Prof. Maghembe anazidi kuchemka!!!

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Wasambazaji sukari wambana Maghembe WASAMBAZAJI wakubwa wa sukari kutoka Kiwanda cha TPC mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kutazama upya agizo lake la kuzifutia leseni kampuni hizo kwani hazihusiki na tuhuma zilizotolewa dhidi yao. Katika tamko lao la pamoja lililotolewa na wakurugenzi wa Kampuni za Setway Investment Ltd, Marenga Investment Ltd na Mohamed Enterprises Ltd, wamesema hawajawahi kukamatwa au kuonywa kuhusu usafirishwaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi. Walisema, hakuna magari yao yaliyokamatwa na shehena ya sukari ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi, lakini pia wakaiomba Serikali kutoa uthibitisho usio na shaka juu ya uhusika wao katika madai hayo. "Katika agizo lake, Mheshimiwa Waziri Maghembe amesema amekwenda nchini Kenya zaidi ya mara tatu na kukuta sukari ya Tanzania, lakini hakueleza kama wamekamata malori mangapi ya kampuni zetu au jinsi ambavyo tumeiuza sukari hiyo nchini humo. Tunaomba haki itendeke," walieleza katika taarifa hiyo ambayo gazeti hili ina nakala yake. Ilisema kampuni zao zinajihusisha na usambaza wa sukari ndani ya nchi pekee na kwamba hata hivyo kabla ya agizo la Serikali, hawajawahi kuitwa ili kujadiliana na kufahamu tatizo lao ili nao waeleze mikakati yao ya kuhakikisha sukari haivushwi kwenda nje ya nchi. Walisema pamoja na upungufu wa sukari katika soko likiwemo la dunia, lakini mawakala hao walikutana na Mkuu wa Mkoa na walijiwekea mikakati ya kuwadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu na kuwapa utaratibu wa kununua na kuuza kwa kiwango maalumu. Walisema wanathibitisha hawakukiuka masharti ya mikataba kati yao na TPC na hivyo hatua iliyochukuliwa siyo sahihi na haikuzingatia haja na haki ya kusikiliza pande zote. "Tumekuwa tukiuza sukari kwa kutumia vitabu vya risiti na tunatoa taarifa kwa ofisa biashara, katika vitabu vyetu vya risiti hakuna kampuni ya Kenya au nchi nyingine tuliyowauzia sukari, iweje sisi ndiyo tuonekane tunauza nje?," Walihoji. "Tunauza sukari kwa wakala wetu na tunafanya hivyo kwa uaminifu mkubwa, tungeonekana wakosaji kama wakala hao wasingepata sukari kutoka kwetu, suala la sukari kuuzwa nje ya nchi, makampuni yetu yasibebeshwe mzigo huo." Ilisema suala la bidhaa hiyo kukutwa nje ya nchi lisisababishe kampuni zao kubebeshwa mzigo usiowahusu kwani jukumu la kudhibiti mipaka ili sukari isiuzwe nje ya nchi ni kazi ya vyombo vya Dola ambalo wao hawana uwezo nalo. "Tunadhani Waziri amekiuka misingi ya kisheria, kutolea maamuzi jambo linalohusu mikataba kati ya pande ambazo yeye siyo mmojawapo. Tunaomba Serikali ifikirie upya kwani uwakala unaozungumziwa upo kisheria," zilieleza kampuni hizo katika taarifa yao. Kuhusu sukari kuuzwa kwa bei ya kati ya Sh 2,000 hadi 2,500 kwa kilo moja kwa watumiaji wa nyumbani, kampuni hizo zimesema hazihusiki kwa namna yoyote kwani hawauzi rejareja na mawakala wanaouwauzia wanauza kwa bei iliyokupangwa na siyo vinginevyo. Juzi, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe alitangaza kufutwa rasmi kwa leseni za wasambazaji wakubwa wa sukari kutoka kiwanda cha sukari TPC mkoni hapa kwa madai wanahusika kuuza sukari hiyo Kenya kinyume cha maagizo ya Serikali. "Kutokana na uchunguzi wa Serikali, tumebaini kampuni hizo ndizo zinazosababisha upungufu uliopo sokoni kwa sasa na usafirishwaji wa sukari nje ya nchi jambo ambalo ni kinyume na maagizo ya Serikali," alisema. Kutokana na agizo hilo, Waziri Maghembe alisema Serikali imeiteua Kampuni ya Modern Holdings (EAC) Ltd na Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU) kusambaza sukari hiyo mkoani hapa, kazi ambayo ilikuwa ikifanywa na kampuni zilizofutiwa leseni.

