Penguini
JF-Expert Member
- Apr 24, 2013
- 377
- 293
Prf Ibrahim Haruna Lipumba, amekuwa mwanasiasa aliyevuma miaka ya nyuma kdg, licha ya kuwa alikuwa mwenyekiti wa CUF amewahi kugombea nafasi ya kuwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na hilo wote tunajua,
Mwaka Jana (2015) katika harakati za kuelekea uchaguzi Lipumba alikuwa mwenyekiti mwenza katika umoja wa katiba ya wananchi, (UKAWA) ulioundwa chini ya ushirikiano wake na viongozi wa vyama vingine vya upinzani, sina haja ya kulielezea sana hili najua linafahamika, ulipofika wakati wa kugombea u Rais ukawa walikubaliana kumsimamisha mgombea mmoja;
Edward Lowassa aliyekuwa mgombea u Rais mwana CCM baada ya kukatwa kule akahamia kwenye umoja wa UKAWA kisha wakampa nafasi ya kugombea u Rais na viongozi wanaounda umoja huo prf. Alikuwa mmoja wao.
Muda mfupi mbele Lipumba aliandika barua ya kujivua uenyekiti na kukiacha chama chake alichokiunga kwenye ukawa (kama mwenyekiti mwenza), katika hali ya sintofahamu, lakini pia alipotea kabisa katika medani za siasa.
Sasa ni miezi kadhaa kuelekea mwaka, amerudi katika medani za siasa
na si tu kurudi kama mwanachama Bali kwa kuutaka uenyekiti aliojivua katika muda wa kuelekea uchaguzi na kukiacha chama katika hali ya taharuki.
Baada ya viongozi waliopo "kumkata" (katika uchaguzi wa viongozi wapya) anatangaza ubavu wa uwepo wake kama kiongozi.
Je CUF, wanaweza kumpokea vyema na kumpa madaraka tena?
Na je, kiongozi wa aina hii kama akipewa majukumu ya kuliongoza Taifa si hatari hii?
Je kama wakati alipogombea urais kura zingetosha kumpa ushindi, Tanzania ingekuwa katika hali gani?
Nadhani sasa ufike wakati vyama vya siasa viongeze mbinu za kuchuja au kutafuta wagombea. Ni afadhali uchaguzi ufanyike bila chama kuweka mgombea kuliko kuteua mgombea wa sampuli hiyo.