Prof. Lipumba: JK anastaahili kuwa Waziri wa Sanaa na Michezo

BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
117
661
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema kuwa kutokana na usanii wa Rais Kikwete alistahili kuwa Waziri wa michezo na utamaduni ili awe na kazi moja tu ambayo ni ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua michezo ya warembo.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya ambao walihudhuria katika mkutano wa UKAWA uliofanyika katika uwanja unaojulikana kwa jina la Dk.Slaa uliopo jijini Mbeya.

Alisema analazimika kusema hivyo kutokana na usanii wake ambao anaufanya wakati wa kuongoza nchi kutokana kwa kutokuwa na maamuzi.

“Wakati nagombea urais nilitamani nikiwa rais niweze kumchagua Kikwete kuwa Waziri wa Michezo na utamaduni ili aweze kuwa na kazi moja ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua sherehe za warembo.

“Nilitamani kufanya hivyo kutokana na kile nilichokiamini kuwa rais Kikwete siku zote ni msanii na ndiyo maana amekuwa akishindwa kusimamia maamuzi ndani ya serikali yake ikiwa ni pamoja na kushindwa kukubaliana na mawazo ya vyama vya siasa vya upinzani kwa kudai katiba mpya

“Lakini nilimwona Rais Kikwete kutokuwa Msanii pale ambapo alikubali maoni ya vyama vya upinzani kukubali kuanzisha mchakato wa katiba mpya na kutokana na hilo nililazimika kumwandikia barua ya kumwomba radhi kwa kumwita msanii nikidhani sasa ameachana na usanii wake..

“Lakini cha kushangaza wakati wa uzinduzi wa rasimu ya katiba alipokuja kuzindua Bunge Maalum la Katiba alikuwa kioja kwa kupinga tume ya Jaji Warioba ambayo aliiunda mwenyewe jambo ambalo lilinifanya kumwona rais Kikwete kuwa bado ni Msanii na bado hajaacha usanii wake”alisema Prof Lipumba.

Aidha alisema kuwa kwa upande wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda hana lolote ambalo anaweza kulifanya katika serikali yake bali amefanikiwa kuanzisha mkoa mpya wa katavi tu.

Alisema kuwa CCM imekuwa ikiwazeesha wananchi wa Tanzania kutokana na kuwa na viongozi wasiojali masilahi ya wananchi hususani vijana wa Jiji la Mbeya.

Kwa upande wake Alatanga Nyagawa ambaye ni makamu mwenyekiti Chadema nyanda za Kusini alisema kauli za Katibu wa CCM taifa Abrahamanhman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Nauye kudai kuwa wananchi hawana haja ya katiba ni sawa na kuwatusi wananchi.

Mbali na hilo alisema kuwa ili kuthibitisha maneno yao kuna kila sababu ya kujia nia yao ni nini kwani wanafanya mambo ambayo utadhani kuwa wao siyo watanzania.

Hata hivyo alisema kuwa Kinana amekuwa akifanya biashara nyingi ambazo zinatakiwa kuchunguzwa uhalali wake kutokana na kuwa amekuwa akituhumiwa kufanya biashara ambazo si halali.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema kuwa kutokana na usanii wa Rais Kikwete alistahili kuwa Waziri wa michezo na utamaduni ili awe na kazi moja tu ambayo ni ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua michezo ya warembo.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya ambao walihudhuria katika mkutano wa UKAWA uliofanyika katika uwanja unaojulikana kwa jina la Dk.Slaa uliopo jijini Mbeya.

Alisema analazimika kusema hivyo kutokana na usanii wake ambao anaufanya wakati wa kuongoza nchi kutokana kwa kutokuwa na maamuzi.

"Wakati nagombea urais nilitamani nikiwa rais niweze kumchagua Kikwete kuwa Waziri wa Michezo na utamaduni ili aweze kuwa na kazi moja ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua sherehe za warembo.