Source:http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=21681

My take:

Wakati tunaipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kusimamia kwa dhati uvushaji holela sukari nje ya nchi kwa lengo la kuwasaidia watanzania, kwa upande fulani bado inaonekana Serikali haijajidhatiti kwenye hili hasa kutokana na kutumia watendaji wenye kukurupuka na wasio makini.

Mhe. Maghembe ni Profesa na msomi mzuri sana lakini kwa ujumla, ukifuatilia historia ya matukio ya Mhe. Maghembe tokea awe Waziri kwenye Serikali ya JK, utendaji wake umekuwa ukita mashaka makubwa hasa kwa kufikia maamuzi mengi ambayo hayatekelezeki kabisa na kumwanika kama mbabaishaji. Maghembe
alishindwa kumudu mambo alipokuwa Wizara ya Elimu ya Juu, Mhe. JK sijui alifikiri nini kumpeleka huyu Prof. Wizara nyeti kama Kilimo ambapon tokea ainge inaonekana kama hakuna lolote lenye tija alilolifanya.

Ikiwa hakuwa na ushahidi wa kuyahusisha makampuni hayo ya usambazaji sukari na matukio ya kuvusha nje sukari, aliwezaje kutamka hadharani kuwa "anayafuta leseni??".

Maswali ya kujiuliza hapa ni Je, yeye kama Waziri ndiye anayehusika na utoaji wa lesni kwa makampuni yanayosambaza sukari au zipo mamlaka nyingine kama vile Bodi ya Sukari, Maafisa Biashara (Wizara ya Viwanda na Biashara) au Halmasahuri za Wilaya??. imekuwaje atoe amri ambayo pia inaingilia mahusiano ya kimakataba kati ya wasambazaji hao na viwanda vinavyozalisha suakri wakati huo huo kuteua kampuni mpya ambayo hakueleza ni vigezo gani alitumia kuziteua kampuni hizo mpya kama si maslahi binafsi?? .

Je, amewezaje kuchukua maamuzi kama haya ambayo yanaweza kuligharimu taifa iwapo iwapo makampuni aliyoyafutia leseni yataamua kuishitaki serikali, yeye hakuthubutu hata kutaja sheria ambayo aliizingatia kutoa tamko la kuyafutia leseni makampuni hayo lakini alisema tu nimeyafutia (Je, hizo leseni alizitoa kwa vigezo vipi kiasi cha kuamua kuzifuta mbele ya waandishi wa habari?/) . Alipata wapi uthubutu wa kuwaita waandishi wa habari na kutangaza amefuta leseni bila kuwa na ushahidi wala sheria. Haya ni yale yale ya Katibu Mkuu Kiongozi ya kurejesha Ofisini Jairo wakati yeye si mamlaka ya Uteuzi wala ya Nidhamu ya Makatibu wakuu!!!. ..
 
Wasambazaji sukari wambana Maghembe

WASAMBAZAJI wakubwa wa sukari kutoka Kiwanda cha TPC mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kutazama upya agizo lake la kuzifutia leseni kampuni hizo kwani hazihusiki na tuhuma zilizotolewa dhidi yao. Katika tamko lao la pamoja lililotolewa na wakurugenzi wa Kampuni za Setway Investment Ltd, Marenga Investment Ltd na Mohamed Enterprises Ltd, wamesema hawajawahi kukamatwa au kuonywa kuhusu usafirishwaji wa bidhaa hiyo nje ya nchi. Walisema, hakuna magari yao yaliyokamatwa na shehena ya sukari ambayo ilikuwa ikisafirishwa kwenda nje ya nchi, lakini pia wakaiomba Serikali kutoa uthibitisho usio na shaka juu ya uhusika wao katika madai hayo. "Katika agizo lake, Mheshimiwa Waziri Maghembe amesema amekwenda nchini Kenya zaidi ya mara tatu na kukuta sukari ya Tanzania, lakini hakueleza kama wamekamata malori mangapi ya kampuni zetu au jinsi ambavyo tumeiuza sukari hiyo nchini humo. Tunaomba haki itendeke," walieleza katika taarifa hiyo ambayo gazeti hili ina nakala yake. Ilisema kampuni zao zinajihusisha na usambaza wa sukari ndani ya nchi pekee na kwamba hata hivyo kabla ya agizo la Serikali, hawajawahi kuitwa ili kujadiliana na kufahamu tatizo lao ili nao waeleze mikakati yao ya kuhakikisha sukari haivushwi kwenda nje ya nchi. Walisema pamoja na upungufu wa sukari katika soko likiwemo la dunia, lakini mawakala hao walikutana na Mkuu wa Mkoa na walijiwekea mikakati ya kuwadhibiti wafanyabiashara wasio waaminifu na kuwapa utaratibu wa kununua na kuuza kwa kiwango maalumu. Walisema wanathibitisha hawakukiuka masharti ya mikataba kati yao na TPC na hivyo hatua iliyochukuliwa siyo sahihi na haikuzingatia haja na haki ya kusikiliza pande zote. "Tumekuwa tukiuza sukari kwa kutumia vitabu vya risiti na tunatoa taarifa kwa ofisa biashara, katika vitabu vyetu vya risiti hakuna kampuni ya Kenya au nchi nyingine tuliyowauzia sukari, iweje sisi ndiyo tuonekane tunauza nje?," Walihoji. "Tunauza sukari kwa wakala wetu na tunafanya hivyo kwa uaminifu mkubwa, tungeonekana wakosaji kama wakala hao wasingepata sukari kutoka kwetu, suala la sukari kuuzwa nje ya nchi, makampuni yetu yasibebeshwe mzigo huo." Ilisema suala la bidhaa hiyo kukutwa nje ya nchi lisisababishe kampuni zao kubebeshwa mzigo usiowahusu kwani jukumu la kudhibiti mipaka ili sukari isiuzwe nje ya nchi ni kazi ya vyombo vya Dola ambalo wao hawana uwezo nalo. "Tunadhani Waziri amekiuka misingi ya kisheria, kutolea maamuzi jambo linalohusu mikataba kati ya pande ambazo yeye siyo mmojawapo. Tunaomba Serikali ifikirie upya kwani uwakala unaozungumziwa upo kisheria," zilieleza kampuni hizo katika taarifa yao. Kuhusu sukari kuuzwa kwa bei ya kati ya Sh 2,000 hadi 2,500 kwa kilo moja kwa watumiaji wa nyumbani, kampuni hizo zimesema hazihusiki kwa namna yoyote kwani hawauzi rejareja na mawakala wanaouwauzia wanauza kwa bei iliyokupangwa na siyo vinginevyo. Juzi, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Profesa Jumanne Maghembe alitangaza kufutwa rasmi kwa leseni za wasambazaji wakubwa wa sukari kutoka kiwanda cha sukari TPC mkoni hapa kwa madai wanahusika kuuza sukari hiyo Kenya kinyume cha maagizo ya Serikali. "Kutokana na uchunguzi wa Serikali, tumebaini kampuni hizo ndizo zinazosababisha upungufu uliopo sokoni kwa sasa na usafirishwaji wa sukari nje ya nchi jambo ambalo ni kinyume na maagizo ya Serikali," alisema. Kutokana na agizo hilo, Waziri Maghembe alisema Serikali imeiteua Kampuni ya Modern Holdings (EAC) Ltd na Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro (KNCU) kusambaza sukari hiyo mkoani hapa, kazi ambayo ilikuwa ikifanywa na kampuni zilizofutiwa leseni.

Back
Top Bottom