Prof. Lipumba anusurika kipigo, akimbilia msikitini kujinusuru!

Kasimba G

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,428
2,611
Habari wanajamvi!

Kwa tetesi nilizozipata kumbe Bwana yule alienda Moro kuvuruga shughuli halali za kisiasa Morogoro.

Amesalimiwa na kichapo!

----
prof-lipumba-new-jpg.462910

MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba amenusurika kupigwa na vijana wanaoaminika kuwa ni wa Ukawa wakati akitoka kwenye mkutano wa kampeni mjini Morogoro.

Katika vurugu zilizotokea juzi jioni wakati vijana wa Ukawa na kikundi cha ulinzi cha CUF (blue guard) cha Dar es Salaam wakiwa na Profesa Lipumba walikuwa wakitoka kwenye mikutano ya kampeni maeneo tofauti walipokutana barabarani na kuanza kurushiana maneno na hatimaye kupigana.

Katika vurugu hizo, vijana wa Ukawa waliwazidi wenzao wa blue guard na Profesa Lipumba kulazimika kukimbilia kwenye Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja ili kujinusuru.

MTANZANIA lilishuhudia ghasia hizo zilizodumu kwa takribani saa moja na nusu ambapo baada ya Profesa Lipumba kukimbilia msikitini hapo, wafuasi wa Ukawa walibaki nje mpaka polisi walipofika na kuwatawanya.

Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonce Rwegasira alikiri kutokea kwa vurugu hizo ambapo alisema wafuasi watatu wa CUF walijeruhiwa.

Alisema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini walioanzisha vurugu hizo ikiwa ni pamoja na kuweka doria kali katika mikutano ya vyama vya siasa.

Profesa Lipumba hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, baada ya simu yake kutokuwa hewani jana.

Chanzo: Mtanzania
 
Kama kachapwa bora maana ndicho alichokuwa anakitafuta siku nyingi
 
PROF  LIPUMBA new.jpg

Kazi aliyopewa lipumba na watawala kaifanya kwa usahihi wampe tuzo kabisa
 
Tuzo ya nini wakati analipwa mamilioni ya pesa tena pesa unachukuliwa Hazina kienyeji tu,pesa anayopewa Lipumba kwa ajili ya kudhoofisha ukawa na kuua CUF ingeweza kujenga Hosptal kubwa kama Apolo Dodoma na kuwajili madaktari toka india wagonjwa wa Africa wangekuja Dodoma kutibiwa na mji ungekuwa kwa kasi lakini CCM wamekufa wameoza kwa Lipumba wanachunwa buzi bila kujielewa.
 
Lipumba kwa sasa anatumia robo ya pesa inayokusanywa na TRA yaani kwa sasa kamkamata mkulu habanduki kila siku jioni wanakuwa pamoja ni mshauri wake mkuu kwenye Uchumi na mbinu za kudhoofisha upinzani na siasa za maji taka.
 
Siku CUF wakija kumfanyiahivyo maMvi au DJ msiseme wametumwa na CCM.
 
Mwenyekiti wa Cuf anayetambulika na msajili wa vyama Lipumba.Amenusurika kichapo huko morogoro baada ya kukimbilia msikitini.
Lipumba alikutana na kadhia hiyo baada ya kumaliza kuhutubia mkutano.
 
Back
Top Bottom