Uchaguzi 2020 Prof. Lipumba akiwa Kigoma Kaskazini: Nikiwa Rais nitaimarisha mazingira ya uwekezaji, kufanya biashara na ujasiriamali

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Screenshot_20200922-190453.png
Screenshot_20200922-185234.png

NIKIWA RAIS NITAIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI,KUFANYA BIASHARA NA UJASIRIAMALI"PROF.LIPUMBA"

KIGOMA KASKAZINI

Mazingira ya kufanya bishara Tanzania ni magumu sana.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Benki ya Dunia ya mazingira ya kufanya biashara ya mwaka 2020 – (Doing Business 2020), Tanzania ni nchi ya 141 kati ya nchi 190.

Rwanda ni nchi ya 38 na Kenya ni nchi ya 56. Idadi ya kampuni mpya zinazosajiliwa kila mwaka zimepungua kutoka 8,890 mwaka 2015 na kufikia 5,278 mwaka 2018.

Ili mazingira ya biashara nchini yawe rafiki zaidi na yenye gharama nafuu inabidi kuwepo na utashi wa kisiasa tokea uongozi wa juu wa nchi. Ni lazima uongozi wa juu wa nchi uridhike kuwa kuwa sekta binafsi ni muhimili muhimu wa uchumi wa nchi.

Serikali isiwabughudhi wafanyabiashara na wawekezaji, alimuradi sekta binafsi inaheshimu na kufuata sheria za nchi. Kauli za vitisho na kuingilia kati shughuli za kibiashara kama ulivyofanyika kwenye ununuzi wa korosho kunapunguza imani ya sekta binafsi kuwa unaweza kuwekeza na kufanya biashara kwa taratibu na kanuni zinazotabirika.
 
Back
Top Bottom