Prof. Lipumba alipounguruma Tangamano Tanga uchaguzi mkuu 1995

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,906
30,247
LIPUMBA%2BSAME%2B1995%2B-%2BCopy.jpg
Prof. Lipumba akizungumza katika mkutano wa kampeni ya urais Same Uchaguzi Mkuu 1995

Picha hiyo hapo juu ni Prof. Ibrahim Haruna Lipumba, msomi wa Chuo Kikuu Cha Stanford Marekani, akihutubia mkutano Same wa kampeni ya urais Uchaguzi Mkuu 1995. Lipumba alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CUF.

Prof; Lipumba alikuwa akitokea Moshi alifanya mkutano mwingine siku hiyo hiyo Muheza lakini mkutano uliovunja rekodi ulifanyika Tangamano Tanga siku ya pili yake. Wenyeji walituambia kuwa katika historia ya mji wao hawajapata kuona umma mkubwa kama ule. Baada ya mkutano ule Prof. Lipumba na waliokuwa katika msafara wake walifanyiwa dhifa kubwa nyumbani kwa marehemu Mama Ummy binti Anzuwani, Ngamiani.

Kundi kubwa la wananchi waliizunguka nyumba ile ya Bi. Mkubwa huyu wakiimba nyimbo za kuwahamasisha watu waunge mkono CUF. Hali ilikuwa ngumu kwa CCM ikabidi Mwalimu Nyerere aje Tanga kusaidia. Ilibidi Mwalimu Nyerere aende Tanga kwa sababu katika hotuba yake katika viwanja vya Tangamano, Prof. Lipumba alizungumza na nyoyo za watu wa Tanga.

Hali ya uchumi wa Tanga ilikuwa mbaya, viwanda vyote vilivyokuwa mjini hapo vilikuwa vimekufa, mkonge ambao ndiyo lilikuwa zao kuu ulikuwa umekufa na mengi ya mashamba yalikuwa katika hali duni sana. Prof. Lipumba akiwa mchumi bingwa aliwapitisha katika ilivyokuwa Tanga katika miaka ya nyuma.

Prof. Lipumba aliwauliza Tanga, taarab ya Shakila iliyokuwa ikivuma wapi imekwenda, akawauliza tena zile timu kali za mpira za Tanga za Coastal Union na African Sports na wachezaji mashuhuri kama Abdallah Luo, Hemed Seif, Mbwana Abushir, John Limo, Saleh na Omari Zimbwe ule moto umefia wapi. Watu walikuwa kwa hakika wameguswa nafsi zao na walikuwa wakishangilia kila nukta aliyoigusa Prof. Lipumba kuhusu hali ya Tanga. Ikawa lazima Mwalimu Nyerere afike Tanga kuokoa jahazi lililokuwa linazama.

LIPUMBA%2BTANGA%2B1995.jpg
Nyumbani kwa marehemu Mama Ummy Bint Anzuani kushoto ni Juma Duni, Prof. Lipumba na wenyeji wake.

Katika mkutano wa Mwalimu Nyerere Tangamano alisema maneno mengi ambayo kwa hali ya sasa kuhusu, ‘’uchochezi,’’ ni vigumu kwangu kuyaandika na kufanyia uchambuzi. Kwa mukhatasari Mwalimu Nyerere alionya kuhusu ''kuchanganya dini na siasa'' na ''umwajikaji wa damu.'' Leo nikiangalia nyuma tulikotoka miaka 20 iliyopita na khasa baada ya CUF kupata mafanikio makubwa Tanga katika uchaguzi wa 2015 picha ile ya 1995 inanijia kwa majonzi makubwa. Hali ya Tanga ilikuwa inashabihiana na hali ya Tanga 1955 wakati wazalendo akina Hamisi Kheri, Mohamed Kajembe, Sheikh Rashid Sembe, Mwalimu Kihere, Mzee Makoko kwa kuwataja wachache walipokuwa wanajikusanya kujiondoa katika dhulma ya utawala wa Waingereza.

Baada ya dhifa ile wakati wa kuondoka Mama Ummy alitukabidhi keki iliyotengenezwa na binti yake Ummy mwenyewe makhsusi kwa ajili ya Prof. na tuliibeba hadi White Rose Hotel tulipofikia. Usiku ule ule Mariam Shamte wa BBC, London alifika hotelini kufanya mahojiano na Prof. Lipumba na Juma Duni mgombea mwenza na asubuhi Prof. Lipumba alisikika akinguruma BBC Idhaa ya Kiswahili. Hakika Prof. mtu ambae mwezi mmoja tu uliopita hakuna mtu aliyekuwa akimfahamu sasa akawa midomoni mwa wananchi wengi.

