Prof. Maghembe agombea kipaza sauti na kupelekea kuzomewa na wapiga kura wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Maghembe agombea kipaza sauti na kupelekea kuzomewa na wapiga kura wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MTENGETI, Oct 30, 2012.

 1. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Wanabodi Heshima Mbele

  Inawezekana kwa haraka ukajua ni gossip lakini ni kweli bila chembe ya shaka.
  Jana tarehe 29/10/2012 Rais Jakaya Mrisho Kikwete alifanya ziara ya kuweka jiwe la Msingi la Bweni (ambalo kimsingi bweni hilo limekamilika) Katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dr. Asha Rose Migiro iliyopo Wilayani Mwanga
  Sakata lenyewe lipo hivi:-
  Pamoja na Rais kuchelewa kufika eneo la Mkutano saa 12.30 jioni akitokea same Baada ya Utambulisho Mkuu wa Wilaya ya Mwanga alimpa nafasi Mkuu wa Mkoa amkaribishe Rais ahutubie wananchi ndipo wakati Rais anajitayarisha kwenda kwenye kipaza Sauti Prof Maghembe akakurupuka na kuwahi jukwaani. Tukio hilo pamoja na kuacha watu na mshangao akiwemo Rais Mwenyewe Maghembe alikutana na dhahma ya kuzomewa na wananchi kwa kumwambia "huna maana waziri mzima wa maji jimbo halina maji. kwanza tumezoea sound zako mpishe mwenye nchi aongee." Ndipo kwa aibu akashuka na Rais akawashukuru UWT ambao ndio waliojenga majengo ya shule hiyo na kukabidhi serikalini baada ya kukosa mtaji wa kundeshea shule hiyo. Pia alimpongeza Mzee CD Msuya kwa michango na misaada katika Ujenzi wa Shule hiyo ambapo Bweni hilo lilipewa jina la Rhoda Msuya kama kumbukumbu ya Marehemu Mke wa Mzee Msuya ambaye ndie alietoa wazo la kuanzissha shule hiyo kabla umauti haujamkuta
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Prof aliona hakutakuwapo nafasi nyingine tena!!
   
 3. Khakha

  Khakha JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 2,983
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  nyerere,mwinyi na che mkapa wameshawahi kunyang'anywa mic na waziri kwenye mikutano ya hadhara waliokuwa wanaifanya enzi zao uongozini? tatizo ni UDHAIFU.

  urais umekuwa mwepesi sana siku hizi na mawaziri wote wa jk wanajiona kuwa they can manage it thats why wanafanya vituko km hivyo.
   
 4. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mtengeti ?
  Kwanini hawakufikilia kumpiga mawe huyo majembe agrrrrrrr ?
  Kuna mawaziri nawachukia huyu na naibu wake basi tu.
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Majitu mengine bana, labda alitaka kuanza kampeni za ubunge 2015 kwa wapiga kura wake.
   
 6. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Prof.alijua ni kampeni za uchaguzi 2010 zinaendelea, aibu yake.
   
 7. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Labda alitaka kumleta dhaifu jukwaani si unajua alivyo na lips za ukwel alitaka kuzitumia kuchangamsha watu wampokee kwa bashasha
   
 8. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,357
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Hah hah hah! Ciello unajua ku-notice! Mr Lips kweli he thought he was in campaign!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. k

  kinauche JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 7,682
  Likes Received: 838
  Trophy Points: 280
  Mtengeti, huu ni uongo wa dhahiri ambao haupaswi kuongelewa na mtu anayejiita great thinker. Kilichotokea ni kwamba protocali ilikosewa na ndipo mkuu wa mkoa akamwambia mkuu wa wilaya kuwa ni lazima mbunge aongee kabla ya Rais. Ndipo mbunge alipopewa kipaza sauti. Hapakuwepo na aliyezomea hata mmoja kwani alielezea programu nzima ya kupeleka maji kwenye jimbo na kisha akazungumzia uhaba wa walimu. Nadhani chuki binafsi zisiwe zinaletwa mahali kama hapa. Kwani yeye ni mjinga kiasi kwamba hajui kampeni bado. Ona aibu! Mambo haya yamefanyika hadharani. Ungeweza kusema hayo uliyoyaandika kama ulikuwa ni mkutano wa ndani. Shame on you!
   
 10. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Itifaki haikufuatwa ndio amnyang'anye maiki?
   
 11. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Mkuu kinauche! aibu na iwe juu yako mwenyewe ambaye unajaribu kutoa utetezi usio na kichwa wala miguu. Hivi mkuu wa Mkoa na Waziri nani Mkubwa anayepaswa kumkaribisha Rais?

  Kwa kifupi hili ni tukio la pili la Prof kuvuruga protocal kwa kukmbilia Mic hapa Mwanga Likishuhudiwa na Rais Kikwete aliwahi pia kumnyanganya mama vikck swai wakati wa kampeini 2010.

  wananchi waliozomea na sababu kubwa ni shida ya maji iliyokumba jimbo hasa mji wa mwanga ambapo jana ndo maji yalitoka rasmi kwenye mabomba baada ya adha ya karibu miezi miwili.

  Acha kufanya utetezi usiokuwa na mashiko. Haya kama hakuzomewa alikimbia nini leo alfajiri kwenda Dar na kumucha rais akirudi kukagua shule upya leo asubuhi?
   
 12. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,926
  Likes Received: 945
  Trophy Points: 280
  gamba gembe
   
 13. Jodeny

  Jodeny JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Acheni majungu
   
 14. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu, hata mimi nilishangaa kidogo - kunyaganyana mic kunakujaje - hivi Raisi anaweza akukurupuka na kuanza kuzungumza kwenye himaya ya Mbuge bila kufuata protocali!!!!

  Mimi naona kuna kitu hapa, kwa nini wanasifia sana michango ya Mh.Msuya as if Mh.Majembe hakuwahi ku-contribute chochote kwenye Wilaya yake!! Siasa za Upareni zimekaa vipi - Prof.Maghembe ni academician zaidi kuliko longologo iliyo jaa kwenye mambo ya SIASA, msimamishe anytime barabarani hata kama hakujuhi atasimama na kukusikiliza hana majivuno au kujisikia. Hulka yake hiyo ya kutotaka makuu ndio inawafanya wabaya wake kujaribu kumtupia madongo nk.
   
 15. j

  jumys5ya Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtengeti unachokiongea ni uzushi mtupi! anachokueleza kinauche ni kweli kabisa, hakukuwa na zomea unayoisema. Prof alishuka baada ya kuelezea vizuri kabisa sababu za maji kutokuwepo, pia na mikakati iliyopo,ukosefu wa walimu na tatizo la mradi wa umeme na ndiyo rais akaipigia mistari. Tatizo ulichopost ni siasa za Mwanga tu ambazo kila mtu anazijua
  Kuwa Great Thinker wa Ukweli bwana!
   
Loading...