"Nilitamani kufanya hivyo kutokana na kile nilichokiamini kuwa rais Kikwete siku zote ni msanii na ndiyo maana amekuwa akishindwa kusimamia maamuzi ndani ya serikali yake ikiwa ni pamoja na kushindwa kukubaliana na mawazo ya vyama vya siasa vya upinzani kwa kudai katiba mpya

"Lakini nilimwona Rais Kikwete kutokuwa Msanii pale ambapo alikubali maoni ya vyama vya upinzani kukubali kuanzisha mchakato wa katiba mpya na kutokana na hilo nililazimika kumwandikia barua ya kumwomba radhi kwa kumwita msanii nikidhani sasa ameachana na usanii wake..

"Lakini cha kushangaza wakati wa uzinduzi wa rasimu ya katiba alipokuja kuzindua Bunge Maalum la Katiba alikuwa kioja kwa kupinga tume ya Jaji Warioba ambayo aliiunda mwenyewe jambo ambalo lilinifanya kumwona rais Kikwete kuwa bado ni Msanii na bado hajaacha usanii wake"alisema Prof Lipumba.

kama kweli lipumba angekuwa na uwezo wa fikra pana angemshauli mbowe juu ya hili.
[h=2]Prof Baregu: Siu[/h][h=2]Prof Baregu: Siungi Mkono Maamuzi juu ya Zitto ila "SULUHU" ni njema[/h]
UAMUZI wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumvua madaraka, Zitto Kabwe unadaiwa kuanza kukitesa chama hicho na kwamba sasa uongozi wa juu umeamua kusaka suluhu ya jambo hilo.

Taarifa ambazo RAI Jumatano imezinasa kutoka Kinondoni, jijini Dar es Salaam yalipo Makao Makuu ya Ofisi za Chadema, zinaeleza kuwa, tayari baadhi ya viongozi wamekubali kuketi meza moja ya mazungumzo na Zitto baada ya kupewa ushauri na watu mbalimbali wakiwamo wasomi wakubwa wanaoheshimika ndani ya chama hicho.

Hatua hiyo imekuja wakati ambao tayari uamuzi wa kuwavua madaraka, Zitto pamoja na Mwanazuoni wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo, umesababisha mtafaruku na mgawanyiko ndani ya chama.

Uamuzi wa kuwavua uongozi makada hao ambao ulitangazwa na Tundu Lissu mbele ya Freeman Mbowe, ulipokelewa kwa mtazamo tofauti na makada wa chama hicho, ambapo baadhi waliamini kuwa ni sahihi huku wengine wakiyapinga kwa madai kuwa yanaua demokrasia hasa kwa chama ambacho kimejipambanua kupigania demokrasia nchini.

Miongoni mwa makada wanaodaiwa kupingana na hatua hiyo ya kamati kuu ni wasomi, ambapo mmoja wao amemtaka Mbowe kutumia nafasi yake ya uenyekiti kuzungumza na Zitto ili kukinusuru chama.

Msomi huyo aliyebobea katika masuala ya sheria nchini, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, pamoja na kutokubaliana na baadhi ya vitendo vya Zitto, anadaiwa kuweka wazi kwamba utaratibu uliotumika kumuadhibu si sahihi na hivyo ni vema jitihada za haraka zikafanyika ili kulimaliza suala hilo.

Kwa mujibu wa taarifa hizo kutoka kwenye chanzo cha kuaminika kilicho karibu na Mbowe, mara baada ya kutangazwa kwa maamuzi ya kuwavua uongozi Zitto, Dk. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, msomi huyo alizungumza kwa kina na Mwenyekiti wake na inaelezwa kuwa baadhi ya maneno mazito aliyotumia kumfikishia ujumbe yalisababisha Mbowe amwage machozi.

"Mwenyekiti alilia baada ya kuelezwa maneno mazito na mmoja wa wanasheria wa chama, alimtaka aachane na mivutano hii na badala yake akae mezani na Zitto ili wayamalize," alisema mtoa habari wetu.

