Prof. Lipumba unakumbuka ulichosema? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Prof. Lipumba unakumbuka ulichosema?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Facts1, Nov 5, 2010.

 1. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  BARAZA Kuu la Uongozi la Taifa la CUF, limesema wawakilishi walioshinda majimbo ya Pemba na Unguja, watakula kiapo na kuingia ndani ya Baraza la Wawakilishi lakini hawatatoa ushirikiano kwa Serikali isiyo halali hadi uchunguzi wa uchaguzi utakapofanyika.


  Akitoa tamko kuhusiana na Uchaguzi MKuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 30 Mwaka huu (2005), Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba alisema uchaguzi huo ulitawaliwa na mizengwe,hadaa, udanganyifu na wizi wa kura.

  Alisema hatua ya wawakilishi hao kutoshirikiana na Wawakilishi kutoka CCM pamoja na Serikali itakayoundwa visiwani humo inatokana na kutotekelezwa masharti ya muafaka yaliyokubaliwa.

  "Baraza Kuu halitambui matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa na ZEC,(Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar) pia halimtambui Amani Karume kama Rais wa Zanzibar pamoja na Serikali atakayounda mpaka litakapojiridhisha baada ya uchunguzi huru na wakina kufanyika," alisema Prof. Lipumba.

  Akielelezea msimamo wa CUF uliotolewa na Baraza hilo, Prof.Lipumba alisema wanaitaka Serikali iunde haraka Tume ya Uchunguzi ambayo itahusisha chombo huru, watu au taasisi inayoheshimika.
   
Loading...