Jackson Turary
Senior Member
- Jan 1, 2014
- 154
- 129
Mnyonge anyongewe mbali ila haki yake apewe pamoja na unafiki wa Profesa hapa kasema kweli
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba asema Haingii akilini gaidi na mhaini akapelekewa salamu za rambirambi tarehe 8 Julai 2021 na Rais ambaye ni amiri jeshi Mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, halafu tarehe 23 Julai 2021 Freeman Mbowe akakamatwe kwa ugaidi wa mwaka 2020.
Maana rais kila siku hupewa taarifa za usalama za nchi nzima, iweje tarehe 8 Julai 2021 Freeman Mbowe apelekewe salamu za pole za rambirambi za msiba wa kaka yake. Ina maana rais alikuwa hana taarifa za ugaidi wa Freeman Mbowe mpaka tarehe 21 Julai 2021 siku ya kongamano la CHADEMA juu ya katiba ya nchi, anahoji Prof. Haruna Lipumba.
Prof. Ibrahim Haruna Lipumba anakwenda mbali na kuhoji kuwa haiwezekani vyombo vya ulinzi na usalama kutomfahamisha Rais juu ya mipango ya kuwakamata watuhumiwa wa mipango ya ugaidi wa kulipua sehemu mbalimbali, njama za kuua viongozi na kufanya uhaini za mtuhumiwa Freeman Mbowe kiasi rais atatuma pole kwa mtu Mwenye kutuhumiwa nzito ambaye yupo mbioni kutiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka mazito ya ugaidi na uhaini.