Ngushi
JF-Expert Member
- Jul 8, 2016
- 9,066
- 18,348
Katika siku zote leo ndio nimekuona kichwa! hongera sana mkuuWadau, amani iwe kwenu.
Binafsi nilikuwa ni miongoni mwa watu ambao tulionesha wasiwasi wetu mara tu baada ya Prof Maghembe kuteuliwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii. Wasiwasi wangu haukutokana na location ambayo Prof Maghembe anatoka bali ni kutokana na ugumu wa Wizara hiyo na uwezo wa Maghembe kukabiliana na changamoto za Wizara.
Hakika nilikuwa sahihi kumjudge negatively. Huko Kagera, Mhifadhi Mkuu wa Pori amefukuzwa kazi kutokana na kuwaondoa watu waliovamia pori hilo kwa kukata miti na kuingiza mifugo mingi. Mhifadhi huyo amefukuzwa kutokana na amri ya Mamlaka ya Juu ya Wizara.
Kama hiyo haitoshi, kuna operesheni inayoendelea ya kuwakamata vibompa wa Meno ya Tembo. Operesheni hiyo imeanza juzi. Hata hivyo, mamlaka ya Juu ya Wizara ya Maliasili na Utalii ikaingilia kati ili wanaohusika na biashara hiyo akiwemo jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Mpemba asikamatwe. Bahati nzuri Mheshimiwa Rais aliinyaka hiyo hewani na akasimama yeye mwenyewe kuongoza Operesheni hiyo. Hivi tunavyozungumza hali ni mbaya sana kwa hao jamaa ambao walidhani kuwa kwa nguvu ya pesa waliyonayo hawawezi kukamatwa.
Kwa mifano hii michache, sioni wapi ataponea Prof Maghembe. Jipu tayari limeiva na litatumbuliwa soon.
hata mimi nimeshangaa ile taarifa ya kuachiwa kwa mifugo bila masharti yoyote