Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba: Nchi hii inahitaji Rais mchumi na mwenye huruma na Watanzania. Mkinichagua kuwa Rais nitafuta umasikini katika nyanja zote

CUF Habari

Verified Member
Dec 12, 2019
212
250
"NCHI HII INAHITAJI RAIS MCHUMI NA MWENYE HURUMA NA WATANZANIA MKINICHAGUA KUWA RAIS NTAFUTA UMASIKINI KATIKA NYANJA ZOTE," PROF. LIPUMBA, NZEGA - TABORA

Ukuaji wa uchumi wa Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini. Idadi ya watu masikini kwa kutumia kipimo cha taifa cha umasikini (mtu mzima kutumia shilingi 50,000/ au zaidi kwa mwezi) imeongezeka toka watu milioni 12.3 mwaka 2011 na kufikia watu milioni 14 mwaka 2018. Kwa kutumia kipimo cha kimataifa cha umaskini, Watanzania zaidi ya milioni 27 ni masikini.

Utafiti uliofanywa na serikali mwaka 2016 kuhusu umaskini wa watoto (Child Poverty in Tanzania) ulibaini kuwa asilimia 74 ya watoto wa Tanzania wanaishi katika mazingira ya umaskini kwa tafsiri pana inayojumuisha lishe, afya, hifadhi iliyo salama, elimu, mazingira, maji na makazi.

IMG_20200916_183634_480.jpg
Screenshot_20200916-180746.png
IMG_20200916_181536_339.jpg
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
18,340
2,000
"Nitafuta umaskini nyanja zote"

Wote tujiulize kama hiki kitu kinawezekana kwa miaka 5 au 10 atakayokaa madarakani.
 

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,198
2,000
CUF Habari,hamuoni hata aibu kujitambulisha kuwa na ninyi ni wapinzani?

Mlininuliwa na Maccm,yamewatelekeza .

Sharif amewaacha kwenye mataa.
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
981
1,000
Ukidhindwa kufuta umaskini wa mawazo, sahau kuufuta unaskini mwingine wa aina yeyote.
 

Omusolopogasi

JF-Expert Member
Aug 31, 2017
3,886
2,000
Uzi umeshindwa kupata hata comments 10! Ndio malipo ya usaliti haya. Fanyeni kama Mrema - unga mkono juhudi kwa wazi bila ya kujificha. Wananchi wanaenda kuwafuta katika ramani ya siasa ya nchi.
"NCHI HII INAHITAJI RAIS MCHUMI NA MWENYE HURUMA NA WATANZANIA MKINICHAGUA KUWA RAIS NTAFUTA UMASIKINI KATIKA NYANJA ZOTE," PROF.LIPUMBA, NZEGA - TABORA...
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,908
2,000
Prof Lipumba amesema Tanzania inahitaji Rais mchumi na mwenye huruma kwa watanzania.

Ndiposa najiuliza huyu Prof Lipumba ana huruma gani kwa watanzania?
Atueleze kwanza matumizi ya ruzuku iliyolalamikiwa na CAG.

Maendeleo hayana vyama!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom