Prof. Maghembe kuanzisha kampeni ya upandaji miti

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Wizara ya Maliasili na Utalii, Tamisemi na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano inategemea kuanzisha programu ya pamoja wa upandaji miti nchini kwa ajili ya uhifadhi na undelezaji wa mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja uliwakutanisha Mawaziri wa Wizara ya Maliasili, Utalii na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na
Muungano na jopo la wataalamu, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amesema Serikali ya awamu ya tano imekusudia kuboresha uhifadhi wamazingira.

Prof. Maghembe. Ameongeza kuwa Wizara ina maeneo makubwa yaliyotengwa kwa ajili ya kupanda miti ili kuzuia uharibifu
wa Mazingira ikiwa ni pamoja na kuzuia ukataji miti hali inayotishia nchi kuwa jangwa kama hatua stahiki hazitachukuliwa mapema.

‘’Tupo tayari tumejiandaa na tunaweza ikiwa nia yetu ni kuhakikisha nchi nzima inapandwa miti kwa wingi na kwa
usimamizi wa hali ya juu kwa kuwashirikisha wananchi’’ Prof. Maghembe alisisitiza.

Mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba ulikuwa na lengo
la kuipa kazi kamati maalum kwa ajili ya kuandaa andiko maalum litakalotumika kuandaa mpango mkakati huo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Mhe. January Makamba Kamati hiyo imepewa wiki mbili kuhakikisha inakamilisha kazi hiyo ambapo utekelezaji wake unategemewa kuanza mara moja ukiwa na mbinu mpya zaidi.
 
Ni jambo jema ila huku mbugani ambako watu hata maji ya chakula hawana sijui watatumia mbinu gani
 
mhe. magembe, zoezi la kupanda miti ni jambo jema. lakini wizara yako ni jipu, kwani inazungumziwa sana kama ilivyo kwa bandari. idara zifuatazo inasemekana ni majipu: tanapa, kinapa, wanyama pori, ngorongoro conservation, bodi zote, misitu na pale penye tozo toka kwa watalii. je, umejiridhisha kuwa sehemu zote hizi kazi inafanyika kwa uadilifu na serikali inapata kilicho chake? je,yanayoongelewa ni uzushi tu au yana ukweli? wakujibu ni wewe. bandari ilisemekana na ikajadhihirika ni kweli.
baadhi ya wafanyakazi katika wizara yako wananuka pesa na baadhi dollar. kupata kazi katika baadhi ya idara ni shughuli pevu.
wewe si waziri mzigo? prove it.
 
Back
Top Bottom