Prof. Lipumba vs Dr. Slaa kuhusu kushuka kwa bei ya saruji n.k | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Lipumba vs Dr. Slaa kuhusu kushuka kwa bei ya saruji n.k

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mashayo, Oct 29, 2010.

 1. M

  Mashayo Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kiuchumi kushuka kwa bei za bidhaa mbalimbali kunawezekana, nadhani Lipumba akiwa kama mchumi analielewa hili vizuri sema tuu labda alipitiwa au alikuwa na maana ya tofauti au alikosa muda wa kulielezea kwa kinagaubaga pale alipohoji hoja ya Dr. Slaa kuhusu kushusha bei. Kiuchumi ni wazi kabisa kuwa serikali ina uwezo mkubwa wa kushusha au kushindikiza ushushaji wa bei za vitu nchini. Kama prof alisahau hili naomba ni mkumbushe baadhi ya concept kwenye uchumi ambazo zinaweza kumpa mwananchi nafuu kwenye bei. Baadhi ya topic hizo ni price discrimination(bei ndogo kwa watu wa kipato kidogo na kubwa kwa watu wa kipato kikubwa), government interventionist, subsidies (serikali inauweza kumlipia mwananchi asilimia fulani ya bei), Supply theories (ongezeko la makampuni ya watoa huduma hushusha bei ya huduma) etc. Hivyo hapa Prof. Lipumba kama alimaanisha alichosema basi alikosea kwani kiuchumi bei kushuka inawezekana.
   
 2. i

  ilboru1995 JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,331
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Wachina walisomea wapi uchumi wao? ifikie wakati sasa watanzania tuamke na tuelimike kuwa hakuna the so called a clear prescriptions ya dawa ya uchumi wa watanzania iliyowahi kutibu uchumi wetu.. kila kukicha WB na IMF huwa wanatuletea sera zao ambazo wanazi brand kuwa ndiyo suluhisho la uchumi wetu na huwa wanapata baraka zote kutoka kwa viongozi na wataalamu wetu kama akina prof... Watanzania tubadilike, tujitambue na zaidi ya yote maslahi ya watanzania yawe mbele...
   
 3. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 869
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Mi naona Prof hakutaka tu kusema live kama naye anamkubali Dr kwa aliyoainisha japo asema yeye ndo zaidi. Huyu angemuunga tu mkono hata kumpigia urais. Mi naona vyama vingine viko pale kwa ruzuku tu, better vinyimwe kama havioneshi uhai. Kwa sababu ukununua shamba na ukashindwa kuliendeleza, lazima utanyang'anywa. Bora nao wafanyiwe hivo. Hebu fikiri kuhusu akina rungwe, mziray ...., hakuna kitu, kelele tu
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Asante kwa somo la uchumi. Bila shaka Professor analijua hili lakini may be hakuelewa swali au alilijibu kisihasa.
   
 5. W

  We can JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 681
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tusividharau vyama vidogo. Huwezi kuwa mkubwa kabla hujawa mdogo. La sivyo ukubwa wako ni feki.
   
 6. c

  chamajani JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizi mbili hizi ngumu kidogo kufikia lengo kama anavyotaka Dr. Slaa, kwa sababu dhana ya ongezeko la makampuni ya watoa huduma ili kushusha bei ya huduma limefanyiwa kazi vizuri na watoa huduma siku hizi, kwa mfano, makampuni ya bdhaa nyeti "sensitive products" kama saruji huwa inakuwa owned na mtu mmoja, so ana-regulate production capacity na supply powers ili kupata faida nzuri zaidi (I do no huko Tz but hope to be ze same). Na kuhusu hii government intervetion kwa Tanzania ni ngumu kwa sababu umaskini wetu umefanya most of ze sensitive products kuwa sensitive products-So huenda kwa majority wa Tanzania, hata ukiwagawia saruji bure, hawatojenga badala yake wataziuza kwa wengine tu, na kama ita-identif key products na ku-apply dhana hizi-certainly kutakuwa na market failure kubwa na hatimaye hali kuwa mbaya zaidi-so let me agree both with higher marks to Lipumba followed by Slaa!
   
 7. hope 2

  hope 2 Senior Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 155
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila kitu kinawezekana, wakati makampuni ya mawasiliano yanaanza nani alijua kama itafika siku tuongee kwa dhumni au shiling moja?
  Hata ungewaambia watu kipindi hicho wangebisha sana, Mbona sasa wanaendesha makapuni vizuri kwa hicho kidogo wanachowatoza, mnataka kusema hawapati faida?

  Ninachowaambia ni kwamba Cement kuuzwa elfu tano mpaka saba inawezekana....
   
 8. T

  Tata JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Safi sana Mkombozi. Huu uchumi wa kimagharibi tunaoukariri bila kuuelewa wanaouita "classical economics" umeshindwa na ndio maana migogoro ya kiuchumi haiishi ulaya na marekani. Mimi nadhani kuna haja ya kujifunza uchumi wa wachina kwani umewasaidia kukuza uchumi kwa kasi ya ajabu hata wakati wamarekani na watu wa ulaya walipokuwa wakiweweseka na mbinyo wa kiuchumi.
   
 9. T

  Tata JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,729
  Likes Received: 645
  Trophy Points: 280
  Ndio maana inabidi tumpe kura Dr. Slaa tuone kama ataweza kushusha bei mpaka kiwango anachosema. Cement inatoka Pakistan mpaka Dar inalipiwa kodi zote za serikali na bado inauzwa kwa bei nafuu kuliko hii ya Twiga Cement. Mimi nadhani kuna kuna tatizo kubwa sana hapa ni wizi mtupu tu. Inaelekea tunalipia gharama kubwa sana za "inefficiencies" za viwanda vyetu vya hapa nchini.
   
 10. c

  chamajani JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mawasiliano is not a ginuine case kwenye issue hii, ndo maana hakuna hata mgombea mmoja aliyezungumzia hilo-Hata hivyo, pamoja na kudhani kuwa wanatoza rate ndogo, faida wanapata kwa sababu structure ya uanzishwaji na uendeshaji wa mawasiliano tofauti sana na bidhaa nyingine. Ili kuthibitisha hili, jiulize kwa nini price ya mawsiliano tz ni reciprocal na karibu price ya bidhaa zote-regardless dollar imeshuka, imepanda wao kila ukicha dk/shilingi, nusu shilingi an so on?
   
 11. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2014
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,041
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Old is.....
  Worth reading
   
Loading...