BAVICHA Taifa
Senior Member
- Jul 25, 2013
- 117
- 661
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba amesema kuwa kutokana na usanii wa Rais Kikwete alistahili kuwa Waziri wa michezo na utamaduni ili awe na kazi moja tu ambayo ni ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua michezo ya warembo.
Alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya ambao walihudhuria katika mkutano wa UKAWA uliofanyika katika uwanja unaojulikana kwa jina la Dk.Slaa uliopo jijini Mbeya.
Alisema analazimika kusema hivyo kutokana na usanii wake ambao anaufanya wakati wa kuongoza nchi kutokana kwa kutokuwa na maamuzi.
Wakati nagombea urais nilitamani nikiwa rais niweze kumchagua Kikwete kuwa Waziri wa Michezo na utamaduni ili aweze kuwa na kazi moja ya kuwa mgeni wa heshima katika kufungua sherehe za warembo.
Nilitamani kufanya hivyo kutokana na kile nilichokiamini kuwa rais Kikwete siku zote ni msanii na ndiyo maana amekuwa akishindwa kusimamia maamuzi ndani ya serikali yake ikiwa ni pamoja na kushindwa kukubaliana na mawazo ya vyama vya siasa vya upinzani kwa kudai katiba mpya
Lakini nilimwona Rais Kikwete kutokuwa Msanii pale ambapo alikubali maoni ya vyama vya upinzani kukubali kuanzisha mchakato wa katiba mpya na kutokana na hilo nililazimika kumwandikia barua ya kumwomba radhi kwa kumwita msanii nikidhani sasa ameachana na usanii wake..
Lakini cha kushangaza wakati wa uzinduzi wa rasimu ya katiba alipokuja kuzindua Bunge Maalum la Katiba alikuwa kioja kwa kupinga tume ya Jaji Warioba ambayo aliiunda mwenyewe jambo ambalo lilinifanya kumwona rais Kikwete kuwa bado ni Msanii na bado hajaacha usanii wakealisema Prof Lipumba.
Aidha alisema kuwa kwa upande wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda hana lolote ambalo anaweza kulifanya katika serikali yake bali amefanikiwa kuanzisha mkoa mpya wa katavi tu.
Alisema kuwa CCM imekuwa ikiwazeesha wananchi wa Tanzania kutokana na kuwa na viongozi wasiojali masilahi ya wananchi hususani vijana wa Jiji la Mbeya.
Kwa upande wake Alatanga Nyagawa ambaye ni makamu mwenyekiti Chadema nyanda za Kusini alisema kauli za Katibu wa CCM taifa Abrahamanhman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi,Nape Nauye kudai kuwa wananchi hawana haja ya katiba ni sawa na kuwatusi wananchi.
Mbali na hilo alisema kuwa ili kuthibitisha maneno yao kuna kila sababu ya kujia nia yao ni nini kwani wanafanya mambo ambayo utadhani kuwa wao siyo watanzania.
Hata hivyo alisema kuwa Kinana amekuwa akifanya biashara nyingi ambazo zinatakiwa kuchunguzwa uhalali wake kutokana na kuwa amekuwa akituhumiwa kufanya biashara ambazo si halali.