Prof. Lipumba: ACT-Wazalendo imeongeza damu yenye virusi ikidhani ni damu salama

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi,

Pamoja na tuhuma za baadhi ya wanabodi kutotazama TBC kwa hoja kuwa eti ina boa, hadi wengine kuuita TBCCM, lakini hii ndio TV yetu pekee inayoendeshwa kwa kodi zetu, hivyo kutazama TBC sio issue ya choice bali ni wajibu, hivyo tutimize wajibu wetu kwa kuangalia TBC. Mimi naangalia TBC japo nina kaugomvi kidogo na wife hapa kuhusu hili, yeye anataka kuangalia Clouds 360, hivyo sometimes lazima ubaba utumike kinguvu, TV ya kuangaliwa na baba ni TBC!, hivyo mtu kuwa mzalendo wa kweli wa taifa lako, ni pamoja na kuiangalia TV ya Taifa lako, hata kama ni kweli sometimes inaboa, uzalendo ni kuweka utaifa mbele, hivyo TV ya Taifa ndio TV yetu sisi wazalendo wa kweli wa taifa letu, hivyo tunaangalia TBC.

Leo Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa mujibu wa Msajili wa Vyama Siasa, na kwa mujibu wa Mahakama, Prof. Ibrahim Lipumba, yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo.

Natoa wito, karibuni tumsikilize.

Paskali
Update 1
Prof. Lipumba amesema kazi kubwa ya kwanza ya chama chake ni kuwaleta pamoja wanachama wake, kuwa kitu kimoja kujenga chama.

Lipumba amemshutumu Maalim Seif kwa kusema analeta usultani, anachotaka yeye tuu ndicho, hivyo kitendo cha kuhamia ATC chama chenye sera tofauti kabisa na malengo ya CUF, huko sasa kutakuwa ni kumfuata mtu kama usultani na sio kufuata sera au itikadi.

Sasa wameweka kipande cha Maalim Seif Akitangaza kuhamia ACT, kwa msisitizo kuwa "umma haujawahi kushindwa hata mara moja", hivyo Maalim Seif anaamini umma utashinda ndani ya ACT Wazalendo.

Prof. Lipumba anasisitiza ofisi za CUF nchini kote ni mali ya chama cha CUF na sio mali ya mtu, hivyo amelaani kitendo cha watu kupora ofisi za CUF na kuzigeuza ni za ACT, amesema atazipigania ofisi hizo ambalo ni mali halali ya CUF, lazima zibaki CUF.

Prof. Lipumba amesema CUF bado ni chama imara, na kutolea mfano Mrema alipohama na wafuasi na wanachama wake kutoka NCCR Mageuzi kwenda TLP, sasa wako wapi?, NCCR bado ipo imara, Mrema na TLP yake wana hali gani?.

Prof. Lipumba amekiponda ACT, ukimondoa Zitto na mwana mikakati wake Prof. Kitila Mkumbo, amesema ACT ni chama hoi bin taaban kama mgonjwa mahututi aliyepo ICU akihitaji kuongezewa damu, bahati damu yenyewe aliyoongezewa ni damu yenye virusi, badala ya kuponya mgonjwa, itamuangamiza.
Prof. Lipumba amemalizia kwa kusisitiza CUF itashirikiana na vyama vyenye kutaka ushirikiano wa kweli.

My Take ya Lipumba, ningekuwa mimi, ningejiepusha na kusema jambo lolote negative kumhusu Maalim Seif, Lipumba anajua fika kuna watu wanamuabudu Maalim Seif, hivyo akisema anything kumhusu muabudu huyu, watamuona kama amekufuru.

Kipindi kimemalizika, na hapo hapo, wife akanipokonya remote, haikupita hata dakika, akabadilisha!.
Asanteni kwa kufuatilia.
Paskali
 
Wapinzani wa kweli huwa hawaalikwi TBCCM!!

Nakumbuka Jiwe alivyoingia Magogoni Lipumba ndio alikuwa mgeni wa kwanza kumtembelea kitaifa na wakaongea na akakili kuwa bwana mkubwa kasema atamsaidia kwenye kesi yake ambayo allifunguliwaga enzi za JK kwa kufanya mkutano usiohalali na alipigwa virungu,ndani ya wiki kesi ile ilifutwa!!!
 
Lipumba amemshutumu Maalim Seif kwa kusema analeta usultani, anachotaka yeye tuu ndicho, hivyo kitendo cha kuhamia ATC chama chenye sera tofauti kabisa na malengo ya CUF, huko sasa kutakuwa ni kumfuata mtu kama usultani na sio kufuata sera au itikadi.
 
Wapinzani wa kweli huwa hawaalikwi TBCCM!!

Nakumbuka Jiwe alivyoingia Magogoni Lipumba ndio alikuwa mgeni wa kwanza kumtembelea kitaifa na wakaongea na akakili kuwa bwana mkubwa kasema atamsaidia kwenye kesi yake ambayo allifunguliwaga enzi za JK kwa kufanya mkutano usiohalali na alipigwa virungu,ndani ya wiki kesi ile ilifutwa!!!

Namsikiliza hapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanabodi,

Pamoja na tuhuma za baadhi ya wanabodi kutotaza TBC kwa hoja kuwa ina boa, lakini hii ndio TV yetu pekee inayoendeshwa kwa kodi zetu, hivyo kutazama TBC sio issue ya choice bali ni wajibu, hivyo tutimize wajibu wetu kuangalia TBC.

Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa mujibu wa Msajili wa Vyama Siasa, na kwa mujibu wa Mahakama, Prof. Ibrahim Lipumba, yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo.

Natoa wito, karibuni tumsikilize.

Paskali
Sidhani kama hii ni TV ya Taifa bali ni chombo cha propaganda cha chama kinachotumia fedha za umma.

Leo wameamua kumwalika mamluki wao lakini kamwe hawatamwalika maalim.

Ni afadhali kuwasikiliza vijana mitaani kama source ya habari kuliko kupoteza muda kutazama huo upuuzi.
 
Lipumba amemshutumu Maalim Seif kwa kusema analeta usultani, anachotaka yeye tuu ndicho, hivyo kitendo cha kuhamia ATC chama chenye sera tofauti kabisa na malengo ya CUF, huko sasa kutakuwa ni kumfuata mtu kama usultani na sio kufuata sera au itikadi.
Halafu ndio mnasema prof wa uchumi huyo....kazi ipo

Sent from my TECNO K7 using Tapatalk
 
Wanabodi,

Pamoja na tuhuma za baadhi ya wanabodi kutotaza TBC kwa hoja kuwa ina boa, lakini hii ndio TV yetu pekee inayoendeshwa kwa kodi zetu, hivyo kutazama TBC sio issue ya choice bali ni wajibu, hivyo tutimize wajibu wetu kuangalia TBC.

Mwenyekiti wa CUF Taifa kwa mujibu wa Msajili wa Vyama Siasa, na kwa mujibu wa Mahakama, Prof. Ibrahim Lipumba, yuko live TBC kwenye kipindi cha Jambo.

Natoa wito, karibuni tumsikilize.

Paskali
kichwa cha habar chako tu kinaonyesha uko upande gani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
My Take ya Lipumba, ningekuwa mimi, ningejiepusha na kusema jambo lolote negative kumhusu Maalim Seif, Lipumba anajua fika kuna watu wanamuabudu Maalim Seif, hivyo akisema anything kumhusu muabudu huyu, watamuona kama amekufuru.
 
30 Reactions
Reply
Back
Top Bottom