Prof. Lipumba: Hali ya uchumi Tanzania hairidhishi

Mh. Mwenyekiti wa Cuf kipindi Cha awamu ya nne uchumi mbaya, kipindi Cha awamu ya tano uchumi mbaya wakati miradi mingi inafadhiliwa na pesa za ndani sielewi maana ya uchumi wa nchi nisaidieni.
Gunga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu ya tano fedha za ndani zipi zinazoendesha miradi? Yaani unafuata jiwe anayosema jukwaani? Mtu anakopa mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa. Exim china na Egypy, na kuna mkopo mwingine wa trillion nne unakuja toka nje nao ni fedha za ndani? Fuatilia ripoti ya CAG uone kwa mwaka mmoja tu 2017 - 2018 tumekopa trillion ngapi? Hiyo ni mikopo ya nje na bado ya ndani ambayo ni karibia trillion nane. Yaani wewe bado unaamini story za Mzee baba anazopiga majukwaani? Mapato yameshuka sana ndio maana siku hizi hawatutajii tena wanakusanya ngapi!!! Haijawekwa sheria ya takwimu burebure tu, imewekwa kutengeneza watu wa aina yako usiopate information za kutosha na kuihoji serikali Bali utegemee watakachoimba majukwaani. Masikini Tanzania!!

Mh. Mwenyekiti wa Cuf kipindi Cha awamu ya nne uchumi mbaya, kipindi Cha awamu ya tano uchumi mbaya wakati miradi mingi inafadhiliwa na pesa za ndani sielewi maana ya uchumi wa nchi nisaidieni.
Gunga

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Intellectual Skills
 
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema hali ya uchumi Tanzania hairidhishi na kwamba wananchi wanaishi kwenye maisha yasiyokua bora kinyume na matarajio.

Profesa Lipumba ambaye pia ni mbobezi wa uchumi ameyasema hayo leo Jumamosi Aprili 13, 2019 Unguja visiwani Zanzibar wakati akizungumza na viongozi pamoja na wanachama wa chama hicho katika mkutano maalumu uliofanyika Amani mjini hapa.

Amesemea hivi sasa maeneo mengi ya Tanzania hakuna mzunguko mzuri wa fedha hali ambayo imesababisha Watanzania walio wengi mijini na vijijini kuishi kwenye mazingira ya umaskini.
Hata hivyo, Profesa Lipumba amesema uwepo wa hali hiyo haukuwagusa wananchi wa kawaida pekee bali hata wafanyabiashara wakubwa kwa wadogo na ndio maana biashara nyingi hivi sasa hazifanyi vizuri.

“Wafanyabiashara wadogo wakubwa wote wako hoi taabani hivi sasa jambo ambalo linasikitisha kwa nchi yenye rasilimali nyingi kama Tanzania,” amesema Lipumba.

Kutokana na mazingira hayo ameleza dhamira ya chama chao ikiwa ni kuitumia fursa hiyo na kuwaeleza wananchi sababu ya wao kuchaguliwa na kushika madaraka hatimaye waweze kuondoa changamoto hiyo.

Profesa Lipumba amesema kwa changamoto hiyo ambayo imeikabili Tanzania chama chao kitahitaji kuweka wagombea bora na wenye uwezo watakaoweza kunadi sera zenye kuleta tija kwa wananchi wote.

Mwananchi
Mbona Prof Lipumba anaacha kula Ruzuku za hao Watanzania anaojifanya anawaonea huruma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuamini anapata hivi vyote bure au Kwa hisani ni si Kwa sababu za kisheria au kwa kuwa yuko entitled ni upuuzi mtupu na Hapo ndipo udhaifu wako wa kufikiri unapoanzia na kuendelea mbele.
Yuko kwenye payroll... makamu mstaafu... chakula, matibabu, vacations bure
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom