watumishi wa Maliasili kusimamia Sheria hiyo pamoja na kutoa wito kwa wananchi kuifuata kikamilifu.

Katika hatua nyingine, Waziri Maghembe amewataka majangili wote nchini kuachana na biashara hiyo haramu ambayo hailipi kwa sasa na badala yake wachukue matrekta wakalime.

“Mtu ambaye alikuwa anaishi kwa kutegemea ujangili sasa atafute trekta akalime, kwa sababu akifanya ujangili tukamkamata tu, na tukimkamata atakaa kwenye hoteli ya mkuu wa magereza (magereza) kwa zaidi ya miaka 25”.

Aidha, Waziri Maghembe ametoa pongezi kwa watumishi wote wa Wizara ya Maliasili kwa kazi nzuri wanayofanya ya kupambana na ujangili nchini pamoja na ulinzi wa maliasili za taifa (Misitu, Wanyamapori na Mambo ya Kale) ambazo kwa pamoja zinachangia asilimia 20.5 kwenye pato la taifa. Amesema matokeo chanya ya kupambana na ujangili yameanza kuonekana japo ujangili bado upo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Aloyce Nzuki amemueleza Waziri Maghembe kuwa maelekezo yote aliyoyatoa yamepokelewa kwa ajili ya kuyafanyiwa kazi, huku Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexandre Songorwa akimueleza Waziri huyo kuwa watalinda na kusimamia Malisili za Taifa na kwamba katu hawapo tayari kuandikwa kwenye vitabu kuwa walishiriki katika kutoweka kwa maliasili hizo.

Chanzo: PROF. MAGHEMBE ASEMA ZUIO LA KUSAFIRISHA MKAA KUTOKA WILAYA MOJA KWENDA NYINGINE KUANZA MWEZI JULAI | Ministry of Natural Resources and Tourism
 

Attachments

  • IMG-20170418-WA0045.jpg
    IMG-20170418-WA0045.jpg
    66.3 KB · Views: 160
Politics in action
Kila nikitafakari juu ya utekelezaji wa agizo hili naona giza tu. Kimsingi nakubaliana kabisa na katazo hili lakini nadhani kuna kitu kilitakiwa kuanza kabla ya katazo.
Naangalia iwapo kuna uwekezaji wa kutosha hata kwenye mitungi ya Gesi, upatikanaji ukoje? Mafuta ya taa ni muafaka katika matumizi ya kupikia na kupasha joto wakati wa baridi kali hususani kwenye maeneo yenye baridi kali?
Katazo hili utadhani LA mwakyembe na ndoa bila cheti cha kuzaliwa.
 
Jana nimerudi na mtungi wangu kichwani, nimaeondoka kwa biti nyumbani naenda kujaza gesi nafika kumbe bei imepanda bwana, basi nikazugazuga pale nikapitia kibanda cha mkaa nikachukua wa 15000, nikachukua jiko la mkaa bovu lililotupwa na jirani, nikaliongezea maudongo, limetengenezeka, ndo hilo nalitumia sasa,

Nimeshaiona fursa hapa naandaa tangazo la fundi majiko ya mkaa, naona sekta hii imekosa mafundi kabisa
 
Aiseee,

Huyu atakuwa hakula Kwa sababu mkaa ulizingua home kwake siku ya Pasaka, alipouliza kaambiwa mkaa ulizingua.

Baasiiii, tamko ameona akataze mkaa kusafirishwa.

Japo, katika hili, naona nchi nzima magari ya serikali ndiyo yanaongoza kupitisha mkaa haswa STJ, STK, SU, PT, SM n.k.
 
Sasa huku Dar ambapo hakuna miti watu watapikia nini?

Ila wakitaka inawezekana, kama viroba waliweza hili hawawezi lishindwa kamwe
 
Ukisitaajabu ya Musa utayaona ya Filaaun kwa Tanzania hawezi kupika kwa kutumia umeme gass yenyewe bei iko juu, anatafutia maasikali na watu wamaliasili ulaji, ata ukiwa na gunia 2 kwenye gari wanataka rushwa ukikataa wanakunyanganya huwo mkaa
 
Wamechelewas sana kwa hili nawaunga mikono na miguu yote nakumbuka miaka ya 1975 tulikuwa tunaishi palikuwa na mistu mikubwa lakini leo hii ni jangwa hapatamaniki kabisa tena wazuie kabisa mkaa usiingie mjini ubaki huko huko kijini mjini tukomae na gesi ingawa ni bei juu lakini tuokoe misitu yetu inayoangamia kwa kasi anayeona gesi bei juu hama mjini mimi huwa naumia sana nikikumbuka misitu ilivyokuwa zamani leo hii pamekuwa majangwa na ukame
 
Back
Top Bottom