Prof. Lipumba amrarua Trump, alipongeza Bunge la Marekani

CUF Habari

Verified Member
Dec 12, 2019
239
250
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

CUF- Chama Cha Wananchi kimepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya vurugu zilizofanywa na waandamanaji waliovamia Bunge la Marekani kwa Lengo la kulilazimisha Bunge la Marekani kubadilisha Matokeo ya Uchaguzi wa Rais wa Novemba 3, 2020 yaliyompa Ushindi Joe Biden. Waandamanaji hao walivamia Bunge Jumatano tarehe 6 Januari 2021 wakati wabunge wakikutana kuthibitisha ushindi wa Rais Mteule Joe Biden.

Vurugu hizo zimefanyika baada ya Rais Donald Trump kuwahamasisha wafuasi wake waende Bunge la Marekani kwenye mkutano wa hadhara mkubwa uliofanyika jijini Washington D.C. siku hiyo ya Jumatano. Uvamizi wa Bunge umesababisha maafa kadhaa ikiwa ni pamoja na vifo vya watu wanne - mwanamke mmoja aliyefariki kwa kupigwa risasi huko Capitol na wengine watatu walifariki wakipatiwa matibabu.

Matukio katika Bunge la Congress ni fedheha kwa Marekani. Pamoja na mapungufu yake ya kihistoria hasa ukandamizwaji wa Wamarekani wenye asili ya Afrika waliouzwa Marekani kama watumwa na ukandamizaji wa Wamarekani wa asili, Marekani ni muasisi wa demokrasia ya kisasa ambapo watunga sheria na viongozi wakuu wa serikali wanachaguliwa na wananchi. Vurugu za aibu zilizotokea katika Bunge la Marekani zitatumiwa na madikteta wa nchi nyingine kuhalalisha udikteta wao na kupaka matope mfumo mzima wa demokrasia.
Vurugu hizo zinadhoofisha uwezo na hadhi ya Marekani kulaani vitendo vinavyokandamiza demokrasia katika nchi nyingine duniani.

Ni muhimu kuwepo na mabadiliko ya amani ya utawala. Trump na wafuasi wake wanapaswa kukubali maamuzi ya wapigakura wa Marekani na kuacha kuikanyaga Demokrasia.

CUF- Chama Cha Wananchi ni Chama kinachoamini katika Haki Sawa kwa Wote. Demokrasia ni Haki ya msingi. Mamlaka ya kuongoza nchi yatoke kwa Wananchi wenyewe.

Tumefarijika na msimamo wa Bunge la Marekani kukamilisha wajibu wake wa kikatiba wa kumthibitisha Rais Joe Biden na Makamu wa Rais Kamala Harris ambao wataapishwa tarehe 20 Januari mwaka huu.

CUF- Chama Cha Wananchi kinatamani kuona Demokrasia na Haki Sawa kwa Wote vikitamalaki duniani kote na sauti ya wapiga kura ikiheshimiwa.
Tuna matumaini utawala wa Rais Biden utarejesha hadhi ya Marekani kimataifa ya kuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za binadamu na ujenzi wa demokrasia duniani kote.

Haki Sawa na Furaha kwa Wote!

Imetolewa leo Januari 7, 2021 na:

Prof. Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti Taifa
CUF - Chama Cha Wananchi
 

The Underboss

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
3,580
2,000
Lipumba anazungumziaje yeye kuvamia mkutano wa CUF na kufanya fujo? Ana tofauti gani na hao watu wa republican?
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,437
2,000
Lipumba ameshachina maana hakuna anayemsikiliza tena.
 

pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
12,072
2,000
Huyu Propesa-pumba kwani yeye ni nani? atakuwa ameongelea kutoka Buguruni malapa!
Sitaki mwanangu asome kihivi na aje kuwa hivi kabisa!
 

renamaizo

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
1,430
2,000
Ya nchin kwako yamekushinda unaenda kuongea kiswahili wakat ata io lugha hawaijui tena mbaya zaid hata ww mwenyewe hawakujui

Kaa kimya
 

Gutapaka

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
257
250
Naomba mumtumie na Trump kule Twitter na majibu mtuletee.

Yule jamaa akili zake Ni shida...
 

Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,763
2,000
MWenye platform mr Tundu lisu huko yeye kakaaa kimya bila kumtumia Robert Amsterdam kuwatwanga barua wamalekani, au anaogopa kugurushwa huko kama wala majaji wa ICC?
Yeye ana platform gani ya kuwasilisha ujumbe huo kwa wahusika.. Kuna watu wanavuta aisee..
 

Kapumpuli

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
959
1,000
Yaani Lipumba ana effect gani kwa USA, hadi ashtushwe na taarifa za Trump... Na anaibuka kuzungumza....

Aache Utopolo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom