Tunkamanin
JF-Expert Member
- Feb 27, 2015
- 951
- 865
Kwanza kabisa jamaa hana siasa za propaganda ni mpambanaji kweli tangu ameanza siasa zake utamuona front line. Pili sio mwanasiasa wa kupinga kila kitu,ukiangalia comment zake nyingi kwa serikali ni kupinga panapostahiki na kupngeza au kuunga mkono panapostahiki.
Tatu jamaa ni msomi aliyebobea kipaji maalum IQ yake iko kuleee ndio maana maamuzianayoyafanya leo wewe utakuja kuyaelewa miaka 3-5 mbele. Nne jamaa anajua anachokifanya na mpaka atakwenda kaburini bado atabaki kuwa ni alama ya upinzani wa kweli Tanzania,hana kiburi hana ghilba,wivu, umimi, kujitia ukuu, ukubwa ,ubwanyenye,umwinyi bali yeye ni mtu wa watu.
Mtu anaeamini kwamba chama sio mali ya mtu na hata wanachama wa chama chake na viongozi wenzake wamekua wakiyasema waziwazi bla ya yeye kukasirika. lakini kwa upande mwingine washindani wake wanatumia sana uongo,ghilba, chuki, kuchafuana, propaganda nyingi sana mitandaoni kumchafua na kuzima image yake.
wamepata kundi fulani kwa kazi yao hiyo, hasa kwa hawa vijana wa siku hizi ambao kwao siasa ni matusi, uongo, propaganda za kuchafuana, na kupinga kila kitu.
Kizazi cha watanzania wa sasa, wazee wa nyuma ya keyboard. wao ndio waliomleta lowasa, na wakamsafisha na akawapiga chini laiti kama wangekuwa na akili basi wangemwendea prof na kumwomba radhi, ya kwamba ebwana eeh MTU MZITO, ULIKUWA SAHIHI KIPINDI KILE KUMKATAA YULE BWANA. Tusameheane tukae pamoja tujenge chama, lakini badala yake bado wanaendelea kumpaka matope profesa wa watu,kana kwamba wao walikua sahihi kumleta lowasa na hakijawatokea kitu. Mwisho wa yote nimefurahi kuona CUF inainuka wajumbe wa kila mikoa wamefika na inaonesha kabisa somo LIMEELEWEKA. PAMOJA NA PROF. LIPUMBA 2020