PROF%2BLIPUMBA%2BNA%2BMARIAM%2BSHAMTE%2BBBC.jpg

Mariam Shamte wa BBC akimhoji Prof. Lipumba
Asubuhi tuliikata keki ya Mama Ummy na kuila wakati wa kifungua kinywa. Furaha ilikuwa kubwa mno wala haisemeki...msingi mzuri wa siku za baadae ulikuwa umewekwa na baada ya miaka 20 CUF iliiangusha CCM Tanga...

wMoeAdf2-IQ4926S64_MlJGvUkmCOfbnxs0mI6Bj9MtJHXScNJ0C8wgk2dzg5oHXujNM746RPK3B3OWDUzX-7i6Vzix9gyFnDCki-90Fy9y0r5e0-fAxw7JVDSXhkWFX4yaP92Qk25TCssGWGHzqrZq6Hhdra8B6O93Kb6CQVsaZ23thc406iGx43O6nR7pmJJw2c2hK2DrMf_BImCsWlHOEhuwsJdh3rqRa92mG84dXrx9guc3Qd37LIJInJoXKvsHxkN6c4tO-v8Gup_E_3omw-eG6WVb_P7wGKvs5t4iQlzNAQHYXzxLifB5miAu7QbD2gaMGVuZyE93aRPJr2HksJeYn4pYoGQC9qT-Bv9OsiCLcgu6AH5C8hGqd5CdnhNpyZuIyJVrh_JXluUFVwN9Rq5PZ7AKDjCTQVdCD6xfsI8zxlH-3eOvlJ46xle2W7dx_zuShAdxuUerI1s0U3mLCJ1sMWT4mspPzuEUV7MqJM7If_HxLcWf4fp8oxRS1OslSczgPzU689-d6BG1xsY_RVWRPLlnlcX7NHOT2pkSFaFT15eyoAoYE3g6P2JAUL1swOUYAN4RZG2nSi_wyEc6iZ3lgFVhlVNAcywYZ58XMvSV8LRkCcQ=w1133-h696-no

Kushoto: Prof. Ibrahim Lipumba, Shekue, Mama Ummy bint Anzuani na Ummy
Msiba mkubwa ni kuwa nguzo za CUF zilizojengwa kwa kipindi cha miongo miwili kwa jasho na vumbi na katika hali ngumu sana inaelekea kuna nyundo kubwa na nzito ikizipiga ili kuzivunja jengo lipate kuanguka.

Historia hujirudia In Shaa Alah ikitokea nafasi nitakileta hapa kisa cha namna TANU ilivyoingia Tanga kwa kishindo kama hiki cha Prof. Lipumba siku Mwalimu Nyerere na Bi. Titi Mohamed walipokwaa jukwaa katika viwanja vya Tangamano kuwaita wananchi katika TANU wajikomboe na utumwa wa Waingereza.

Wakoloni hawakukaa kimya kupitia United Tanganyika Party (UTP) walitengezeza nyundo nzito kuivunja TANU...
 
ila maneno ya mwalimu itakua ni nukuu alizosema yeye na sio ulizo sema wewe sasa sioni sababu usiziweke hapokwa kuogopa kile kiitwacho "uchochezi"
 
Sheikh Mohammed Mimi ni mmoja wa wafuasi wako ila kwa hili nitakupinga kidogo.. Niwie radhi.

Si kweli kwamba misingi aliyoiweka huyu re professor "bwana yule" ndiyo ilisaidia kubomoa ccm 2015..hapana ni ukweli uliowazi kuwa nguvu ya Edward ngoyai lowawsa ndiyo ilisaidia Sana kubomoa ccm 2015 nakufanikisha cuf kupata madiwani na wabunge na sio tanga tu..bali nchi nzima.

Kama unavyodai 1995 prof "msaliti mkubwa" kuwa alijenga misingi..hebu tusaidie hiyo 1995 cuf ilipata madiwani wa ngapi na wabunge wangapi? Mwaka 2000 bado hili lisaliti likiwepo cuf ilipata wabunge wa ngapi na madiwani wangapi?2005 je Chini ya huyu prof uchwara "mdini mkubwa" cuf ilipata viti vingapi tanga??Kama kweli yeye ndiye aliweka misingi imara??

Na sasa jiuluze..2015 baada ya yeye kutoka nduki..na kikimbia chama na kwenda kuponda "maraha" Kigali baada ya kuhongwa.na kukiacha chama yatima..je chama kilipata wadiwani wangapi na wabunge wangapi tanga??

Najua utajifanya huna jibu..jibu ni kuwa baada ya yeye kukimbia chama hadharani..kwa hoja za kitoto,za kipumbavu kabisa .. Chama kilisimama imara..na ujuo wa ndugu lowwsa ukawa ikawa chachu ya ushindi.

Nikusaidie tu..yeye hoja yake ya kijinga kuwa lowwasa hafai..yeye ndiye alimpokea na kwenye press ya buguruni aliongea...MTU anaekuaja kwenye ukawa na aka busti ukawa kutoka 1 kwenda 1000 utasemaje hafai??

Kwenye utawawala wake tangu akiwa chairman wa cuf..huyu prof wako hajawahi pata zaidi ya wabunge wawili(2)) kwa miaka 20 ya usultani wake..Leo akaja Mzee Edo ukawa..kwa miezi 3..tu..jiulize cuf Ina madiwani wangapi na wabunge wangapi.

Kama kweli haongwi kutuvuruga..basi amerogwa..ama Ana mashetani na anahitaji kupigiwa ngoma ya "maswezi".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakusoma,
Ahsante nimekusoma lakini hayo yote uliyoandika hayamo katika
niliyosema mie.

Mie nimekwenda kwenye kumbukumbu zangu na Prof. Lipumba
1995.

Sijakusudia msingi wa kujengwa siku moja.
Tafadhali hebu nisome tena.

Juu ya hayo yote umeleta hoja za kufikirisha wala hili halina wasiwasi.
 
!
!
Profesa ana mchango mkubwa sana kwenye Ongezeko la wageni wanaofanya utalii nchini. Hawaamini kama kuna profesa wa hivi. Ni ajabu lingine la dunia
 
Wakusoma,
Ahsante nimekusoma lakini hayo yote uliyoandika hayamo katika
niliyosema mie.

Mie nimekwenda kwenye kumbukumbu zangu na Prof. Lipumba
1995.

Sijakusudia msingi wa kujengwa siku moja.
Tafadhali hebu nisome tena.

Juu ya hayo yote umeleta hoja za kufikirisha wala hili halina wasiwasi.
Sheikh wangu nakusoma Sana Sana na huwa nakuelewa.tena huwa na print kabisa mabandiko yako na kuyahifadhi.

Ila kwa hili sheikh msingi wa hoja yako ni kuwa mafanikio yoote ya cuf sasa ni msingi aloujenga lipumba since 1995 .

Mimi nikasema si kweli hata kidogo..ingekuwa hivyo 2000,2005,2010 tungeona mafanikio ama dalili za hayo mafanikio...

Tofauti yake ni kuwa kuondoka kwake ni Kama "nuksi" hivi iliondoka na cuf ikapata mafanikio makubwa yeye akiwa hayupo.

Kurejea kwake kibabe ni Kama "nuksi"sasa imerudi tena..ama nakuhakikishia Mzee wangu huyu bwana anakiua chama na panapo uzima inshallah 2020 cuf haitapata hata diwani wa dawa.

Hakujenga chama ila alichokuwa anafanya ni kuki involved chama na dini." Ambavyo mbinu hiyo haikuwa na mafanikio .rejea ile video clip akikaribishwa na sheikh basaleh kutoa mawaidha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ila maneno ya mwalimu itakua ni nukuu alizosema yeye na sio ulizo sema wewe sasa sioni sababu usiziweke hapokwa kuogopa kile kiitwacho "uchochezi"
Mr. Q,
Hizi ni nyakati ngumu sana kwa watu wenye fikra huru.

Itasaidia nini kutoa hoja hizo kuwa unakuu maneno yaliyosemwa
ukiwa tayari uko Segerea na mahakama inasema inakuweka
huko kwa usalama wako kukukinga na wananchi wenye hasira kali
wasikudhuru?
 
mimi napinga mojakwamoja kama ujie wa Lowasa ndio uloifanya cuf ifanye vizuri kwenye uchaguzi.
Cuf wamekua wakiibiwa kura na ccm kwenye ngome zake kwenye chaguzi nyingi. Ushindani mkali wa uchaguzi safari hii ndo uloifanya ccm ishindwe kutengeneza mazingira mazuri kila sehem yakupiga bao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom