Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Tarakea, Rombo: Mkinichagua kuwa Rais nitawaunganisha Watanzania wote, kukuza uchumi na kufuta umasikini

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
NITAWAUNGANISHA WATANZANIA WOTE" PROF. LIPUMBA

Lipumba.jpg

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CUF, Prof. Ibrahim Haruna Lipumba amesema endapo atachaguliwa kuwa rais atahakikisha anawaunganisha watanzania.

Pia, Prof. Lipumba amesema endapo watanzania watampa ridhaa ya kuwa Rais atahakikisha anakuza uchumi na kufuta umasikini,

Ukuaji wa uchumi wa Tanzania haujaambatana na kasi kubwa ya kupungua kwa watu masikini. Idadi ya watu masikini kwa kutumia kipimo cha taifa cha umasikini (mtu mzima kutumia shilingi 50,000/ au zaidi kwa mwezi) imeongezeka toka watu milioni 12.3 mwaka 2011 na kufikia watu milioni 14 mwaka 2018. Kwa kutumia kipimo cha kimataifa cha umaskini, Watanzania zaidi ya milioni 27 ni masikini.

Utafiti uliofanywa na serikali mwaka 2016 kuhusu umasikini wa watoto (Child Poverty in Tanzania) ulibaini kuwa asilimia 74 ya watoto wa Tanzania wanaishi katika mazingira ya umaskini kwa tafsiri pana inayojumuisha lishe, afya, hifadhi iliyo salama, elimu, mazingira, maji na makazi.
 
maliza salama baba upewe ruzuku yako urudi zako nyumbani ...
 
Dhambi ya kumdhulumu Mzee Mapalala chama chake haitawaacha salama. Ukweli ni kwamba mnachezea ruzuku ya mwisho mwisho mliyo mdhulumu Maalim. Baada ya huu uchaguzi mnaenda kujiunga na kundi ya NCCR Mageuzi kama vyama vilivyojifia kibudu. Nendeni mkatubu kwenye kaburi la Mapalala kabla halinhaijawa mbaya zaidi
 
Back
Top Bottom