Elections 2010 Prof. Lipumba na Wizi wa Kura

Supervisor

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
559
207
Poleni na vuguvugu wana JF.

Jamani mm kuna kitu najiuliza sana kwa nn Prof Lipumba hakuzungumzia suala la yeye au chama chake kwa ujumla kwamba ktk zoezi zima ka upigaji na kuhesabu kura kulikuwa na udanganyifu mkubwa? Hv kwel hakuona hilo? Nilichomsikia alikuwa anadai tume huru ya uchaguzi basi. Prof bado simuelewi kabsa..! Naomba kupata mawazo yenu wana JF.
 
Hivi leo hii kuna tofauti kati ya CCM na CUF.
CUF kaolewa na CCM ndoa ya mkeka kasha pigwa unyumba katulia kazi kwenu.
 
Asingeweza fanya hivyo,unafiki ulimlazimu ili kumshikia mwenzake wa zenji mwamvuli
 
Lipumba hawezi kuuma mkono unaomlisha, hilo analijua fika kuwa ugali wake unatoka CCM via Zanzibar!!
 
WASOMI HUWA HAWAHITAJI KUIMBA WIMBO WA AINA MOJA SIKU ZOTE... PROFESA ALIPOSEMA AMEIBIWA MBOWE AKAGOMA KWENDA KWENYE KUAPISHWA KWA RAIS MH. MBOWE ALIBEZA. SIASA ZA TANZANIA NI NGUMU SANA, WACHENI KUDANDIA MAGARI YENYE KWENDA KASI.... NITAWAKUMBUSHA:

12/25/2005
Na Mwandishi Wetu
ALIYEKUWA mgombea urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema hajashindwa uchaguzi, bali huu ni mwanzo wa harakati mpya za kuwakomboa watanzania.

Badala yake, amesema wanaostahili kupewa pole ni Watanzania kwa kutumiwa, kutishwa na kurubuniwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi wakakirejesha madarakani.
Akizungumza na gazeti hili wiki hii jijini Dar es Salaam, Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, alisema kwamba badala ya wananchi kumsikitikia kwa kushindwa kuwa rais, wanapaswa kulisikitikia taifa, ambalo limepoteza fursa ya kufanya mabadiliko ya kweli ya

Akizungumzia hatua yake ya kukubali matokeo ya uchaguzi, na hata kushiriki sherehe za kuapishwa kwa Rais Kikwete wakati wapinzani wengine wamesusa, Mbowe alisema kususa si mbinu yake ya kisiasa.
Alitoa mfano wa baadhi ya wanasiasa wa upinzani ambao wamekuwa wakisusia na kukataa matokeo ya uchaguzi tangu mwaka 1995, akasema mbinu hiyo haikuwawezesha kuidhoofisha CCM....
Kwa sababu hiyo, alisema yeye na chama chake wameona ni vema kufanya siasa za kisasa, za kistaarabu na kiungwana kwa kuwa hata walipokuwa wanaingia kwenye ushindani, walijua kuwa kuna kushinda na kushindwa.
Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za nchi, hata kama mshindi kapatikana kwa njia zisizo sahihi, akishatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hakuna anayeweza kuhoji mahali popote.
ati wapinzani wameendelea kusema hawamtambui Rais Benjamin Mkapa (aliyestaafu wiki hii) hawakuweza kumzuia kuwaongoza kwa miaka 10.
Kwa sababu hiyo, alisema yeye na chama chake wameona ni vema kufanya siasa za kisasa, za kistaarabu na kiungwana kwa kuwa hata walipokuwa wanaingia kwenye ushindani, walijua kuwa kuna kushinda na kushindwa.
Hata hivyo, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sheria za nchi, hata kama mshindi kapatikana kwa njia zisizo sahihi, akishatangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) hakuna anayeweza kuhoji mahali popote.

JE HADI HAPA TUTASEMA BADO TUNA WANAMAPINDUZI WA UKWELI???

NIMESOMEKA HAPO:smile-big: HUYO HUYO ANATUAMBIA TUSIKUBALI MPAKA KIELEWEKE
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom