Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Uvunjifu na ukiukwaji wa Haki za Binadamu ni tatizo kubwa hapa Tanzania, Azory Gwanda alipotea hapa Kibiti hadi leo hajulikani alipo

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
PhotoGrid_1_20200910115911.jpg
UVUNJIFU NA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NI TATIZO KUBWA HAPA TANZANIA AZORY GWANDA ALIPOTEA HAPA KIBITI HADI LEO HAJULIKANI ALIPO"PROF.LIPUMBA KIBITI"

Uvunjifu na ukiukwaji wa Haki za binadamu ni tatizo kubwa nchini Tanzania.

Hakuna chombo huru chenye nguvu cha kusimamia haki za binadamu. Tume ya haki za binadamu haina nguvu za kuweza kupambana na wavunjaji wa haki za binadamu. Wengi wa hawa ni watendaji wakuu wa Serikali ambaowanalindwa na mfumo uliopo.

Mkinichagua kuwa Rais wa nchi hii nitasimamia ipasavyo haki za Binadamu.
 
Lipumba anaongea na watu ambao wakati A. Gwanda akipotea tayari eneo lao lilikuwa limepoteza viongozi wao wa serikali za mitaa kibao kwa kuuwawa na wengine kukimbia makazi yao. anaongelea katika eneo ambalo wananchi wanajua kulikuwa na vikundi vya kigaidi ambapo kama sio juhudi za jeshi la polisi kuwafurumisha na kukimbilia Msumbiji, sijui hali ingekuwaje.
 
Una akili timamu? Kwa hiyo kama viongozi wa serikali za mitaa waliuawa, ni halali Azory kupotea? Kwani ni Azory ndiye alikuwa anaua hao viongozi wa serikali za mitaa!!

Tuna watu ni wajinga kupindukia!!
 
Sent using Jamii Forums mobile app
Unapoongelea mtu mmoja hali ya kuwa kuna watu kibao wamepotea na kupoteza maisha yao kwa tukio hilohilo ni upunguwani zaidi ya kukosa akili timamu. Mwenye akili timamu ataenda mbali zaidi ya hapo, angeorodhesha majina ya watu waliouwawa na atwambie kama Magaidi wanajua hizo haki za binadamu
 
Mambo ya Kibiti mbona ya zamani? Zaidi ya hayo, mbona unamtaja mtu mmoja tu wakati wengi sana 'walipotea' huko Kibiti, wakiwemo polisi, watumishi wa Serikali, wana-CCM, wafanyabiashara na watu wa kawaida wengi tu.

Ilibidi vyombo vya usalama vifanye kazi kubwa sana kukomesha vituko hivyo. Kama ni kuishuku Serikali, hivi kweli Serikali ingeweza kuwa na mkakati wa 'kupoteza' polisi au watumishi wa Serikali na CCM na watu wengine wa kawaida tu? Haiingii maanani.
 
Back
Top Bottom