Imeelezwa kuwa baada ya ushauri huo, Mbowe alimuomba mwanasheria huyo kumtafuta, Zitto ili wakae mezani.

Imebainika kwamba ni suala gumu kwa Mbowe kukaa meza moja na Zitto bila ya kuwepo kwa mtu wa kuwasuluhisha kutokana na wawili hao kuwa na migogoro iliyodumu kwa muda mrefu.

Katika kuhakikisha Mbowe na Zitto wanakutana na wanamaliza tofauti zao zilizoanza kuchomoza mwaka 2009, tayari kuna mipango ya kuunda Kamati ya usuluhishi ambayo inatajwa huenda ikaongozwa na Profesa Mwesigwa Baregu na Mabere Marando.

Jukumu la wateule hao ni kuhakikisha wanawakutanisha mahasimu hao ili kurejesha umoja na amani ndani ya chama.

Aidha zipo taarifa kwamba katika kuhakikisha amani ya moja kwa moja inarejea ndani ya chama, Zitto amepangiwa kupewa nafasi ya kuwania umakamu Mwenyekiti Bara, huku Mbowe akiachiwa nafasi yake.

Mbali na kuachiwa nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti, pia zipo taarifa kwamba Zitto ataachiwa jukumu la kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, wakati ambapo mwaka 2015, Dk. Willbrod Slaa atawania nafasi hiyo kwa mara ya pili.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa, Profesa Baregu na Marando wamepewa jukumu hilo la kusuluhisha, kutokana na ushawishi walionao kwa pande zote mbili.

Inaelezwa kuwa Profesa Baregu amekuwa ni muumini wa demokrasia ya kweli ndani ya chama na kwamba hakukubaliana na maamuzi ya kumvua uongozi Zitto na Dk. Kitila na ndiyo sababu iliyomchagiza kutaka kujiuzulu nafasi yake ya ujumbe wa Mkutano Mkuu.

Profesa Baregu, Said Arfi ambaye amejiuzulu nafasi yake ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho na Dk. Kitila Mkumbo ni miongoni mwa makada wanaoaminika kusimamia demokrasia ya kweli ndani ya chama.

Msemaji wa Chadema, John Mnyika alipotafutwa kuzungumzia taarifa hizo, hakukubali wala kukataa badala yake alisema masuala hayo hayajui.

Kwa upande wake, Zitto ambaye kwa sasa yuko nchini Uingereza kwa kazi za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), aliliambia Rai Jumatano kwamba taarifa hizo za chama kusaka suluhu naye amezisikia na endapo atatakiwa kufanya hivyo haoni sababu ya kukataa.

"Nia yangu ni kuona tunavuka salama kwenye upepo huu na ndio maana nimetangaza kwamba sitoki Chadema, njia pekee ya kuyamaliza haya ni kuzungumza, sidhani kama nitakuwa na kipingamizi," alisema Zitto.

Kwa upande mwingine jana chama hicho kimewaandikia barua yenye mashitaka 11, Zitto, Mwigamba na Dk. Kitila.

Mbali na mashitaka hayo, pia katika barua hizo, wamepewa muda wa siku 14 kujieleza kimaandishi ni kwanini wasichukuliwe hatua za zaidi, kabla ya kujitetea tena mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, Mnyika, alisema sekretarieti iliyokutana juzi, ilikamilisha uamuzi uliopitishwa na Kamati Kuu ya kuwavua nyadhifa zao ndani ya chama.

Alisema sekretarieti ilijiridhisha kuwa makosa yao yalitokana na waraka ambao kimsingi ulikiuka kanuni, maadili na taratibu za chama.

"Mashitaka na makosa 11 waliyofanya, yamejikita katika uamuzi wa Kamati Kuu na si maneno ambayo waliyazungumza mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wao wa Jumapili.

Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, alisema Zitto na wenzake wasipojieleza ndani ya siku 14, taratibu ambazo hakuzitaja zitafuatwa.

Aidha, alimshangaa Zitto kupoteza lengo kwa kuwaambia waandishi wa habari kuwa amefukuzwa kwa sababu za uongo na kwamba ni za kizushi.

