Prof. Lipumba: Hali ya uchumi Tanzania hairidhishi

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema hali ya uchumi Tanzania hairidhishi na kwamba wananchi wanaishi kwenye maisha yasiyokua bora kinyume na matarajio.

Profesa Lipumba ambaye pia ni mbobezi wa uchumi ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 13, 2019 Unguja visiwani Zanzibar wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho katika mkutano maalumu uliofanyika Amani mjini hapa.

Amesemea hivi sasa maeneo mengi ya Tanzania hakuna mzunguko mzuri wa fedha hali ambayo imesababisha Watanzania walio wengi mijini na vijijini kuishi kwenye mazingira ya umaskini.
Hata hivyo, Profesa Lipumba amesema uwepo wa hali hiyo haukuwagusa wananchi wa kawaida pekee bali hata wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo na ndio maana biashara nyingi hivi sasa hazifanyi vizuri.

“Wafanyabiashara wadogo wakubwa wote wako hoi taabani hivi sasa jambo ambalo linasikitisha kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania,” amesema Lipumba.

Kutokana na mazingira hayo ameleza dhamira ya chama chao ikiwa ni kuitumia fursa hiyo na kuwaeleza wananchi sababu ya wao kuchaguliwa na kushika madaraka hatimaye waweze kuondoa changamoto hiyo.

Profesa Lipumba amesema kwa changamoto hiyo ambayo imeikabili Tanzania chama chao kitahitaji kuweka wagombea bora na wenye uwezo watakaoweza kunadi sera zenye kuleta tija kwa wananchi wote.

Mwananchi
Huyu nani wa kumsikiliza ?! Hata wanyamwezi wenzie hawawezi kumsikiliza !!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili punga ndio miongoni ya miphd holder's uchwara waliodhalilisha umuhimu wa elimu.

Cc Pohamba
Pamoja na hayo asemayo ni ya ukweli. Wajibu wake ni kupaza sauti.

Jitokeze na wengine tupaze sauti, hali ni mbaya tuelekeako ni kubaya zaidi.

Binafsi namshukuru.🙏
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema hali ya uchumi Tanzania hairidhishi na kwamba wananchi wanaishi kwenye maisha yasiyokua bora kinyume na matarajio.

Profesa Lipumba ambaye pia ni mbobezi wa uchumi ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 13, 2019 Unguja visiwani Zanzibar wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho katika mkutano maalumu uliofanyika Amani mjini hapa.

Amesemea hivi sasa maeneo mengi ya Tanzania hakuna mzunguko mzuri wa fedha hali ambayo imesababisha Watanzania walio wengi mijini na vijijini kuishi kwenye mazingira ya umaskini.
Hata hivyo, Profesa Lipumba amesema uwepo wa hali hiyo haukuwagusa wananchi wa kawaida pekee bali hata wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo na ndio maana biashara nyingi hivi sasa hazifanyi vizuri.

“Wafanyabiashara wadogo wakubwa wote wako hoi taabani hivi sasa jambo ambalo linasikitisha kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania,” amesema Lipumba.

Kutokana na mazingira hayo ameleza dhamira ya chama chao ikiwa ni kuitumia fursa hiyo na kuwaeleza wananchi sababu ya wao kuchaguliwa na kushika madaraka hatimaye waweze kuondoa changamoto hiyo.

Profesa Lipumba amesema kwa changamoto hiyo ambayo imeikabili Tanzania chama chao kitahitaji kuweka wagombea bora na wenye uwezo watakaoweza kunadi sera zenye kuleta tija kwa wananchi wote.

Mwananchi
akili imeanza kumrudi sasa. jua lishazama.
 
Huyu, yaani huyu!?
Chochote asemacho siwezi kukiamini hata kama ni cha kweli. Kidendo cha kuivuruga Cuf nitamsamehe, ila itachukua mda, anivumilie.
Si huwa anaalikwa kwenye majukwaa ya Mkuu, mbona hamwambii haya. Wazalendo Wanafiki hawa.
Prof. Lipumba anapokuwa kuwa kwenye uchambuzi wa mambo ya uchumi anakuwa Professor Lipumba lakini anapokuwa kwenye siasa anabadilika kuwa Prof. Lipumbavu
 
Wakati mwingine nikimuona huwa naona kama wasomi wote wapo hivyo.Ila nakumbuka kuna wanaosoma kuelewa na wale wanaokariri.
 
Kuamini anapata hivi vyote bure au Kwa hisani ni si Kwa sababu za kisheria au kwa kuwa yuko entitled ni upuuzi mtupu na Hapo ndipo udhaifu wako wa kufikiri unapoanzia na kuendelea mbele.
Sheria boss.. waziri mkuu na makamu na Raisi wako entitled....
Sasa qualified mpuuzi ni wewe unayedhani unajua kila kitu kumbe mbulula wa nguvu 🤣🤣
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema hali ya uchumi Tanzania hairidhishi na kwamba wananchi wanaishi kwenye maisha yasiyokua bora kinyume na matarajio.

Profesa Lipumba ambaye pia ni mbobezi wa uchumi ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 13, 2019 Unguja visiwani Zanzibar wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho katika mkutano maalumu uliofanyika Amani mjini hapa.

Amesemea hivi sasa maeneo mengi ya Tanzania hakuna mzunguko mzuri wa fedha hali ambayo imesababisha Watanzania walio wengi mijini na vijijini kuishi kwenye mazingira ya umaskini.
Hata hivyo, Profesa Lipumba amesema uwepo wa hali hiyo haukuwagusa wananchi wa kawaida pekee bali hata wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo na ndio maana biashara nyingi hivi sasa hazifanyi vizuri.

“Wafanyabiashara wadogo wakubwa wote wako hoi taabani hivi sasa jambo ambalo linasikitisha kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania,” amesema Lipumba.

Kutokana na mazingira hayo ameleza dhamira ya chama chao ikiwa ni kuitumia fursa hiyo na kuwaeleza wananchi sababu ya wao kuchaguliwa na kushika madaraka hatimaye waweze kuondoa changamoto hiyo.

Profesa Lipumba amesema kwa changamoto hiyo ambayo imeikabili Tanzania chama chao kitahitaji kuweka wagombea bora na wenye uwezo watakaoweza kunadi sera zenye kuleta tija kwa wananchi wote.

Mwananchi

Propesa Pumba
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom