Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,735
- 6,292
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema Rais Samia Suluhu Hassan hawezi kukwepa lawama kufuatia tukio la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Mbowe.
"Jeshi la Polisi lingeweza kumkamata Freeman Mbowe popote hata alipokuwa msibani, kama kweli kuna tuhuma zozote dhidi yake.Kumkamata kufuatia kongamano lao la Mwanza na kisha kudai kwamba anatuhumiwa kwa ugaidi, ni jambo linaloibua maswali mengi bila majibu.......CUF kinatoa wito kwa Serikali kupitia Jeshi la Polisi, kuwaachia viongozi wote wa CHADEMA wanaoshikiliwa kufuatia Kongamano la Mwanza" . Aliongeza Prof. Lipumba"
Pia Lipumba ameiomba Serikali imuachie huru Freeman Mbowe na wenzake, waliokamatwa jijini Mwanza, wakijiandaa kufanya kongamano la kudai Katiba Mpya.