"Walichokifanya ni kupoteza lengo kwamba wamefukuzwa kwa masuala ya PAC (Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali), posho za vikao vya Bunge, kuuza majimbo yetu ya uchaguzi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na mambo mengine waliyoyataja.

"Wamefukuzwa kwa kufanya mapinduzi bila kufuata utaratibu, yaani kwa kifupi walikiuka maadili, hata hivyo, katika mashitaka yao hayakuzungumzia habari za PAC," alisema Lissu.

Kuhusu kauli ya Wakili wa Zitto, Albert Msendo, kwamba Kamati Kuu ilijivika mamlaka yasiyoihusu kuwavua nyadhifa zao, isipokuwa Baraza Kuu, Lissu alisema Kamati Kuu ilikuwa sahihi kuchukua uamuzi ule.

Kuhusu kauli ya Zitto kwamba ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu ndani ya Chadema, alisema si kweli kwani haiwezekani amtukane Mwenyekiti (Freeman Mbowe), kisha aseme anaheshimu chama.

Aidha Chadema imesema waraka uliosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kuchapishwa na baadhi ya magazeti ni feki, na kwamba waraka halisi wanao na watautoa kwenye mitandao wakati ukifika.

HISTORIA YA MGOGORO WA ZITTO NA MBOWE

Historia ya mgogoro wa Zitto na Mbowe inaanzia mwaka 2009, wakati Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alipoamua kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti kwa staili ya kumshtukiza Mbowe ambaye alikuwa akiwania kwa awamu ya pili.

Mbowe alichukua nafasi hiyo mwaka 2004 kutoka kwa marehemu Bob Makani, ambaye alikiongoza chama hicho kwa awamu moja kutoka mwaka 1998 hadi 2004, kama alivyofanya mtangulizi wake, Edwin Mtei ambaye ndiye mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho aliyekiongoza kutoka mwaka 1993 hadi 1998.

Katika kipindi cha awamu ya kwanza Mbowe alifanikiwa kuimarisha harakati za chama hicho, ambapo aliweza kuongeza idadi ya wabunge kutoka sita walioachwa na Makani hadi kufikia 11, watano wakiwa ni wa kuchaguliwa na sita wa kuteuliwa.

Hatua hiyo ilimpa hamasa mwenyekiti huyo kukiongoza zaidi chama, ambapo mwaka 2009 wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani, alionesha dhahiri kukataa kupingwa kwenye uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Kiramuu, jijini Dar es Salaam.

Maamuzi ya Zitto kujitosa kuwania nafasi hiyo ya uenyekiti, yaliibua msuguano mkali kati yake na Mbowe aliyekuwa akiungwa mkono na muasisi wa chama hicho, Mtei pamoja na baadhi ya makada waliokuwa na dhana kwamba Mwenyekiti huyo hastahili kupingwa.

Hofu ya Mbowe kupingwa ilizalisha makundi ndani ya chama, ambapo kundi la mwenyekiti huyo lilimuona Zitto ni mtovu wa nidhamu na hamuheshimu kiongozi wake na kwamba hakustahili kumpinga mtu ambaye hajamaliza muhula wake wa pili wa uongozi ndani ya chama.

Wanamtandao wa Mbowe wakaibua hoja kwamba ni vema Zitto akaondoa jina lake kwenye kuwania nafasi hiyo, ili kukiepusha chama na anguko wakati huo kikijiandaa kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kwamba kama chama kingeingia kwenye uchaguzi na mgawanyiko hali ingekuwa mbaya.

Jitihada za haraka za kukinusuru chama na mpasuko zikafanyika, ikiwa ni pamoja na kufanya kikao cha usuluhishi kilichoundwa na wazee kwa nia ya kutafuta muafaka kati ya Zitto na Mbowe, mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alishawishiwa kuliondoa jina lake kwenye kinyang'anyiro hicho.

Hatua hiyo ilififisha dhana ya uwepo wa demokrasia na badala yake ukawa mwanzo wa kuzaliwa kwa makundi.​

[h=2]ngi Mkono Maamuzi juu ya Zitto ila "SULUHU" ni njema[/h]

Lipumba kashindwa kusimamia chama chake mpaka kimekufa leo naye anaweza kumnyoshea kidole mtu mwingine.
 
JK is the most hopeless President kuwahi kutokea Tanzania,,.......Hilo lazima lisemwe...hata kama linaudhi

wenye upungufu wa akili ndiyo wanaamini hivyo lakini wenye akili zao wanajua anachofanya jk mazuzu wabaki wanapiga kelele jk kaweza na sasa anasonga mbele.
 
Huu ndio unafiki wa siasa za Tanzania

lipumba alionekana msikitini akiwaambia waumini jinsi walivyoshiriki kuokoa jahazi JK asishindwe 2010 Leo anaongea utumbo huo???

Siasa za upinzani ni uchumia tumbo tu wananchi tusitekwe na ulaghai wao
 
Naomba isomeke hivii: wenye upungufu wa akili ndiyo wasioamini hivyo lakini wenye akili zao wanajua anachofanya Jk mazuzu yabaki yanashangilia. jk kashidwa na sasa anamalizia muda wake.
 
Hapana,kwa hii list alitakiwa kuwa waziri wa Mapenzi.Kwa uchache hawa ndio watoto wa JK, umri wao na mama zao walipo

1. Mustafa Jakaya 33-Kigoma
2. Mwanaharusi Jakaya-36-Kigoma
3. Isihaka Jakaya-34-Rukwa
4. Halfani Jakaya-31-Bagamoyo
5. Faudhia Jakaya-33-Dodoma
6. Siwema Jakaya-31-Mtwara
7. Faudh Jakaya -3-Iringa kwa Assas
8. Maulid Jakaya-18-Tabora
9. Salama Jakaya-33-Mama alifariki
10. Ridhiwani 36-Mama hajulikani
11. Miraji Kikwete 33- Mama hajulikani
12. Mwanaasha Jakaya- 18- Chalinzr
14. Pili-6-Ikulu
15. Havintishi-5-Ikulu
16. Mwalusembe-4-Ikulu
17. Hafidh 16-Ikulu
 
Huu ndio unafiki wa siasa za Tanzania

lipumba alionekana msikitini akiwaambia waumini jinsi walivyoshiriki kuokoa jahazi JK asishindwe 2010 Leo anaongea utumbo huo???

Siasa za upinzani ni uchumia tumbo tu wananchi tusitekwe na ulaghai wao

ndio kwa kigezo hicho hicho Lipumba katumia kuamini JK ni zuzu.unaendelea kuumbua
 
Lipumba kashindwa kusimamia chama chake mpaka kimekufa leo naye anaweza kumnyoshea kidole mtu mwingine.
Lakini hata sisi wengine tulioshindwa tena mambo mengi bado tunao uwezo wa kuwaona walioshindwa kama sisi!

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema kuwa kutokana na usanii wa Rais Kikwete alistahili kuwa Waziri wa michezo na utamaduni ili awe na kazi moja tu ambayo ni ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua michezo ya warembo.

Alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya ambao walihudhuria katika mkutano wa UKAWA uliofanyika katika uwanja unaojulikana kwa jina la Dk.Slaa uliopo jijini Mbeya.

Alisema analazimika kusema hivyo kutokana na usanii wake ambao anaufanya wakati wa kuongoza nchi kutokana kwa kutokuwa na maamuzi.

"Wakati nagombea urais nilitamani nikiwa rais niweze kumchagua Kikwete kuwa Waziri wa Michezo na utamaduni ili aweze kuwa na kazi moja ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua sherehe za warembo.

"Nilitamani kufanya hivyo kutokana na kile nilichokiamini kuwa rais Kikwete siku zote ni msanii na ndiyo maana amekuwa akishindwa kusimamia maamuzi ndani ya serikali yake ikiwa ni pamoja na kushindwa kukubaliana na mawazo ya vyama vya siasa vya upinzani kwa kudai katiba mpya

"Lakini nilimwona Rais Kikwete kutokuwa Msanii pale ambapo alikubali maoni ya vyama vya upinzani kukubali kuanzisha mchakato wa katiba mpya na kutokana na hilo nililazimika kumwandikia barua ya kumwomba radhi kwa kumwita msanii nikidhani sasa ameachana na usanii wake..

"Lakini cha kushangaza wakati wa uzinduzi wa rasimu ya katiba alipokuja kuzindua Bunge Maalum la Katiba alikuwa kioja kwa kupinga tume ya Jaji Warioba ambayo aliiunda mwenyewe jambo ambalo lilinifanya kumwona rais Kikwete kuwa bado ni Msanii na bado hajaacha usanii wake"alisema Prof Lipumba.

Aidha alisema kuwa kwa upande wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda hana lolote ambalo anaweza kulifanya katika serikali yake bali amefanikiwa kuanzisha mkoa mpya wa katavi tu.

Alisema kuwa CCM imekuwa ikiwazeesha wananchi wa Tanzania kutokana na kuwa na viongozi wasiojali masilahi ya wananchi hususani vijana wa Jiji la Mbeya.

Kwa upande wake Alatanga Nyagawa ambaye ni makamu mwenyekiti Chadema nyanda za Kusini alisema kauli za Katibu wa CCM taifa Abrahamanhman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Nauye kudai kuwa wananchi hawana haja ya katiba ni sawa na kuwatusi wananchi.

Mbali na hilo alisema kuwa ili kuthibitisha maneno yao kuna kila sababu ya kujia nia yao ni nini kwani wanafanya mambo ambayo utadhani kuwa wao siyo watanzania.

Hata hivyo alisema kuwa Kinana amekuwa akifanya biashara nyingi ambazo zinatakiwa kuchunguzwa uhalali wake kutokana na kuwa amekuwa akituhumiwa kufanya biashara ambazo si halali.
swali dogo tumenufaika nn na u prof wako wa uchumi
 
Hapana,kwa hii list alitakiwa kuwa waziri wa Mapenzi.Kwa uchache hawa ndio watoto wa JK, umri wao na mama zao walipo

1. Mustafa Jakaya 33-Kigoma
2. Mwanaharusi Jakaya-36-Kigoma
3. Isihaka Jakaya-34-Rukwa
4. Halfani Jakaya-31-Bagamoyo
5. Faudhia Jakaya-33-Dodoma
6. Siwema Jakaya-31-Mtwara
7. Faudh Jakaya -3-Iringa kwa Assas
8. Maulid Jakaya-18-Tabora
9. Salama Jakaya-33-Mama alifariki
10. Ridhiwani 36-Mama hajulikani
11. Miraji Kikwete 33- Mama hajulikani
12. Mwanaasha Jakaya- 18- Chalinzr
14. Pili-6-Ikulu
15. Havintishi-5-Ikulu
16. Mwalusembe-4-Ikulu
17. Hafidh 16-Ikulu

Heeeeeeee!!!!! Hivi eeeeeeee!!!! Hili nalo neno!
 
kama kweli lipumba angekuwa na uwezo wa fikra pana angemshauli mbowe juu ya hili.
[h=2]Prof Baregu: Siu[/h][h=2]Prof Baregu: ........

Jitihada za haraka za kukinusuru chama na mpasuko zikafanyika, ikiwa ni pamoja na kufanya kikao cha usuluhishi kilichoundwa na wazee kwa nia ya kutafuta muafaka kati ya Zitto na Mbowe, mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini alishawishiwa kuliondoa jina lake kwenye kinyang’anyiro hicho.

Hatua hiyo ilififisha dhana ya uwepo wa demokrasia na badala yake ukawa mwanzo wa kuzaliwa kwa makundi. [/INDENT]
unajaza saver ya jf tu.haujui hata kuandika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom